Back

ⓘ Habari - Kupashwa habari, Teknolojia ya habari, Mwanahabari, Uandishi wa habari, uongo, Leo, Usimulizi wa habari, BBC, Gazeti, Intaneti, Nadharia ya njama ..
                                               

Kupashwa habari

Kupashwa habari kwa Bikira Maria kwamba atapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na hatimaye kuzaa mtoto wa kiume, jina lake Yesu, ni tukio la kuheshimika sana kati ya Wakristo na Waislamu kutokana na masimulizi ya Injili na Kurani.

                                               

Teknolojia ya habari

Teknolojia ya habari na mawasiliano, kama ilivyoainiwa na Shirikisho la Teknolojia ya Habari ya Marekani, ni "utafiti, urasimu, uendeleshaji, utekelezaji, usaidizi au usimamizi wa mifumo ya habari, hasa ala za programu na vifaa vya kompyuta.". TEHAMA inahusika na matumizi ya kompyuta na programu za kompyuta: kubadili, kuhifadhi, kulinda, kuchecheta, kueneza na usalama katika kupokea habari. Leo, neno habari limezunguka nyanja nyingi za kompyuta na teknolojia na limekuwa maarufu sana. Wataalamu wa TEHAMA hutekeleza majukumu mbalimbali kutoka kuweka ala hadi kubuni mitandao tata ya kompyuta ...

                                               

Mwanahabari

Mwanahabari ni mtu anayefanya kazi ya uandishi wa habari akikusanya, kutayarisha na kusambaza habari. Anaweza kufanya kazi hiyo akiwa ameajiriwa na gazeti, redio au kituo cha televisheni au kama mkandarasi wa kujitegemea akiuza kazi yake kama makala, picha au filamu. Wanahabari huajiriwa pia na makampuni, taasisi au ofisi za serikali zinazolenga kueleza kazi yao katika jamii. Akiwa mwandishi wa habari wa gazeti huandika nakala za habari na hadithi kwa magazeti. Katika maandalizi ya makala ataongea na watu, kufuatilia habari kwa jumla, kufanya utafiti na mahojiano na watu wanaohusika katika ...

                                               

Uandishi wa habari

Uandishi wa habari ni kazi ya kukusanya, kupanga na kusambaza habari kwa wasomaji, wasikilizaji na watazamaji katika jamii. Usambazaji hutokea kupitia vyombo vya habari na media mbalimbali kama vile gazeti, redio, televisheni na intaneti. Katika jamii ya kisasa media ni njia kuu ya kushirikisha watu wengi na mambo yote yanayoathiri umma, jamii, siasa, uchumi na utamaduni wake. Penye mfumo wa kisiasa ya demokrasia upatikanaji wa habari huru, nyingi na tofauti ni muhimu sana kwa uwiano sawa kati ya washiriki katika siasa, uchumi na utamaduni. Kutokana na nafasi hii muhimu uandishi wa habari ...

                                               

Habari uongo

Habari uongo ni aina ya habari au taarifa za upotoshwaji ambazo hufanyika kwa makusudi kwenye mitandao wa kijamii au katika magazeti.

                                               

Habari Leo

Habari Leo ni gazeti la kila siku kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania linalotolewa kwa lugha ya Kiswahili. Ni gazeti mojawapo linaloandikwa kwa Kiswahili lenye wasomaji wengi katika Tanzania. Gazeti hili ni mali ya kampuni ya hisa ya Tanzania Standard Newspapers Limited.

                                               

Usimulizi wa habari

Aina ya tukio - msimuliaji anatakiwa kubainisha katika maelezo yake aina ya tukio. Mahali pa tukio - ili msikilizaji aweze kuelewa ile habari lazima msimuliaji aweze kumuelewesha tukio lilifanyika/lilitendeka sehemu gani. Wakati/muda - katika usimulizi ni muhimu pia kutaja tukio lilifanyika muda gani. Wahusika wa tukio - ni muhimu kutaja tukio lilifanywa na watu gani, jinsia zao, wingi wao, umri wao n.k. Chanzo cha tukio - ni muhimu kujua chanzo/vyanzo vya tukio, yaani tukio lilifanyajwe na chanzo chake ni nini. Athari za tukio - athari za tukio nazo ni sharti zibainishwe. Hatima ya tukio ...

                                               

BBC

British Broadcasting Corporation BBC ni shirika la utangazaji la Uingereza. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1922 kwa jina la British Broadcasting Company Ltd kama kampuni binafsi. Baadaye mwaka 1927 lilibadilishwa hadhi yake na kuwa shirika la umma. BBC ndio shirika la habari kubwa kuliko yote duniani likiwa linatoa habari na taarifa mbalimbali kwa njia ya redio, runinga na intaneti. Tangu mwaka 1957 imerusha habari kwa Kiswahili pia.

                                               

Gazeti

Gazeti ni karatasi zilizochapishwa habari na kutolewa mara kwa mara ama kila siku au kila wiki; kuna pia magazeti yanayotolewa mara moja au mbili kwa mwezi tu.

                                               

Shule ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma

Shule ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma ni moja kati ya shule kuu zinazopatika chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, inayotoa masomo ya uandishi wa habari na mahusiano ya umma. Ilianzishwa rasmi tarehe 1 Aprili 2009.

                                               

Intaneti

Intaneti ni mfumo wa kushirikiana kwa kompyuta nyingi unaowezesha tarakilishi mbalimbali duniani kuwasiliana kati yake. Kupiti le-corps.coma mtandao huo, watu huweza kutembelea tovuti mbalimbali, kupiga gumzo, na kuandikiana barua pepe. Intaneti ni mfumo wa kimataifa wa mitandao ya kompyuta inayotumia itifaki inayokubalika ya intanet Suite TCP/IP kutumikia mabilioni ya watumiaji duniani kote. Ni mtandao wa mitandao ambayo ina mamilioni ya mitandao binafsi, mitandao ya umma, mitandao ya elimu, mitandao ya biashara, na mitandao ya serikali zenye upana wa kimitaa na kiulimwengu ambazo zimeung ...

                                               

Nadharia ya njama

Nadharia ya njama ni masimulizi yanayodai kwamba kundi la watu wamepatana kwa siri kufanya mambo haramu au mabaya na kuyaficha mbele ya umma. Nadharia za njama kwa kawaida zina ushahidi mdogo au zinakosa ushahidi wowote. Kuna pia nadharia za njama zinazorejelea matukio halisi lakini kuzieleza kutokana na njama isiyojulikana na watu wengi. Nadharia nyingi za njama zinadai kwamba matukio fulani ya kihistoria hayakutokea jinsi yanavyoelezwa katika vitabu vya historia bali kufuatana na njama fulani.

                                               

Propaganda

Propaganda ni jitihada ya kuathiri mawazo na maoni katika jamii kwenda mwelekeo unaotakiwa na wenye propaganda. Inafanana na njia zinazotumiwa kwa matangazo ya kiuchumi yanayolenga kuuza bidhaa fulani au kusambaza mafundisho ya kidini lakini eneo la propaganda ni kisiasa. Kwa hiyo mara nyingi sehemu muhimu ya propaganda ni kuchora picha baya ya wapinzani au maadui. Jambo muhimu katika propaganda ni kuonyesha habari jinsi inavyofaa zaidi kwa kuathiri watu si kuonyesha hali jinsi ilivyo au pande mbalimbali ya hali halisi. Harakati ya kisiasa kama Ukomunisti au Ufashisti zilitumia propaganda ...

                                               

Taarifa

Taarifa ni habari maalumu inayowasilishwa ama kwa mdomo ama kwa maandishi. Pia ni takwimu zilizochakatwa ambazo zina maana kamili inayoweza kutumika katika kufanya maamuzi fulani. Mfano: Orodha ya namba shufwa 2, 4, 6. ni taarifa. 1, 2, 3, 4, 5, 6. ni takwimu. Lakini Taarifa hutofautiana kulingana na muktadha kama ilivyo kwa takwimu. Taarifa ya habari ni wasilisho la maelezo ya tukio au hali maalumu kwa jamii nzima linalopitia njia yoyote: redio, gazeti, runinga, mbiu au mikutano.

                                               

Tarakilishi

Tarakilishi au Kompyuta ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wa kupokea na kukusanya taarifa, na halafu kuzishughulikia kulingana na kanuni za programu ya kompyuta inayopewa. Inafuata hatua za mantiki katika kazi hii. Hapo hutoa matokeo ya kazi hiyo na namna ilivyoendeshwa, pamoja na kutoa matokeo ya kitu kilichofanyika, yaani kinachoonekana kwa haraka.

                                               

Televisheni

Televisheni au runinga ni chombo chenye kiwambo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti. Neno "televisheni" linatokana na maneno mawili: tele kutoka Kigiriki: kwa mbali sana na visio (kutoka Kilatini: mwono ; kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza television lililotoholewa katika Kiswahili televisheni.

                                               

Tovuti

Tovuti ni mkusanyiko wa kurasa zilizoandikwa kwa lugha mbalimbali za tarakilishi kama vile HTML, PHP, XHTML na kadhalika na ambazo kwa pamoja hujumuika katika kutoa habari au maelezo kuhusu jambo fulani. Lugha hizi, yaani HTML, PHP, XHTML na kadhalika zinaweza tu kusomwa na kutafsiriwa na programu kama vile Internet Explorer Google Chrome na Mozilla Firefox kwa lugha ambayo inaweza kueleweka na binadamu. Wingi wake ni "tovuti" vile vile. Tovuti zote pamoja zinaitwa "mtandao" au "Intaneti" au "wavuti".

                                     

ⓘ Habari

  • Uzushi ni hali ya kueneza habari zisizo na ukweli au habari za uongo kabisa. Mtu anayeeneza uzushi huwa na madhumuni ya kumdhalilisha mwingine, kumuharibia
  • yanayotumika katika ufahamu au kifungu cha habari fulani. Kwa kawaida msamiati huwa unafafanuliwa kwa kusoma kifungu cha habari hicho. Vilevile msamiati tunaweza
  • data Vyombo vya habari vya kutangaza, vyombo vya habari mbalimbali, habari ya kutangazwa, kununua na kuweka kwa utangazaji Vyombo vya habari vya kielektroniki
  • ya fahamu, ni kundi la seli za pekee mwilini zenye kazi ya kuwasilisha habari kati ya ubongo na sehemu za mwili. Tukigusa kitu cha moto kwa kidole, tunaondoa
  • la Kilatini Datum ambayo kutumika kwa nadra inamaanisha makundi ya habari Data kwa kawaida ni matokeo ya vipimo na inaweza kuwa msingi wa jedwali
  • Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009. Habari za historia ya Wakamba Habari za mlima Kituluni karibu na Machakos Archived Januari 15
  • elimu ya data. Data ni habari juu ya watu, nchi, uchumi, matukio au hali ya vitu mbalimbali. Takwimu inakusanya na kuangalia habari nyingi za aina hiyo ikijaribu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
                                               

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Wizara ya Habari, Utamudini na Michezo) ni wizara ya serikali nchini Tanzania. Ofisi kuu ya wizara hii zipo mjini Dar es Salaam.

                                               

Shirikisho la vyombo vya habari

Shirikisho la vyombo vya habari inaelezea makampuni yanayomiliki idadi kubwa ya makampuni katika nyanja mbalimbali za vyombo vya habari kama vile televisheni, redio, uchapishaji, filamu, na hata Intaneti. Pia hutajwa kama asasi ya vyombo vya habari au kundi la vyombo vya habari. Na kwa mwaka wa 2008, The Walt Disney Company imekuwa moja kati ya shirikisho la vyombo vya habari lililo kubwa zaidi duniani, ikiwa ni pamoja na News Corporation, Viacom na Time Warner.

Users also searched:

bbc habari, taarifa ya habari itv leo asubuhi, taarifa ya habari leo 2021,

...
...
...