Back

ⓘ Sayansi - UNESCO, Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Upatanisho wa imani na sayansi, ya kilimo, Fizikia ..
                                               

UNESCO

UNESCO ni kifupisho cha United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization yaani Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa. Ni kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kinashughulika habari za elimu, sayansi na utamaduni duniani. Kisheria UNESCO ni shirika la kujitegemea lenye madola wanachama 191. Kati ya shughuli muhimu za UNESCO mojawapo ni Orodha la Urithi wa Dunia linalojumlisha mahali penye umuhimu wa pekee kihistoria, kisayansi au kiutamaduni. Nchi zote zina mahali angalau moja orodhani, nyingine zina pengi, hasa Italia na Hispania.

                                               

Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia

KAST ni kifupi chake cha Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia iliyoandaliwa na wataalamu wa TUKI na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1995. Kamusi hii inakusanya maneno ya kisayansi na ya kiteknolojia kwa utaratibu ufuatao: neno la Kiswahili maana yake kwa Kiingereza katika mabano maelezo yake kwa Kiswahili Mwishowe kuna faharasa ya Kiingereza inayoweza kutumiwa kama kamusi ndogo ya Kiingereza-Kiswahili ya maneno ya kisayansi. Kati ya kamusi za Kiswahili hii ni hatua kubwa mbele katika ukuzaji wa Kiswahili hata ikionyesha bado mapengo na kasoro mbalimbali. Hali halisi kuna kiasi kikubwa ...

                                               

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia) ilikuwa wizara ya serikali nchini Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2008. Ilitanguliwa na Ministry of Higher Education, Science and Technology, iliyoitwa Ministry of Science, Technology and Higher Education kabla ya mwaka 2005. Ofisi kuu ya wizara hii zilikuwa jijini Dar es Salaam. Mwaka 2015 wizara hiyo ilifutwa na idara zake kugawiwa kati ya Wiraza ya Elimu na Idara ya Kazi. Katika baraza ya mawaziri ya pili chini ya rais Magufuli wizara ilianzishwa upya mwaka 2020.

                                               

Upatanisho wa imani na sayansi

Upatanisho wa imani na sayansi ni juhudi zinazofanywa na watu wa dini mbalimbali kuondoa mzozo uliotokea kati ya imani na sayansi, hasa kuhusu suala la uumbaji kuhusiana na mageuko ya spishi. Juhudi hizo zinaitwa pengine kwa Kiingereza: theistic evolution, theistic evolutionism, evolutionary creationism, divine direction, au God-guided evolution. Ieleweke mapema kwamba juhudi hizo hazilengi kutunga au kupitisha nadharia yoyote katika sayansi, ila kuonyesha uwezekano wa kukubali kweli zilizothibitishwa na utafiti wa sayansi pamoja na kweli zilizosadikiwa kwa kupokea ufunuo wa Mwenyezi Mungu ...

                                               

Sayansi ya kilimo

Sayansi ya kilimo ni tawi la biolojia linalojumuisha sehemu za elimu mbalimbali zinazotumiwa katika kilimo. Mara nyingi hugawiwa katika elimu ya kilimo cha mimea, elimu ya mifugo na uchumi wa kilimo. Tiba ya mifugo mara nyingi haihesabiwi humo.

                                               

Fizikia

Fizikia ni fani ya sayansi inayohusu maumbile ya ulimwengu, hususan asili ya dunia na viumbe vyote. Ni taaluma yenye kushughulika na maada na uhusiano wake na nishati. Fizikia imetoa mchango mkubwa katika sayansi, teknolojia na falsafa.

                                               

Ugonjwa

Ugonjwa ni hali ya mvurugo katika utendaji wa kawaida wa shughuli za mwili na roho inayoathiri vibaya starehe ya kiumbehai. Hakuna tofauti kamili baina ya ugonjwa na hali ya kujisikia vibaya. Sayansi inayochungulia magonjwa ni sayansi ya tiba. Magonjwa yanaweza kugawanyika kutokana na vyanzo/asili zake kama vile: magonjwa ya kansa magonjwa yaliyosababishwa na mfumo wa kingamaradhi uliomo mwilini magonjwa yaliyosababishwa na tiba magonjwa kutokana na dutu za nje ya mwili sumu, asidi au moto magonjwa ya kuambukiza magonjwa ya kurithi magonjwa ya roho magonjwa kutokana na ajali

                                               

Darubini

Darubini ni kifaa cha kutazamia vitu ambavyo viko mbali. Kutegemeana na kusudi lake kuna aina mbalimbali: Darubini ndogo za mkononi ni vyombo vinavyotumiwa na wapenda mazingira asilia, wawindaji, polisi na jeshi. darubiniakisi reflecting telescope. darubinilenzi refracting telescope Darubini kubwa hupatikana mara nyingi katika paoneaanga vituo vya astronomia; kuna hasa aina mbili darubini maonzi optical telescope kubwa hutumiwa na wanaastronomia kwa kutazama magimba ya angani kama jua, mwezi, nyota, sayari au kometi. Darubini hizo huwa ama darubiniredio hutumiwa pia na wanaastronomia zikik ...

                                               

Data

Data inamaanisha makundi ya habari. Data kwa kawaida ni matokeo ya vipimo na inaweza kuwa msingi wa jedwali, picha, au uchunguzi wa seti ya variables. Mara nyingi data huchukuliwa kama kiwango cha chini kabisa kwa ujumla ambapo habari na maarifa yaweza kutolewa.

                                               

Entomolojia

Entomolojia ni sayansi ya wadudu. Watu ambao hujifunza wadudu wanaitwa wanaentomolojia. Wadudu wamekuwa wakisomwa tangu nyakati za awali, lakini haikuwa mapema kama karne ya 16 kwamba wadudu walisomwa kisayansi. Wataalamu wengine wanajifunza jinsi wadudu wanavyohusiana. Wengine hujifunza jinsi wadudu wanavyoishi na kuzaa kwa sababu hatujui mengi kuhusu aina fulani za wadudu. Wataalamu wengine wanajifunza njia za kuweka wadudu mbali na mazao ambayo watu huyatumia kama chakula. Kuna mabilioni ya aina zisizojulikana ulimwenguni kote na wataalamu wa taksonomia au uainishaji wanajumuisha wapya ...

                                               

Fikira

Fikira au Fikra ni ujumbe uliotumwa kutoka akilini kwa ajili ya viumbe hai ili kujua kutenda jambo bila kukosea. Fikra husaidia na maamuzi: wanyama mara nyingi huishi bila ya kufikiri, yaani kujua nini kesho atafanya, lakini wanadamu hutumia fikra na kufikiria na kuvumbua vitu ambavyo vinahitajika. Bila fikra za mawazo, dunia isingeendelea sana.

                                               

Hadubini

Hadubini ni kifaa cha kutazama vitu vidogo sana. Ni chombo muhimu cha sayansi kwa utafiti wa vitu ambavyo ni vidogo mno kwa jicho la binadamu.

                                               

Hisabati

Hisabati ni somo linalohusika na idadi, upimaji na ukubwa wa vitu. Kwa ujumla linahusika na miundo na vielezo. Hisabati linaundwa na masomo mbalimbali, kama hesabu, jiometria na aljebra. Neno hisabati katika lugha ya Kiswahili limetokana na neno la Kiarabu حسابات halisi: hesabu wingi). Somo hili huweza kutumika kutatua matatizo mbalimbali, lakini hasa ni la msingi katika uelewa wa ulimwengu kisayansi. Hivyo hutumiwa na masomo mengine kama Fizikia, Jiografia, Kemia katika mafunzo yake.

                                               

ICSU

ICSU ni kifupisho cha International Council of Scientific Unions yaani Baraza la Kimataifa la Mashirika ya Kisayansi. Jina lingine ni International Council for Science, yaani Baraza la Kimataifa kwa ajili ya Sayansi. Makao makuu yako Paris, Ufaransa. Ina wawakilishi wa nchi 140.

                                               

Jiodesia

Jiodesia ni sayansi ya dunia inayohusika na upimaji na uelewaji wa umbo lake, mwelekeo wake angani, na uvutano wake. Utafiti wake unaenea katika mabadiliko ya tabia hizo za dunia na katika zile za sayari nyingine.

                                               

Jiografia

Jiografia ni somo la Dunia na vipengele vyake, wakazi wake, na maajabu yake. Neno la Kiswahili jiografia linafuata matamshi ya Kiingereza ya neno la Kigiriki "γεωγραφία", geo-grafia kutoka gê "dunia" na graphein "kuandika". Lina maana ya "kuandika kuhusu Dunia". Neno hili lilianza kutumiwa kwa mara ya kwanza na mwanasayansi Eratosthenes 276-194 KK. Sehemu za jiografia ni vitu kama mabara, bahari, mito na milima. Wakazi wake ni watu wote na wanyama waishio juu yake. Maajabu yake ni vitu vinavyotokea kama vile maji kujaa na kupwa, upepo, na tetemeko la ardhi.

                                               

Kemia

Kemia ni sayansi ya mata kwa kiwango cha atomi. Kemia yahusu tabia ya elementi na viungo vya atomi, ni somo la kujua mabadiliko ya mata na uhusiano wa mata na mata ndogo tofauti, na pia huhusika wa nishati. Kimsingi kemia ni somo la atomi na mkusanyo wa atomi kwa molekyuli, bilauri ama madini ambavyo vinajenga mata za kawaida. Kulingana na kemia ya kisasa ni ujenzi wa mata kwa kiwango cha atomi.

                                               

Maabara

Maabara ni jengo au chumba maalumu kinachotumika kwa ajili ya majaribio na utafiti wa kisayansi. Kuna aina mbalimbali za maabara, mfano: maabara za biolojia, maabara za kemia, maabara za fizikia n.k. Vilevile kuna maabara zinazotumika katika hospitali na katika majaribio mengine ya kisayansi. Kwa mfano, maabara ya biolojia ni jengo au chumba maalumu kwa ajili ya kufanyia majaribio yahusuyo viumbe hai.

                                               

Mango

Mango ni moja kati ya hali maada. Maana yake ni imara, tofauti na kiowevu au gesi. Katika hali mango atomu zinakaa mahali pamoja katika gimba, hazichezi wala kusogea ndani yake. Kila atomu ina mahali pake. Gimba mango lina umbo, mjao na uzani maalumu. Umbo mango lina urefu, upana na kimo chake, tofauti na kiowevu kinachobadilika umbo kufuatana na chombo chake au gesi isiyo na umbo wala mjao maalumu. Kama mango inabadilika kuwa kiowevu tunasema inayeyuka. Kama inabadilika kuwa gesi au mvuke moja kwa moja tunaliita badiliko hili mvukemango. Maana ya asili ya "mango" ni jiwe gumu jeusi lililo ...

                                               

Mitalojia

Mitalojia ni elimu ya upimaji. Inalenga kuweka msingi kwa maelewano kuhusu vizio na matumizi yake ambayo ni jambo la msingi kwa shughuli za kimataifa.

                                               

Uasilia

Uasilia, maana yake ni ulimwengu ulivyo kwa asili, kabla ya binadamu kuuathiri kwa utamaduni na hasa kwa ustaarabu wake, uliokuza teknolojia inayomwezesha kufanya mengi, mazuri na mabaya, pengine mambo yanayoleta faida ya haraka lakini yana madhara makubwa kwa siku za mbele. Uasilia wote unasomwa kwa mpango na sayansi katika matawi yake yote.

                                               

Ufichamishi

Ufichamishi ni sayansi ya kulinda mawasiliano kwa kuficha maana yake kwa watu wasiolengwa. Kabla ya kupatikana kwa mitambo ya kisasa ujumbe uliandikwa kwa kubadilisha herufi au majina kwa kutumia mfumo uliojulikana kwa mwandishi na mpokeaji aliyelengwa peke yao. Mtu mwingie aliyeona ujumbe alishindwa kuelewa chochote. Siku hizi ufichamishi hufanywa kwa kutumia mitambo na programu za kompyuta.

                                               

Ukungu

Lu C., Liu Y., Niu S., Zhao L., Yu H., Cheng M. 2013. Kigezo:Fontcolor, Acta Meteor. Sinica, 276, 832–848. Filonczuk, Maria K., Cayan, Daniel R., Riddle, Laurence G. 1995. Variability of marine fog along the California coast. SIO-Reference, No 95-2, Climate Research Division, Scripps Institution of Oceanography, University of California, San Diego. Corton, Christine L. London Fog: The Biography 2015 Ahrens, C. 1991. Meteorology today: an introduction to weather, climate, and the environment. West Pub. Co. ISBN 978-0-314-80905-6. Lu C., Niu S., Tang L., Lü J., Zhao L., Zhu B. 2010. Kigezo:F ...

                                               

Utungisho katika wanyama

Utungisho katika wanyama ni kitendo cha seli za gameti ya kiume kuungana na gameti ya kike, na kuunda seli moja ambayo baadaye hukua na kufikia hali ya kiumbe kikubwa. Utungisho hutokea kwa wanyama hali kadhalika kwenye mimea pia ambayo huzaliana kwa ogani zote za kike na kiume kuchangia katika kutengeneza kiumbe kipya. Makala hii inalenga utungisho unaotokea katika wanyama. Utungisho ni wakati muafaka katika mchakato mzima wa kuzaliana. Huanza pale manii inapokutana na sehemu ya nje ya yai ovum na humalizikia pale kiini nyukliasi cha manii kinapoungana na kile cha yai.

                                     

ⓘ Sayansi

  • wataalamu wake wa fani mbalimbali waliweka misingi muhimu ya maendeleo ya sayansi katika karne zilizofuata. Hata baada ya Ugiriki kuingizwa katika Dola la
  • Katika historia watu wameweka nguvu nyingi katika maendeleo ya silaha. Kila sayansi na kila teknolojia huangaliwa na watu kwa faida yake katika utengenezaji
  • Usanifu majengo ni sanaa na sayansi ya kubuni muundo na sura ya majengo. Sanaa na sayansi hii inajumuisha pia mambo kama mipango miji, usanifu wa eneo
  • katika nyanja mbalimbali za maisha na kulisha mawazo mengi. Upande wa sayansi yanahusika na ongezeko la ujuzi kutokana na utafiti na mabadilishano ya
  • nalo na kulipendekeza kwa wengine ili lizidi kuchunguzwa upande wa falsafa, sayansi n.k. kwa kutumia hoja, vipimo na njia nyingine za kufikia ukweli.
  • kinachotolewa kwa mtu aliyeonyesha utaalamu wake kufuatana na masharti ya sayansi kwenye Chuo Kikuu fulani mfano: Shahada ya awali BA, BSc uzamili MA
  • kabisa ni uso wa dunia. Ni sehemu ya tabakamwamba. Dunia yetu hutazamiwa na sayansi kuwa na tabaka mbalimbali kama kitunguu. Tabaka ya nje ni imara yaitwa
  • wa watu. Sayansi ya metorolojia huifanyia halihewa utafiti kwa kupima hali mbalimbali hadi kutabiri mabadiliko yanayokuja karibuni. Sayansi hii inafundishwa
  • mama ya lahaja zilizoendelea na kuwa lugha za Kirumi lugha ya elimu na sayansi katika Ulaya kwa karne nyingi lugha rasmi ya serikali katika nchi nyingi
Sayansi bandia
                                               

Sayansi bandia

Kiputiputi, O. M. 2001. Kufundisha sayansi kwa Kiswahili. Mdee, JS and Mwansoko, HJM, Makala ya kongamano la kimataifa KISWAHILI 2000 Proceedings. Dar-es-Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

Sayansi za dunia
                                               

Sayansi za dunia

Sayansi za dunia nu jumla ya sayansi zinazochungulia maumbile na sifa za dunia yetu au sayari tunapoishi. Kuna matawi manne makuu yanayoshughulikia utafiti huu ni jiodesia jiofizikia jiolojia jiografia Yote hutumia matokeo na mbinu za masomo kama fizikia, kemia, biolojia na hisabati na kuyatumia kwa upimaji na utafiti wa dunia yetu.

                                               

Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania

Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania ni shirika la umma ambalo linashirikiana na serikali ya Tanzania. Ilianzishwa kwa agizo la Bunge la Tanzania mnamo mwaka wa 1986 ikiwa kama mpokezi wa Baraza la Sayansi na Utafiti Tanzania. Tume hii ni tawi la taasisi na Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia. Ofisi zake kuu zipo mjini Dar es Salaam.

                                               

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ni chuo kikuu cha umma kinachopatikana katika jiji la Mbeya, Tanzania. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya zamani kilijulikana kama chuo cha ufundi Mbeya.

Audiolojia
                                               

Audiolojia

Audiolojia ni kiwanja cha sayansi kinachohusika na masomo kuhusu sikio, kusikia na magonjwa ya masikio. Wanaaudiolojia hutumia ujuzi wao, kupeleleza kiwango cha kusikia cha mtu binafsi na kama kuna tatizo, huweza kujua tatizo liko wapi na pia hueleza matibabu yepi yanawezekana au yanapatikana.

Jaribio
                                               

Jaribio

Jaribio ni taratibu zinazofuatwa ili kuthibitisha, kukanusha au kuhalalisha makisio. Majaribio yanatofautiana sana katika malengo na vipimo, lakini kwa kawaida hutegemea na kurudiwa kwa taratibu husika na uchambuzi yakinifu wa matokeo yaliyopatikana. Mtoto anaweza kufanya majaribio ya msingi ili kuelewa uzito, lakini kundi la wanasayansi wanaweza kuchukua miaka mingi kufanya uchunguzi kuongeza uelewa wao kuhusu jambo fulani.

Jiofizikia
                                               

Jiofizikia

Jiofizikia ni fani ya sayansi ya miamba na dutu nyingine zinazounda dunia, pamoja na muundo wa kimaumbile uliomo duniani, ndani yake na juu ya uso wake.

                                               

Kiwango utatu

Kiwango utatu ni kiwango cha maji au dutu nyingine inapoweza kutokea mahali pamoja katika hali mango, kiowevu na gesi. Kiwango hiki kinategemea halijoto na shindikizo. Kiwango utatu cha maji ni kiwango cha kukadiria skeli ya selsiasi au sentigredi 273.16 K au 0.01 °C.

Mfululizo
                                               

Mfululizo

Katika hisabati, mfululizo ni tendo la kihesabu la kujumlisha lisilo na mwisho toka idadi inayoanza. Mfululizo hutumika katika utarakilishi.

Mwanasayansi
                                               

Mwanasayansi

Mwanasayansi ni mtu anayejihusisha na shughuli maalumu ili kupata maarifa. Kwa maana pana zaidi, mwanasayansi anaweza kutajwa kama mtu anayetumia mbinu za kisayansi. Mtu huyo anaweza kuwa mtaalamu katika eneo moja au zaidi ya sayansi. Wanasayansi hufanya utafiti kuelekea uelewa mkubwa zaidi wa uasilia, ikiwa ni pamoja na ulimwengu kimwili, kihisabati na kijamii. Kwa kawaida wanasukumwa na udadisi wao.

Nyuklia
                                               

Nyuklia

Nyuklia ni neno ambalo linatumiwa katika lugha ya sayansi. Asili yake ni Kilatini "nucleus" inayomaanisha "kiini". Inatumiwa hasa kama tafsiri ya Kiingereza "nuclear". Kwa Kiswahili neno hili linatumiwa hasa katika fani za fizikia kwa kutaja mambo yanayohusu kiini cha atomu, na pia biolojia kwa mambo yanayohusu kiini cha seli. Nyuklia inaweza kutaja:

Stellarium (Programu)
                                               

Stellarium (Programu)

Stellarium ni programu ya bure yenye leseni ya matumizi ya bure kwa umma. Ni programu nzuri na mahususi kwa kuona anganje kupitia kompyuta au simu ya mkononi. Programu hii inasaidia katika mambo ya astronomia na unajimu.

Users also searched:

moe co tz, wizara,

...
...
...