Back

ⓘ Familia - Familia, Familia, biolojia, takatifu, nyuklia, Sheria ya Familia, Detepwani, familia, Nyoka, Bibi, Kizazi, Mama, Mitara, Mjane, Mjomba, Mpwa, Ndugu ..
                                               

Familia

Familia ni kikundi cha watu wanaokaa pamoja kama baba, mama na watoto. Kikundi hicho mara yingi ni sehemu ya kundi kubwa zaidi la ukoo unaounganisha watu wenye asili katika uzazi wa pamoja.

                                               

Familia (biolojia)

Familia ni ngazi katika uainishaji wa kisayansi wa viumbehai. Familia ya wanyama au mimea hujumlisha spishi mbalimbali zilizo karibu. Kwa mfano paka-kaya ni spishi mojawapo pamoja na spishi 41 nyingine ndani ya familia ya Felidae inayojumlisha paka pamoja na chui, simba, tiger n.k. Ndani ya familia kuna jenasi mbalimbali zinazojumlisha spishi za karibu zaidi; kila familia ni sehemu ya ngazi ya juu zaidi inayoitwa oda. Familia ya Felidae wanyama wanaofanana na paka ni sehemu ya oda ya Carnivora yaani wanyama walanyama. Kwa kawaida majina ya kisayansi ya kila familia huishia kwa - "idae" kam ...

                                               

Familia takatifu

Familia takatifu katika Ukristo ni hasa ile iliyoundwa na Mtoto Yesu, Bikira Maria na mtakatifu Yosefu. Kwa imani ya Wakristo ni kwamba Mungu alipomtuma Mwanae pekee kujifanya mtu hakutaka azaliwe nje ya familia, kwa kuwa hiyo ndiyo mpango wake asili kwa ajili ya watu tangu alipoumba Adamu na Eva akawabariki wazaliane. Heshima kwa Familia takatifu katika Kanisa Katoliki ilianzishwa rasmi na Fransisko wa Laval, askofu wa kwanza wa New France Kanada katika karne ya 17.

                                               

Familia nyuklia

Familia nyuklia ni familia iliyoundwa na wazazi wawili na watoto wao. Ni tofauti na familia pana, inayohusisha ndugu wengi wa wazazi, na aina nyingine za familia.

                                               

Sheria ya Familia

Sheria za familia ni sehemu za sheria ambazo zinahusika na masuala ya familia na mahusiano ya ndani ikiwa ni pamoja na: Kikomo cha uhusiano pamoja na talaka, mali, wajibu wa mzazi kwa watoto). Masuala yanayojitokeza katika ndoa, ikiwa ni pamoja na dhuluma, uhalali, watoto, na dhuluma kwa mtoto. Asili ya ndoa, vyama vya muungano, na ushirikiano wa nyumbani; Sheria za familia zinaweza pia kuashiria mkataba wa ndoa katika imani ya Kiislamu, ambayo inaruhusu wanaume kuoa wake hadi wanne.

                                               

Detepwani (familia)

Detepwani ni ndege wa nusufamilia Cerylinae katika familia Alcedinidae. Spishi kubwa zinaitwa mkumburu au zumbulu. Wanafanana na midiria lakini spishi nyingi ni wakubwa zaidi na zote zina kishungi. Kwa kweli baina ya spishi hizi kuna zile kubwa kabisa za familia hii, lakini American pygmy kingfisher ni mdogo sana. Takriban spishi zote zina rangi ya majani ya metali mgongoni na nyekundu kidarini, lakini detepwani wa kawaida ni mweusi na mweupe tu. Detepwani hubobea katika kukamata samaki lakini hula gegereka, vyura na wadudu pia. Huchimba tundu katika ukingo wa mto ambalo ndani lake jike hu ...

                                               

Nyoka

Nyoka ni watambaachi au reptilia wasio na miguu. Kuna takriban spishi 3.000 duniani: wako kwenye mabara yote nje ya Antaktiki na Aktiki. Kama reptilia wote wana damu baridi na ngozi ya magamba. Wote ni wala nyama na spishi mbalimbali hutumia sumu kwa kuvionda lakini nyoka walio wengi hawana sumu wanashika windo kwa miili yao au kwa mdomo tu. Wote wanazaa kwa njia ya mayai lakini spishi kadhaa hubeba mayai ndani ya mwili hadi wadogo wamekua tayari. Mijusi wasio na miguu wanafanana sana na nyoka lakini nyoka hawana makope machoni wala masikio ya nje. Kuna nyoka wadogo wenye sentimita kumi tu ...

                                               

Bibi

Bibi kwa mjukuu wake ni hasa mama wa mzazi wake mmojawapo. Katika DNA anachangia 25%. Inakadiriwa kwamba miaka 30.000 iliyopita idadi ya watu waliofikia umri wa kuona wajukuu wao iliongezeka sana na kuwezesha ushirikishaji wa ujuzi na mangamuzi mbalimbali kuliko awali. Pia bibi anaweza kushika nafasi ya mama ikiwa huyo hayupo k.mf. amekufa na kumfaidisha mtoto kimalezi. Hata kama mama yupo, bibi anaweza kutoa mchango mzuri katika makuzi ya mtoto. Mwanamke aliyewahi kuliko wote kupata mjukuu ni Rifca Stănescu, a gypsy wa Romania, aliyejifungua mara ya kwanza akiwa na miaka 12, halafu binti ...

                                               

Kizazi

Kizazi ni kundi la watu waliozaliwa takriban wakati wa pamoja na waliokuwa watoto na vijana pamoja. Dhana hiyo inafanana kiasi fulani na "rika" katika jamii za Kiafrika lakini haitegemei sherehe za pamoja jinsi ilivyo katika rika. Kwa lugha nyingine kizazi ni pia watu ndani ya familia au ukoo ambao wamekuwa wazazi takriban wakati moja kwa kutofautisha na kizazi cha mababu waliotangulia au kizazi cha viijana kinachofuata. Kutokana na matumizi haya neno latumiwa pia kwa kutaja kipindi cha miaka kadhaa, mara nyingi miaka 20 au 25.

                                               

Mama

Mama ni mwanamke anayemlea mtoto hasa aliyemzaa mwenyewe, lakini pengine sivyo, lakini anamlea. Upande wa pili anatarajiwa kuwepo baba, yaani mwanamume aliyeshirikiana naye katika kuzaa au anashirikiana naye katika kulea. Wale ambao si wazazi wanaitwa ka kawaida "mama wa kambo" na "baba wa kambo". Katika historia na utamaduni wa makabila na mataifa mengi, umama ni sifa maalumu ya mwanamke inayotangaza kuwa amekomaa na kukamilika kwa kuendeleza uhai wa binadamu kadiri anavyoelekezwa na umbile lake upande wa mwili na wa nafsi. Wastani wa idadi ya watoto wanaozaliwa na mwanamke mmoja unatofau ...

                                               

Mitara

Mitara ni hali ya watu zaidi ya wawili kuishi katika uhusiano wa kindoa. Hali hiyo ilikuwa ya kawaida barani Afrika, ambapo mwanamume mmoja aliweza kuwa na wanawake zaidi ya mmoja, lakini kwa sasa inazidi kupungua. Ya nadra zaidi ni hali ya wanaume kadhaa kuchanga mwanamke mmoja. Baadhi ya nchi zinakubali hali hiyo, lakini nyingi zinaikataza. Vilevile baadhi ya dini zinakubali mitara, hususan Uislamu, lakini nyingine zinaikataza, hususan Ukristo. Katika Biblia tunakuta maendeleo ya ufunuo kuhusu hali hiyo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya.

                                               

Mjane

Mjane ni mtu aliyewahi kuwa na mwenzi wa ndoa, halafu akafiwa asioe tena ama asiolewe na mwingine. Ni tofauti na yule asiyewahi kufunga ndoa na yule aliyetoa ama kupata talaka anayeitwa mtaliki.

                                               

Mjomba

Mjomba ni jina ambalo mtoto anamuita mwanamume ambaye ni ndugu wa mama yake. Upande wa pili, mjomba anamuita mtoto huyo "mpwa". Ukilinganisha na lugha za Ulaya, zile za Kibantu zinazingatia zaidi umri na hasa jinsia za wazazi na ndugu zao. Hivyo, kwa Kiingereza "nephew" linaweza kumaanisha "mpwa" lakini pia "mtoto" ikiwa anayesema ni wa jinsia ileile ya mzazi. Hivyo, anayeitwa kwa Kiingereza "uncle" anaweza akaitwa kwa Kiswahili "mjomba", lakini "baba mkubwa" kama ni kaka wa baba au "baba mdogo" kama ni mdogo wa baba. Vilevile neno "aunt" linaweza kumaanisha "shangazi" dada wa baba, "mama ...

                                               

Mpwa

Mpwa ni jina ambalo mwanamume anamuita mtoto wa dada yake. Upande wa pili, mpwa anamuita mwanamume huyo "mjomba". Ukilinganisha na lugha za Ulaya, zile za Kibantu zinazingatia zaidi umri na hasa jinsia za wazazi na ndugu zao. Hivyo, kwa Kiingereza "nephew" linaweza kumaanisha "mpwa" lakini pia "mtoto" ikiwa anayesema ni wa jinsia ileile ya mzazi. Tena anayeitwa kwa Kiingereza "uncle" anaweza akaitwa katika Kiswahili "mjomba", "baba mkubwa" kama ni kaka wa baba au "baba mdogo" kama ni mdogo wa baba. Vilevile neno "aunt" linaweza kumaanisha "shangazi" dada wa baba, "mama mkubwa" kama ni mkub ...

                                               

Ndugu

Ndugu ni hasa mtu anayechanga na mwingine mzazi mmojawapo, lakini pia anayechanga naye babu, bibi au asili moja. Kwa kawaida uwepo wa ndugu katika maisha ya binadamu unasaidia kukua vizuri, ingawa pengine unaweza ukasababisha matatizo. Katika Kiswahili, ndugu wa kiume anaitwa kaka, hasa kama ni mkubwa kuliko mhusika. Hapo mara nyingi anakubalika kuwa na haki za pekee na majukumu kwa wadogo wake na dada zake.

                                               

Shangazi

Shangazi ni jina ambalo mtoto anamuita ndugu mmojawapo wa familia ambaye anajulikana kama dada wa baba, awe ni mkubwa au mdogo vilevile kwa umri. Ukilinganisha na lugha za Ulaya, zile za Kibantu zinazingatia zaidi umri na hasa jinsia za wazazi na ndugu zao. Hivyo, neno la Kiingereza "aunt" linaweza kumaanisha "shangazi" dada wa baba, "mama mkubwa" kama ni mkubwa wa mama au "mama mdogo" kama ni mdogo wa mama. Vilevile anayeitwa kwa Kiingereza "uncle" anaweza akaitwa kwa Kiswahili "mjomba", lakini "baba mkubwa" kama ni kaka wa baba au "baba mdogo" kama ni mdogo wa baba. Tena kwa Kiingereza " ...

                                               

Siku ya Mama

Siku ya Mama ni sikukuu ya maadhimisho ya kuonyesha heshima na thamani ya akina mama katika familia kutokana na mchango na ushawishi wao mkubwa katika jamii. Siku hii husherehekewa katika tarehe tofauti duniani lakini miezi maarufu zaidi ni ile ya Machi na Mei. Siku ya Mama ya kisasa ilianza kusherehekewa nchini Marekani mapema kabisa katika karne ya 20. Siku hiyo haihusiani moja kwa moja na siku ya Mama iliyokuwepo katika jamii nyingine kwa miaka mingi iliyopita hata maelfu ya miaka iliyopita. Kwa mfano katika tamaduni za Wagiriki kulikuwa na siku inayofanana na siku ya mama inayoadhimish ...

                                               

Wazazi

Wazazi ni wale waliofanya watoto wapatikane katika spishi yao. Kwa wanadamu, mzazi ndiye mlezi wa mtoto. Inafaa sana uzazi uendelezwe na malezi hadi kumfanya mtoto akomae pande zote na kuwa mtu mzima, tena bora. Mzazi wa kibiolojia ni mtu ambaye gamete yake imetoa mtoto, mzazi wa kiume kupitia manii, na mwanamke kupitia kijiyai. Wazazi hao, baba na mama, ni jamaa ya kwanza na kuchangia asilimia 50 ya maumbile ya mtoto. Mwanamke, mbali ya kujifungua, anaweza kuwa mzazi kwa njia ya upasuaji pia, hasa pale ambapo ujauzito una matatizo. Siku hizi inawezekana kuwa na wazazi wa kibiolojia zaidi ...

                                               

Yatima

Yatima ni mtoto aliyefiwa au kutelekezwa moja kwa moja na wazazi wake wote. Kwa kawaida mtoto aliyewapoteza wazazi wake wote wawili anaitwa yatima. Watu wazima pia wanaweza kuitwa mayatima. Ingawaje, watu waliofikia utu uzima kabla wazazi wao hawajafariki kwa kawaida hawaitwi hivyo. Kwa ujumla hili ni neno ambalo hutumika kuelezea watoto ambao wazazi wao walifariki kabla ya wao kufikia umri wa kujitegemea.

                                     

ⓘ Familia

  • Mwanzoni, wataalamu waliangalia lugha hizo kama familia moja ya kilugha, lakini tangu pale familia tofautitofauti zilibainishwa, k.m. lugha za Kitorricelli
  • Jenasi kutoka Kigiriki Γένος genos Kilatini genus nasaba, ukoo, familia aina ni ngazi katika uainishaji wa kisayansi unaopanga viumbehai mimea
  • Lemuriformes Familia ya juu Lemuroidea Familia Archaeolemuridae Familia Cheirogaleidae: Lemuri kibete na lemuri - panya Familia Daubentoniidae: Ai - ai Familia Indriidae:
  • Kila mtu ana wajibu wake, hata kama ni baba wa familia Mifano ya wajibu: kwa baba: kulinda familia yake kusomesha watoto wake kufanya kazi kwa bidii
  • Lugha za Kiaustro - Asiatiki ni familia ya lugha ambazo huzungumzwa katika nchi za Asia ya Kusini - Mashariki. Katika familia hiyo kuna lugha 168 zenye wasemaji
  • Lentulidae Familia Lithidiidae Familia Ommexechidae Familia Pamphagidae panzi - chura Familia Pamphagodidae Familia Pyrgacrididae Familia Romaleidae Familia Tristiridae
  • Guruguru ni mijusi wa familia Gerrhosauridae walio na magamba magumu mgongoni. Mbavuni wana kunyanzi la ngozi kwa urefu mzima wa mwili. Mwongoni mwa mijusi
  • Sheshe, familia ya Timotheo Mnzava, familia ya mzee Fundi, familia ya mzee Kirito, familia ya mzee Hoseni Kaloko familia ya Mapande, familia ya Zuberi
Familia pana
                                               

Familia pana

Familia pana ni jamii iliyoundwa na ndugu wa vizazi kadhaa, kwa mfano babu, bibi, wazazi na watoto wao, au pia shangazi, mjomba, binamu n.k., si wazazi na watoto peke yao kama familia nyuklia. Katika nchi ambazo zinakubali mitara, familia zinaweza kuwa pana zaidi.

                                               

Familia (maana)

Familia inaweza kumaanisha Familia biolojia - vikundi vya viumbehai kama wanyama wanaopangwa pamoja katika uainishaji wa kisayansi Familia - kama kundi la baba, mama na watoto wanaoishi pamoja Kundi mbalimbali za vitu, magimba na kadhalika zinazopangwa pamoja kwa sababu zina tabia za pamoja; wanafalaki wanaweza kujadili "familia za nyota"; wanahisabati hupanga "familia za namba" n.k.

Lugha za Kiniger-Kongo
                                               

Lugha za Kiniger-Kongo

Lugha za Kiniger-Kongo ni familia ya lugha barani Afrika. Katika familia hiyo kuna lugha takriban 1400 zenye wasemaji milioni 370 katika Afrika Magharibi, mashariki na kusini. Kundi kubwa hasa ndani ya familia hiyo ni lugha za Kibantu kama Kiswahili.

Babu
                                               

Babu

Babu kwa mjukuu wake ni hasa baba wa mzazi wake mmojawapo. Katika DNA anachangia 25%. Inakadiriwa kwamba miaka 30.000 iliyopita idadi ya watu waliofikia umri wa kuona wajukuu wao iliongezeka sana na kuwezesha ushirikishaji wa ujuzi na mangamuzi mbalimbali kuliko awali. Pia babu anaweza kushika nafasi ya baba ikiwa huyo hayupo k.mf. amekufa na kumfaidisha mtoto kimalezi. Hata kama baba yupo, babu anaweza kutoa mchango mzuri katika makuzi ya mtoto.

Binamu
                                               

Binamu

Binamu ni ndugu wa ukoo tofauti, kwa sababu ni mtoto wa mjomba au wa shangazi, si mtoto wa baba mkubwa, baba mdogo, mama mkubwa wala mama mdogo. Kuhusu mahusiano na uwezekano wa kuoana kuna desturi na sheria tofauti duniani.

Users also searched:

...
...
...