Back

ⓘ Uchumi - Uchumi, Supamaketi za Uchumi, Somo la Uchumi, Maduka Makubwa, London School of Economics, Kilimo, Wizara ya Fedha na Uchumi, Maliasili, Bajeti, Bei ..
                                               

Uchumi

Uchumi ni jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao. Ni hasa uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali. Uchumi mara nyingi hutazamwa kwenye ngazi za kijiji, eneo, taifa au dunia. Sayansi ya Uchumi kwa Kiingereza economics ni tawi la elimu inayochunguza masharti ya uchumi kufaulu au kushindwa.

                                               

Supamaketi za Uchumi

Supamaketi za Uchumi ni mtandao wa supamaketi nchini Kenya ulioanzishwa mwaka wa 1975 na uliorodheshwa katika Soko la Hisa la Nairobi mwaka wa 1992.

                                               

Somo la Uchumi

Somo la uchumi ni sayansi ya kijamii ambayo hutafiti uzalishaji, usambazaji, na matumizi ya bidhaa na huduma. Neno uchumi linatokana na kitenzi "kuchuma". Jina la Kiingereza economy linatokana na neno la Kigiriki cha Kale oikonomia lenye maana ya "usimamizi wa kaya, utawala", kwa hiyo "sheria za nyumba kaya". Aina za masomo ya kiuchumi ya kisasa zilizotokana na somo pana la uchumi wa kisiasa katika miaka ya mwisho ya karne ya 19, kutokana na matamanio ya kuchukua mwelekeo jarabati unaofaa zaidi sayansi za kiasilia. Ufafanuzi unaojumuisha mengi ya masomo ya kiuchumi ya kisasa ni ule wa Lion ...

                                               

Uchumi Maduka Makubwa

Uchumi Maduka makubwa ni mfuatano wa maduka makubwa Kenya ambayo ilianzishwa mwaka 1975 na ambayo iliorodheshwa kwenye Soko la hisa la Nairobi mwaka 1992. Jina Uchumi maana yake ni "economy" katika kiingereza.

                                               

London School of Economics

Chuo kilianzishwa mwaka 1895 mjini London na leo hii ni sehemu ya Chuo Kikuu cha London. Hasa idara ya uchumi ina sifa za kimataifa. Zaidi ya wakuu wa dola 39 walisoma katika chuo hiki na 8 kati yao wanashika nafasi ya mkuu wa nchi mwaka 2007. Maprofesa pamoja na waliopata digrii chuoni hapa jumla 14 walipokea tuzo ya Nobel ya uchumi, amani au fasihi. Nafasi za kuendesha utafiti pamoja na nafasi kwa ajili ya wanafunzi huhesabiwa kati ya bora kabisa duniani.

                                               

Kilimo

Kilimo ni uzalishaji wa mazao kwenye mashamba. Kilimo kina maana pana inayojumuisha mifumo ya uzalishaji mimea, ufugaji wa wanyama, na uvuvi wa samaki. Mara nyingi kilimo cha mimea kinaenda sambamba na ufugaji wa wanyama. Watu hupanda mimea na kuitunza hadi mavuno hasa kwa uzalishaji wa chakula cha binadamu na lishe ya wanyama, lakini pia kwa shabaha ya kupata malighafi mbalimbali zinazotumiwa kwa kutengeneza nguo za watu. Siku hizi kilimo kinalenga pia nishati ya mimea. Mtu anayejihusisha na kilimo huitwa mkulima.

                                     

ⓘ Uchumi

  • binadamu ambazo ni lazima kutimizwa. Taratibu hizi zinaweza kuwa za afya, uchumi biashara, kilimo, dini n.k. Mfano wa kanuni za afya: Nawa mikono kabla
  • uwezo mkubwa wa kiuchumi. Kama California ingekuwa nchi huru ya kujitegemea uchumi wake ungekuwa na nafasi ya 8 duniani. Utalii, kilimo na viwanda vya ndege
  • Mteja wakati mwingine hujulikana kama mnunuzi katika mauzo, biashara na uchumi ndiye mpokeaji wa huduma, bidhaa, au wazo kutoka kwa muuzaji kupitia shughuli
  • msukumo au mgongano wa vitu ambao unatoa nishati na unaitwa kani katika uchumi ni rasilimali au fedha za mtu katika elimu jamii ni tunda la mshikamano
  • na kutawala maeneo ya mbali yanayokaliwa na watu wengine kwa nyanja za uchumi utamaduni na jamii. Maeneo hayo yanaweza kuitwa makoloni ya kawaida au
  • 1946 alikuwa mtaalamu wa hisabati na uchumi kutoka nchini Uingereza. Yeye ni maarufu kwa mafundisho yake juu ya uchumi yaliyo na athira kubwa katika siasa
  • pili, kwa sababu ni muhimu sana kwenye nyanja za mawasiliano, sayansi na uchumi wa kimataifa. Lugha ya Kiingereza ilianzia huko Uingereza kutokana na kuingiliana
  • ng ambo la Uingereza. Visiwa hivyo viko karibu na Bahamas. Uvuvi ni msingi wa uchumi Hiki ni kisiwa kikuu penye uwanja wa ndege na ofisi za serikali. Ni kisiwa
  • Mazingira ya Mbale kuna kahawa nyingi na pia kilimo cha mazao mengine. Hivyo uchumi wa mji umetegemea kilimo na biashara ya mazao. Kuna pia kiwanda cha maziwa
  • watu kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo. Kampuni zinapatikana sana katika uchumi wa kibepari, nyingi zikiwa zinamilikiwa na watu binafsi kwa ajili ya kupata
Wizara ya Fedha na Uchumi
                                               

Wizara ya Fedha na Uchumi

Wizara ya Fedha na Uchumi) ni wizara ya serikali nchini Tanzania. Ofisi kuu ya wizara hii zipo mjini Dar es Salaam.

Maliasili
                                               

Maliasili

Maliasili ni vitu ambavyo watu au taifa hawajatengeneza, ila vipo nao huvitegemea kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa taifa husika. Kwa mfano Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi ambazo ni kama mbuga za wanyama, madini na mengine mengi. Suala ni hizo maliasili zinatumikaje katika kuendeleza uchumi wa nchi. Ingewekeza katika uendelezaji wa maliasili, nchi ingekuwa na uchumi wa hali ya juu. Pia wananchi wanatakiwa kuzitunza na kuzijali ili zitumike vyema katika ukuaji wa uchumi wetu.

Bajeti
                                               

Bajeti

Bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha katika kipindi fulani ili kuhakikisha mipango inafanikiwa kwa wakati uliotarajiwa.

Bei
                                               

Bei

Bei inaweza kufafanuliwa namna tofauti. Pengine ufafanuzi rahisi ni kusema "bei ni thamani ya bidhaa au huduma". Bei inaonyeshwa kwa bidhaa nyingine, huduma, au kwa pesa.

Bidhaa
                                               

Bidhaa

Bidhaa ni kitu chochote kinachotoka kwenye soko na kinachoweza kuridhisha watu. Kwenye utengenezaji kwa kawaida hununuliwa kama malighafi kama vile vyuma na kuuzwa kama bidhaa. Bidhaa hatarishi ni zile zinazoweza kusababisha madhara kwa jamii. Mazao ya kilimo na huduma ni aina nyingine ya bidhaa kuu.

Bima
                                               

Bima

Bima ni njia ya ulinzi wa kiuchumi dhidi ya hasara ya kifedha au hata dhidi ya kifo ambayo watu au kampuni wanafuata kwa kulipa kiasi fulani kwa shirika la bima kadiri ya mkataba maalumu, hivi kwamba shida ikitokea shirika litoe fidia.

                                               

Chumvini

Chumvini ni mahali ambapo chumvi huvunwa kwa wingi. Nchini Tanzania chumvi huvunwa hasa katika mkoa wa Lindi na mikoa mingine mingi yenye bahari. Chumvi hutolewa ikiwa ya mawe na hupelekwa viwandani kwa ajili ya kusagwa na pengine kuongezewa madini mbalimbali kama kalisium, iodini n.k.

                                               

Fidia ya kifedha

Fidia ya kifedha inamaanisha kitendo cha kumpatia mtu pesa au vitu vingine vyenye thamani ya kiuchumi badala ya bidhaa zake, malipo ya kazi aliyofanya, au kulipia gharama za hasara ambayo amepata. Aina ya fidia ya kifedha ni pamoja na: Uharibifu Ujira Malipo Fidia ya utaifishaji inayolipwa kukitokea kutaifishwa kwa mali Fidia iliyoahirishwa Fidia ya mtendaji Mirabaha Mshahara Faida za mfanyakazi Fidia ya wafanyakazi, kulinda wafanyakazi ambao wamepata majeraha yanayohusiana na kazi

Ingizo la shajara
                                               

Ingizo la shajara

Katika biashara, ingizo la shajara ni tendo la kuzishika au kuzirekodi shughuli za kibiashara za kiuchumi au zile zisizo za kiuchumi.

                                               

Kipato

Kipato ni kitu chochote au malipo anayopata mtu baada ya kufanya kazi fulani. Kila mmoja lazima awe na kipato chake, haijalishi ni kiasi gani, tena kipato cha mtu ni siri yake mwenyewe. Hata hivyo watafiti wanajitahidi kujua kipato cha taifa zima na cha wastani wa wananchi wake ili kuratibu uchumi n.k.

Users also searched:

...
...
...