Back

ⓘ Cheo - Kaizari, Sultani, Papa, Askofu, Askofu mkuu, Gavana, Cheo, Ofisa, Admirali, Chansela, elimu, Dame, Farao, Jenerali, Kamanda, Kiranja Mkuu, Meja Jenerali ..
                                               

Kaizari

Asili ya cheo ni Julius Caesar aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka 44 KK. Watawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar kwa heshima yake hadi jina likawa cheo. Cheo cha Kaizari kiliendelea kutumika katika eneo la Dola la Roma ya Mashariki Bizanti hadi mwaka 1453.

                                               

Sultani

Neno lenyewe lamaanisha "nguvu", "mamlaka" au "utawala" likawa baadaye kama cheo cha mtawala wa kiislamu mwenye kujitegemea bila kuwa na mwingine juu yake.

                                               

Papa

Kwa samaki anayeitwa kwa Kiswahili "papa" tazama papa samaki Papa ni cheo cha kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote. Cheo hicho kinategemea kile cha askofu wa Roma.

                                               

Askofu

Neno episkopos linaonekana kama cheo katika maandishi ya mwisho wa karne I na mwanzo wa karne II kama vile waraka wa kwanza wa Klementi ambapo askofu aonekana kuwa kiongozi mkuu wa kanisa la mji fulani. Katika uenezi wa Ukristo madaraka ya askofu yalipanuka. Kadiri makanisa yalivyoenea hata nje ya miji hadi mashambani askofu akawa kiongozi wa eneo, si wa mji tu. Wakati ule ngazi za daraja zilionekana: Kanisa la mji au eneo likiongozwa na episkopos askofu akishauriana na "presbiteri" kiasili: wazee; baadaye: makasisi na kusaidiwa na mashemasi au madikoni.

                                               

Askofu mkuu

Askofu mkuu ni cheo cha askofu kiongozi anayesimamia maaskofu katika jimbo la kanisa lenye dayosisi mbalimbali. Asili ya neno lenyewe ni Kigiriki αρχή arché mwanzo, wa kwanza. Sehemu ya pili ni neno la Kigiriki επίσκοπος episkopos mwangalizi lililofikia Kiswahili kupitia umbo la Kiarabu uskuf.

                                               

Gavana

Kuna nchi ambako gavana ni mtendaji mkuu wa serikali katika dola la shirikisho au jimbo. Kwa mfano katika Marekani ina madola 50 ndani yake na kila moja huwa na gavana kama mkuu wa serikali ya kidola. Cheo hiki kinalingana na waziri mkuu wa sehemu ya nchi yenye kiwango cha kujitawala na bunge lake pamoja na serikali ya kieneo, kwa mfano waziri mkuu wa jimbo la Afrika Kusini au Ujerumani.

                                     

ⓘ Cheo

  • serikalini katika ufuatano Kama mtu ameshika cheo alipaswa kupumzika miaka miwili kabla ya kugombea cheo kilichofuata. Cheo kimoja cha dikteta pekee kilishikwa
  • mengi ya ndani. Majimbo haya 50 yako pamoja na maeneo mengine yasiyo na cheo cha jimbo kamili lakini yapo moja kwa moja chini ya shirikisho kwenye ngazi
  • mtawala wa kike juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka kwa mzazi wake aliyekuwa mfalme au malkia pia. Lakini kuna pia
  • Negus ni cheo cha kifalme katika historia ya Uhabeshi au Ethiopia. Maana ya neno hili ni mfalme Cheo hiki kilitumiwa katika historia ya Ethiopia na
  • Jenerali ni cheo kikuu cha kijeshi katika nchi nyingi za dunia. Jenerali huwa kiongozi wa ngazi ya juu katika jeshi. Idadi ya majenerali si kubwa. Kazi
  • ya Kiarabu: خان ni cheo cha mtawala chenye asili kati ya wafugaji Wamongolia na Waturki wa Asia ya Kati. Mwanzoni kilikuwa cheo cha kijeshi kilichomaanisha
  • kumaanaisha Shahada Uislamu ni ungamo la imani katika dini ya Uislamu cheo cha kielimu kinachotolewa kwa mtu aliyeonyesha utaalamu wake kufuatana na
  • thamani ya utu utukufu, daraja la juu au jaha Heshima inadaiwa na wenye cheo na mamlaka, kuanzia wazazi kutoka kwa watoto wao. Pia heshima inatarajiwa
  • Waziri Mkuu ni cheo cha kiongozi wa serikali. Neno lasema ya kwamba yeye ni mkubwa kati ya mawaziri wa serikali. Madaraka yake hutegemea na katiba ya nchi
  • katika cheo cha pili katika utendaji wa nchi huru, dola la shirikisho au koloni. Yeye huongoza Baraza la Mawaziri. Cheo hicho hutofautiana na cheo cha mkuu
Cheo
                                               

Cheo

Cheo ni rejeo linaloongezwa kwa jina la mtu kuonyesha heshima, wadhifa au kazi yake. Pia ni kimo cha kitu fulani, kama vile vazi. Tena ni jina la vifaa mbalimbali: mti wa kufulia nazi, ubao mwembamba wa kushonea mkeka, kifimbo cha kuagulia ambacho mganga wa jadi anatafuta vitu.

                                               

Ofisa

Ofisa ni mtu mwenye cheo katika ofisi au katika mfumo wa shirika fulani. Neno latumiwa hasa kwa wanajeshi wa vyeo vyenye mamlaka juu ya wanajeshi wa kawaida. Katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyeo vya maofisa vimepokewa kutoka jeshi la kikoloni vikifuata mfumo wa jeshi la Uingereza. Maofisa hutofautishwa baina ya wenye kamisheni ambavyo ni vyeo vya juu zaidi na maafisa wa ngazi za chini.

Admirali
                                               

Admirali

Admerali ni cheo cha kiongozi mkuu wa kijeshi wa wanamaji. Cheo hicho kinalingana na jenerali katika matawi mengine ya jeshi. Neno linatokana na Kiarabu أمير البحر amir-al-bahr yaani "mwenye mamlaka baharini". Iliingia katika lugha za Ulaya kama "admiral". Cheo hicho si kawaida katika jeshi la majini la Tanzania wala Kenya, lakini hutumiwa kutafsiri vyeo vya kigeni.

                                               

Chansela (elimu)

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Chansela ni kiongozi wa chuo kikuu. Matumizi ya cheo hiki katika Kiswahili na lugha nyingine yanatokana na mapokeo ya Uingereza yaliyoenea kupitia makoloni yake na kuendelea katika idadi ya nchi huru. Vinginevyo mkuu wa chuo kikuu mara nyingi huitwa "rais wa chuo". Vyuo vingi katika Jumuiya ya Madola huwa na chansela ambaye si mtendaji mkuu. Katika hali hiyo, mtendaji mkuu huwa ni makamu wake.

                                               

Dame

Dame kwa Kiingereza ni cheo cha chini kwa mkabaila wa kike. Inalingana na cheo cha "Sir". Kwa maana hii hupatikana nchini Uingereza na katika nchi za Jumuiya ya Madola zinazomkubali malkia wa Uingereza kama mkuu wa dola. Siku hizi cheo hiki ama kinarithiwa katika familia zilizokuwa zamani watawala wa makabaila au kinatolewa kwa heshima na kama kitambulisho cha kazi nzuri ya kujitolea katika utumishi wa umma. Kwa Kijerumani neno linapatikana kama namna ya kumsemesha mama kiheshima.

Farao
                                               

Farao

Farao lilikuwa jina la heshima ambalo kila mfalme wa Misri ya kale alipewa. Jina hilo lilitumika hadi Warumi walipoiteka Misri mwaka 30 KK. Farao wa mwisho alikuwa malkia Kleopatra. Kabla ya hapo, wafalme wa kale wa Misri walikuwa na majina matatu: Horus, Nesu Bety na Nebty. Maarufu zaidi ni Ramses II aliyekuwa farao wa masimulizi ya Biblia kuhusu Musa, pamoja na Tutankhamun ambaye ni farao wa pekee ambaye kaburi lake lilihifadhiwa bila kuporwa na majambazi.

Jenerali
                                               

Jenerali

Jenerali ni cheo kikuu cha kijeshi katika nchi nyingi za dunia. Jenerali huwa kiongozi wa ngazi ya juu katika jeshi. Idadi ya majenerali si kubwa. Kazi yao ni kuongoza na kupanga kazi ya jeshi. Kwa kawaida hawashiriki wenyewe katika mapigano. Neno limeingia katika Kiswahili kutoka lugha ya Kiingereza. Asili yake ni Kilatini generalis yenye maana ya "kwa ujumla".

                                               

Kamanda

Kamanda ni cheo cha afisa wa nevi na jeshi la anga kilicho chini ya Nahodha na juu ya Luteni Kamanda. Cheo cha kamanda pia hupatikana katika baadhi ya vikosi vya polisi.

                                               

Kiranja Mkuu

Kiranja Mkuu au Mkuu wa viranja ni kiongozi wa serikali ya wanafunzi shuleni, hasa katika shule ya msingi na sekondari. Kiranja ni mwanafunzi aliyechaguliwa na walimu au wanafunzi wenzake kwa lengo la kuwasimamia usafi, nidhamu, mazingira ya wanafunzi na kuweka daraja kati ya waalimu na wanafunzi. Kiranja Mkuu ndiye anayewasimamia na kuwaagiza viranja wengine, ni kama Rais na wizara zake.

Luteni jenerali
                                               

Luteni jenerali

Luteni jenerali ni ofisa wa jeshi mwenye cheo cha juu kuliko meja jenerali na chini ya jenerali. Luteni jenerali wa jeshi la Tanzania kwa sasa ni Yakubu Hasan.

Luteni wa Pili
                                               

Luteni wa Pili

Luteni wa Pili, pia Luteni-usu, ni cheo cha chini kabisa cha afisa wa jeshi waliopewa kazi ya usimamizi. Kiko chini ya Luteni wa Kwanza.

                                               

Meja Jenerali

Meja Jenerali ni cheo cha afisa wa jeshi kilicho chini ya Luteni Jenerali na juu ya Brigedia au Brigedia Jenerali, kulingana na nchi.

Mwinjilisti
                                               

Mwinjilisti

Mwinjilisti ni Mkristo mwenye utume wa kuhubiri na kutoa elimu ya Biblia na maadili ya Kikristo katika madhehebu kadhaa ya Uprotestanti. Majukumu yake yanafanana na yale ya katekista au ya shemasi wa Kanisa Katoliki.

Users also searched:

...
...
...