Back

ⓘ Karafuu ni matumba makavu ya mikarafuu ambayo ni miti ya familia ya Myrtaceae. Karafuu hutumiwa kama kiungo cha chakula na chanzo cha mafuta yenye harufu inayop ..
Karafuu
                                     

ⓘ Karafuu

Karafuu ni matumba makavu ya mikarafuu ambayo ni miti ya familia ya Myrtaceae.

Karafuu hutumiwa kama kiungo cha chakula na chanzo cha mafuta yenye harufu inayopendwa na watu wengi.

Asili ya mti na pia matumizi ya matumba ni visiwa vya Indonesia. Katika karne ya 19 mikarafuu ilipelekwa Unguja na Pemba hasa na mtawala wa Omani na kuanzisha uzalishaji mkubwa saa wa karafuu kwenye visiwa hivi.

                                     

1. Matumizi

Karafuu hutumiwa katika upishi wa nchi nyingi za Asia, Afrika, Ulaya na hata Amerika. Hutumiwa katika kupika nyama, curry na michuzi mbalimbali pamoja na kupika matunda pamoja na vinywaji. Ni kiungo cha lazima kwenye pilau.

Hutafunwa pia mdomoni kuboresha harufu ya pumzi.

Kutafuna karafuu ni dawa ya kupunguza maumivu ya meno.

Nchini Indonesia sigara huungwa na mafuta ya karafuu.

                                     

2. Historia

Karafuu zilifanyiwa biashara tangu kale. Kuna ushuhuda wa karafuu katika chombo kilichopatikana nchini Syria kilichogunduliwa kuachwa huko mnamo mwaka 1721 KK.

Kuna taarifa ya kwamba mtawala nchini China alitaka watu wanaotaka kuongea naye watafune karafuu ili wawe na pumzi ya kupendeza.

Katika karne ya 17 karafuu ilikuwa kati ya vivutio vya kiuchumi vilivyoleta Uholanzi kuanzisha makoloni yake kwenye visiwa vya Indonesia.

Katika karne ya 18 Mfaransa Pierre Poivre alifaulu kuiba miche ya mikarafuu na kuipeleka Morisi ambako Wafaransa walianzisha kilimo hicho.

Soko la karafuu lilikua duniani na hii ilikuwa changamoto ya Sultani wa Omani kupeleka miti hiyo Unguja na Pemba iliyoendelea kuwa nchi ya kuzalisha karafuu nyingi zaidi duniani na kuunda utajiri wa Zanzibar ilhali kilimo hicho kilichochangia pia katika biashara ya watumwa waliotumiwa kuzalisha zao hili katika karne ya 19.

Mapato ya karafuu yalimsababisha Said bin Sultani kuhamisha makao makuu yake Unguja na baada ya kifo chake Usultani wa Zanzibar ulianzishwa kama nchi ya pekee na Omani.

                                     
 • huitwa karafuu na kutumika kwa kiungo katika aina nyingi za chakula. Vikonyo vya maua huitwa makonyo na hutumika kama mbadala rahisi wa karafuu Majani
 • harufu maalumu katika chakula. Mifano yake ni chumvi, kitunguu, iliki, karafuu au pilipili. Viungo vingi kwa asili ni mbegu, matunda, majani au mizizi
 • na uvuvi kwenye Bahari ya Hindi, ni maarufu pia kwa kilimo cha zao la karafuu zao linalokifanya Kisiwa cha Zanzibar kujulikana zaidi kama kisiwa cha
 • wa Maka. Baada ya kupata uhuru mwaka 1963 usultani uliongeza alama ya karafuu katika bendera yake. Zanzibar yawa na bendera yake Flags of the World
 • wanajishughulisha na uvuvi na kilimo. Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna kilimo cha karafuu Upande wa magharibi utalii umeanza kuwa muhimu. Eneo la Ras Nungwi ni
 • Wananchi wa kata ya Kibungo ni wakulima wa mazao ya biashara kama vile karafuu hiriki, tangawizi, bizari, ndizi, lakini wanalima pia mazao ya chakula
 • Baadhi ya bidhaa za biashara zilizopatikana hapo ni meno ya ndovu, watumwa, karafuu sandarasi, simbi na bidhaa za kutoka nje kama vile nguo za pamba, shanga
 • wa Pemba ni hasa kilimo pamoja na uvuvi. Mazao ya sokoni hulimwa hasa karafuu Katika utamaduni wa Pemba kuna desturi ya kipekee katika Afrika ndiyo
 • ardhi yenye rutba na upatikanaji wa kazi ya watumwa akianzisha kilimo cha karafuu Marekani: Kitabu cha Mormoni chatolewa na Joseph Smith, Mdogo anayedai
 • mazao muhimu ya kibiashara ya Tanzania Bara kwa pamba na Zanzibar kwa karafuu Kanda njano ya maandishi chini ya ngao huonyesha wito la taifa Uhuru
 • katika pwani za Uswahilini. Sayyid Said aliona nafasi kubwa ya biashara ya karafuu kwa ajili ya soko la Uhindi na kwingineko. Mwaka 1829 akaanzisha mashamba

Users also searched:

...
...
...