Back

ⓘ Kiebrania. Lugha ya Kiebrania ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel. Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani. Kiebran ..
Kiebrania
                                     

ⓘ Kiebrania

Lugha ya Kiebrania ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel. Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

                                     

1. Lugha za Kisemiti

Lugha ya Kiebrania pamoja na zile za Kiarabu, Kiaramu na Kiamhari Ethiopia zinatokana na asili moja ya lugha ya Kisemiti. Kuna lugha nyingi ambazo zinatokana na asili hiyohiyo kama Kiashuru, Kifoinike, Kikaldayo na kadhalika.

                                     

2. Mwandiko wa Kiebrania

Makala Kuu: Mwandiko wa Kiebrania

Mwandiko wa lugha hiyo hufanywa kwa mwandiko wa pekee unaojulikana tangu miaka 3.000. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi. Tabia hii ni sawa na alfabeti nyingine za Kisemiti kama Kiaramu au Kiarabu.

Mfano: Jina la Abrahamu huandikwa אַבְרָהָ֛ם ambazo ni herufi "aBRHM" pekee; Alef ambayo ni herufi la kwanza tena si "a" kwa hakika. Vokali zinaweza kuonyeshwa kwa nukta na mistari chini ya herufi lakini mara nyingi haziandikwi.

                                     

3. Historia

Kiebrania kilikuwa lugha ya Israeli ya Kale wakati wa Biblia kuanza kuandikwa. Baada ya Uhamisho wa Babeli Wayahudi walianza kutumia Kiaramu, na polepole Kiebrania hakikuzungumzwa tena, lakini kilifundishwa kama lugha ya kidini. Wayahudi wa kawaida walikitumia katika ibada na wataalamu waliandika vitabu kwa lugha hiyo.

Katika karne ya 20 Wayahudi wa Ulaya waliamua kukifufua kama lugha hai. Kimekuwa lugha ya nchi mpya ya Israel tangu 1948. Watu waliohamia Israel kutoka mahali pengi duniani walijifunza Kiebrania na watoto wao wameishika kama lugha yao ya kawaida.

                                     

4. Viungo vya nje

 • Ghilad Zuckermann 2003, Language Contact and Lexical Enrichment in Israeli Hebrew. Palgrave Macmillan. ISBN 978-1403917232.
 • makala za OLAC kuhusu Kiebrania
 • lugha ya Kiebrania katika Glottolog
 • Muhtasari kuhusu Kiebrania kwenye Ethnologue
 • Modern Hebrew resources
                                     
 • Neno nabii kwa Kiebrania נביא nevì, kwa wingi נ ב יא ים nevi ìm, kwa Kiarabu نبي linatumika kumtajia binadamu anayesema kwa niaba ya Mungu, hasa kwa
 • Yosef Agnon 17 Julai 1888 17 Februari 1970 au שמואל יוסף עגנון kwa Kiebrania alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Israel. Alizaliwa nchini Poland na jina
 • Emanueli au kwa Kiebrania ע מ נו א ל, Immanuel, yaani, Mungu pamoja nasi ni jina la Kiebrania lililotajwa na nabii Isaya Isa 7: 13 - 16 kama ishara
 • Abigaili kwa Kiebrania אביגיל alikuwa mke wa Mfalme Daudi wa Israeli. Alimzalia mwana aliyeitwa Kileabu. Ametajwa katika Biblia ya Kiebrania ambayo ni
 • kinashika nafasi ya kwanza kati ya vitabu vya kinabii vya Tanakh Biblia ya Kiebrania na vya Agano la Kale ambayo ndiyo sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo
 • Kiarabu: فلسطين filastīn, falastīn kutoka Kilatini: Palaestina kwa Kiebrania פלשתינה Palestina ni jina la eneo lililoko upande wa Mashariki wa Bahari
 • Amnoni kwa Kiebrania אמנון alikuwa mwana wa Mfalme Daudi wa Israeli. Mama yake alikuwa Ahinoamu. Ametajwa katika Biblia ya Kiebrania ambayo ni sehemu
 • Biblia ya Kiebrania תנ ך, Tanakh, kifupisho kinachounganisha herufi tatu T - N - Kh ambazo ni mianzo ya maneno matatu ya Kiebrania yanayotaja
 • Wimbo Ulio Bora kwa Kiebrania שיר השירים, Shir ha - Shirim ni kitabu kimojawapo cha Tanakh Biblia ya Kiebrania na hivyo pia cha Agano la Kale katika

Users also searched:

...
...
...