Back

ⓘ Wakati - Wakati, Mwezi, wakati, Muda sanifu wa dunia, Asubuhi, Siku, Kitenzi, Kalenda ya Kiyahudi, Lukuledi, Adhuhuri, ISO 8601, Kali Yuga, Kanda muda, Mwaka ..
                                               

Wakati

Wakati ni neno la kutaja ama ufuatano wa matokeo au muda ama kipindi ambamo jambo latokea. Tunaishi katika wakati na tunapanga maisha yetu kufuatana na wakati lakini si rahisi kusema wakati ni kitu gani. Sayansi, fizikia, falsafa na dini zote zina njia mbalimbali za kuangalia na kueleza wakati.

                                               

Mwezi (wakati)

Uso wa mwezi jinsi unavyoonekana duniani hubadilikabadilika. Mwezi mpevu unaonekana kama duara kamili la kungaa lakini baada ya kuonekana hivi umbo lapungua kila siku hadi kutoonekana kabisa na hali hii huitwa mwezi mwandamo. Baadaye mwezi unaonekana tena kama hilali nyembamba na kuongezeka hadi kuwa duara tena. Muda wa mabadiliko yote kupita mara 1 ni siku 29 1/4. Muda wa mabadiliko kati ya mwezi mwandamo hadi kupotea na kuwa mwezi mwandamo tena ni kati ya siku 28 - 29. Kipindi hiki kinakumbukwa kirahisi, kinatazamiwa na watu wote wakati uleule kwa hiyo pamoja na kipindi cha siku kilikuwa ...

                                               

Muda sanifu wa dunia

Muda sanifu wa dunia ni utaratibu wa kulinganisha saa na wakati kote duniani. Unarejea wakati kwenye longitudo ya Greenwich karibu na London na longitudo hii huitwa pia meridiani ya sifuri.

                                               

Asubuhi

Asubuhi ni kipindi cha siku ambacho kinaleta mwanga wa kwanza wa mchana baada ya giza la usiku. Kwa binadamu na wanyama wengi ndio wakati wa kuamka kwa kutoka usingizini ili kuanza shughuli mbalimbali. Katika dini mbalimbali, ni wakati muhimu wa sala.

                                               

Siku

Mabadiliko hayo ya mchana na usiku husabibishwa na mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake. Upande wa dunia unaotazama jua unapata mwanga wa mchana lakini upande mwingine usiotazama jua unakuwa gizani. Sisi pamoja na vitu vyote vilivyo juu ya uso wa dunia, yaani bahari, mito, milima, binadamu, misitu, majangwa, majengo, barabara na kila kitu unachoweza kuwaza kuwa kipo kwenye uso wa dunia, basi vyote huwa katika mwendo kadiri dunia inavyojizungusha kwenye mhimili wake. Hivyo basi, wakati upande ule wa uso wa dunia tulipo unapogeukia au kutazamana na jua, basi kwetu inakuwa mchana, pale ambap ...

                                               

Kitenzi

Kitenzi ni istilahi ya sarufi kwa maneno yanayotaja matendo kama vile kufanya, kwenda, kulala, kupiga, kuishi na kadhalika. Lugha nyingi zinatumia vitenzi ingawa kuna pia lugha zisizoweka tofauti kati ya vitenzi na majina.

                                               

Kalenda ya Kiyahudi

Kalenda ya Kiyahudi ni kalenda inayotumiwa katika dini ya Uyahudi na pia nchini Israel. Inatumiwa kupanga tarehe za sikukuu za Kiyahudi na utaratibu wa kusoma Torati kwa kila wiki. Liturgia na sala hufuata pia mpangilio wa kalenda hiyo.

                                               

Lukuledi

Kwa maana nyingine ya jina hili angalia Lukuledi Mto Lukuledi ni kati ya mito ya mkoa wa Lindi Tanzania Kusini Mashariki ambayo maji yake yanaingia katika Bahari Hindi kwenye mji wa Lindi. Mto Lukuledi una urefu wa takriban km 160. Wakati wa ukame maji si mengi, lakini kwenye km 40 za mwisho kabla ya mdomo maji hupatikana. Kwenye km 20 za mwisho kabla ya mdomo mto hupanuka kuwa hori ya bahari na sehemu hii ya mwisho huitwa pia Lindi Creek. Bonde la Lukuledi hutenganisha nyanda za juu za Makonde na bonde za juu za Muera.

                                               

Adhuhuri

Adhuhuri ni kipindi cha mchana ambapo jua liko juu zaidi, baina ya asubuhi na alasiri. Adhuhuri ni kipindi kati ya saa sita na saa nane za mchana. Kinyume chake ni usiku kati. Kwa kawaida binadamu anatumia nafasi hiyo kupumzika kidogo na kupata chakula kabla hajaendelea na kazi. Vivyo hivyo, dini mbalimbali, hasa Ukristo na Uislamu, zinamuelekeza kumkumbuka zaidi Mungu kwa kusali kidogo.

                                               

ISO 8601

ISO 8601 ni mfumo wa kimataifa uliokubaliwa kwa maelewano juu ya namna ya kutaja tarehe na wakati. Kimetolewa na Shirika la Kimataifa la Usanifishaji kwa Kiingereza "International Organization for Standardization ISO"). ISO 8601 ni orodha ya mapendekezo namna ya kuandika tarehe na wakati katika mawasiliano ya kimataifa. Jina la kiingereza ni "Data elements and interchange formats -- Information interchange -- Representation of dates and times"

                                               

Kali Yuga

Kali Yuga ni kimoja cha vipindi vinne vya muda wa ulimwengu kufuatana na imani ya Uhindu. Kufuatana na imani hii, ulimwengu baada ya uumbaji una muda wake maalumu unaogawiwa kwa "yuga" au vipindi vinne. Ulimwengu unaanza baada ya kila uumbaji katika yuga au kipindi cha kwanza ambako nguvu ya kimungu ya karma inapatikana kwa nguvu kwa hiyo dunia inajaa maadili mema. Kila yuga nguvu ya karma inapungua hadi katika kipindi au yuga ya nne nguvu ya karma na maadili iko robo moja tu. Pepo baya kwa jina "Kali" anatawala yuga hii. Kufuatana na maandiko ya Kihindu Kali Yuga hii ilianza 23 Januari 31 ...

                                               

Kanda muda

Kanda muda ni eneo la dunia lenye umbo la mlia unaoenea kati ya ncha zote mbili yaani kuanzia kaskazini hadi kusini. Ndani ya mlia huu muda sanifu ni uleule, yaani masaa huonyesha saa ileile. Saa zetu zinalenga kulingana na mwendo wa jua angani. Wakati wa jua kufika kwenye kilele chake angani kabisa ni katikati ya mchana au ni saa 6 mchana. Kwenye ikweta saa ya upweo ni saa 12 asubuhi. Mahali pote panapopatikana kwenye mstari mmoja kati ya kaskazini na kusini huwa pamoja kimuda wakati wa mchana. Lakini maeneo ambayo ni mbali zaidi upande wa mashariki au magharibi huwa na wakati tofauti maa ...

                                               

Mwaka

Katika kalenda za jua mwaka unalingana na muda wa mzunguko mmoja wa dunia kwenye mzingo wake kuzunguka jua letu. Muda kamili wa mzunguko huu ni siku 365.2425. Kwa sababu hiyo kalenda ya Gregori inaongeza mwaka mrefu wa siku 366 katika utaratibu ufuatao: kila mwaka wa nne utakuwa na siku 366 badala ya 365 kwa kuongeza tarehe 29 Februari. Mifano: 1892, 1996, 2004, 2008, 2012 kila mwaka ambao namba yake inagawiwa kwa 100 utakuwa na siku 365 siyo 366 hata kama namba za miaka hii zinagawiwa kwa 4 pia!. Mifano: 1700, 1800, 1900, 2100 kila mwaka ambao namba yake inagawiwa kwa 400 utakuwa tena na ...

                                               

Sekunde

Sekunde ni kipimo cha wakati na kati ya vipimo vya kimsingi wa SI. Kiasili ilihesabiwa kama sehemu ya 60 ya dakika moja lakini kisayansi inapimwa sasa kulingana na mwendo wa mnurulisho wa atomi za sizi -133. Sekunde sitini 60 ni dakika moja, na sekunde elfu tatu na mia sita 3.600 ni saa moja. Kisasili siku iligawiwa kwa masaa, masaa kwa dakika na dakika kwa sekundi. Imeonekana ya kwamba hesabu hii haitoshi kwa matumizi ya kisayansi kwa sababu muda wa siku si sawa kamili kutokana na mwendo wa dunia yetu. Hivyo kipimo kamili cha sekunde ilitafutwa kinachopimika katika fizikia na sasa muda wa ...

                                               

Sikusare

Sikusare ni siku ambako urefu wa mchana na usiku ni sawa kote duniani. Hii inatokea mara mbili kila mwaka, mara ya kwanza mnamo 21 Machi sikusare machipuo na 23 Septemba sikusare otomnia. Katika kanda karibu na ikweta hazionekani kwa urahisi lakini kwenye nusutufe za dunia upande wa kusini na kaskazini wa ikweta zimetambuliwa tangu karne nyingi na zimekuwa siku muhimu kwa makadirio ya kalenda mbalimbali. Kwa kawaida kuna tofauti kati ya urefu wa mchana na usiku isipokuwa karibu na ikweta. Karibu na ncha za dunia muda wa usiku na mchana unaweza kuwa mrefu hadi karibu nusu mwaka lakini kwa k ...

                                               

Solistasi

Solistasi ni jina la siku mbili katika mwaka ambako tofauti kati ya urefu wa mchana na usiku ni kubwa zaidi kuliko siku zingine. Hutokea mara mbili kwa mwaka. Tarehe ya kwanza ni 20 au 21 Juni na ya pili ni tarehe 21 au 22 Desemba. Watu wanaoishi sehemu za jirani na ikweta huwa hawatambui tofauti kati ya muda wa mchana na usiku, ila kadri wanavyoishi mbali zaidi upande wa kusini au kaskazini wa ikweta, tofauti huwa kubwa zaidi. Kwa kawaida kuna tofauti kati ya urefu wa mchana na usiku isipokuwa kwenye ikweta. Karibu na ncha za Dunia muda wa usiku na mchana unaweza kuwa mrefu hadi karibu nu ...

                                               

Usiku

Usiku ni kipindi cha siku kilichopo kati ya machweo na macheo na hasahasa kipindi cha giza kinachotokea baada ya machweo ambapo mwanga wa jua hauonekani tena angani hadi muda mfupi kabla ya macheo yaani kabla ya jua kuonekana juu ya upeo wa anga. Kinyume chake ni mchana. Kutokana na kupoteapotea kwa nuru ya jua, nyota zinaonekana usiku pasipo mawingu. Watu wengi pamoja na wanyama wengi hulala usiku, lakini kuna wanyama wengine wanaofanya shughuli zao usiku kama vile bundi, popo na wadudu wengi.

                                     

ⓘ Wakati

  • Dakika ni kipimo cha wakati Si kipimo cha SI kamili kama ilivyo sekundi. Dakika ni sehemu ya 60 ya saa moja. Dakika yenyewe hugawiwa kwa sekundi 60.
  • umetoholewa kutoka lugha ya Kiingereza census, lakini una asili ya Kilatini: wakati wa Jamhuri ya Roma sensa ilikuwa orodha iliyowekwa ili kufuatilia wanaume
  • kawaida ni wimbo wakati mwingine pia musiki maalumu bila uimbaji ulioteuliwa na serikali au kwa njia ya sheria na kutumiwa wakati wa nafasi maalumu
  • ni eneo la nchi kavu kati ya bahari, ziwa au mto linalozungukwa na maji wakati wote. Ukubwa wake hautoshi kukifanya kiitwe bara Visiwa vilivyo karibu
  • mwezi kama majira ya wakati Mabadiliko ya kuonekana kwake yalisababisha katika Kiswahili neno mwezi litumike kama kipindi cha wakati Awamu zake nne pengine
  • Nyota kwa mang amuzi na lugha ya kawaida ni nuru ndogo zinazoonekana angani wakati wa usiku. Kwa kutumia darubini na vifaa vya kisayansi imegunduliwa ya kwamba
  • kila karne majadiliano kwa sababu watu wengi husikia karne mpya inaanza wakati tarakimu ya mbele waliyozoea muda mrefu inabadilika. Hivyo watu wengi walisheherekea
  • shughuli za kilimo kwa togwa. Wakati wa masika kaya zote huwa na kazi za uzalishaji kwa shughuli za kilimo kwa kulima mpunga na wakati wa kiangazi sherehe nyingi
  • Katika nchi na makabila mbalimbali jina linaweza kubadilishwa, kwa mfano wakati wa ibada wa kuingizwa katika dini fulani, au kuongezewa, kwa mfano kutokana
  • mita 500 likiwa na visiwa vya mchanga. Wakati wa ukame maji hupungua sana hadi watu kuvuka mto kwa miguu wakati wa mvua umbali kati ya pande zote mbili
                                               

Vielezi vya wakati

Vielezi vya wakati vinaweza kuwa vya: Matukio ya Kihistoria, n.k. Nyakati za siku Majina ya miezi Majira ya mwaka Wiki Majina ya siku Mwaka Mifano Wakulima hupanda wakati wa vuli! Harusi yake itafungwa Jumapili hapa inataja majina ya siku katika juma. Masanja alizaliwa wakati wa vita ya majimaji hapa inarejea tukio la kihistoria. Nitasafiri wiki ijayo hapa inataja wiki Ashura alitoroka majogoo. Jambazi sugu ameuawa leo usiku.

Antipapa
                                               

Antipapa

Antipapa ni jina linalotumiwa na wanahistoria kumtajia askofu yeyote aliyejidai kuwa Papa wa Roma, lakini madai yake hayakukubaliwa na wengi wakati wake, au hayakubaliwi na Kanisa Katoliki wakati huu.

Saa
                                               

Saa

Kwa chombo cha kupimia wakati tazama saa ala Saa ni kipimo cha wakati. Si kipimo cha SI kamili kama ilivyo sekunde lakini ni kawaida kote duniani pia katika matumizi ya kisayansi. Saa inagawiwa kwa dakika 60 na sekundi 3.600. Siku ina takriban masaa 24.

Mchana
                                               

Mchana

Mchana ni kipindi chote cha siku ambapo nuru ya jua inaangaza sehemu fulani ya dunia. Kinyume chake ni usiku. Kwa wakati mmoja, jua linaangaza karibu nusu ya dunia. Huko ni mchana, kumbe katika nusu ya pili ni usiku. Kwa binadamu na wanyama wengi ndio wakati wa utendaji mwingi zaidi.

Greenwich Mean Time
                                               

Greenwich Mean Time

Greenwich Mean Time ni kipimo cha wakati kwa ajili ya kanda muda. Mahali pa kipimo hicho ni mji wa Greenwich ambao siku hizi ni sehemu ya jiji la London, Uingereza.

Users also searched:

...
...
...