Back

ⓘ Kasi, nyota. Nyota ya Kasi ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina ..
Kasi (nyota)
                                     

ⓘ Kasi (nyota)

Nyota ya Kasi ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema الكأس al-ka’s inayomaanisha "bilauri, glasi" kwa kurejea umbo la kundinyota hii ndogo na dhaifu. Ptolemaio aliita "kwenye mguu wa bilauri".

Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa tahajia ya "Alkes".

Alfa Crateris ni jina la Bayer ikiwa ni nyota angavu ya pili katika Batiya ingawa Alfa ni herufi ya kwanza katika Alfabeti ya Kigiriki.

                                     

1. Tabia

Kasi iko kwa umbali wa miakanuru takriban 160 kutoka Jua letu. Mwangaza unaoonekana ni mag 4.2.

Kasi ni nyota jitu jekundu inayoyeyunganisha heli kuwa kaboni na oksijeni katika kiini chake. Spektra yake inaonyesha mistari ya metali mbalimbali ambayo ni dokezo ya kwamba nyota hii ilianza maisha yake katika sehemu za ndani za Njia Nyeupe yaani galaksi yetu.

                                     

2. Viungo vya Nje

 • Alkes Alfa Crateris, kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
 • Crater, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, Star Tales, iliangaliwa Oktoba 2017
 • Constellation Guide:Crater
                                     

3. Marejeo

 • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
 • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 437 online kwenye archive.org
 • Reffert, Sabine; Bergmann, Christoph; Quirrenbach, Andreas; Trifonov, Trifon; Künstler, Andreas 2015. "Precise radial velocities of giant stars. VII. Occurrence rate of giant extrasolar planets as a function of mass and metallicity". Astronomy & Astrophysics. 574: A116. online hapa
 • Ptolemys Almagest, translated and annotated by G.J. Toomer, London 1984, ISBN 0-7156-1588-2 online hapa
                                     
 • Anajulikana kwa kupiga chenga, nguvu, na kasi ya kulipuka. Mbappé alijitokeza wakati wa umri mdogo, akiwa na nyota za vijana wa AS Bondy, INF Clairefontaine
 • reli za kwanza zilimwezesha kuonyesha mabadiliko ya sauti ya chanzo chenye kasi fulani. Wakati wa mapinduzi ya 1848 alihamia Vienna akawa mkurugenzi wa taasisi
 • la anga kwa kusudi la kutaja mahali pa nyota jinsi inayoonekana kwenye anga. Kuna mpangilio tofauti wa nyota kwa makundi katika tamaduni mbalimbali duniani
 • zaidi. Joti alianza kujizolea umaarufu baada ya kujiunga na kikundi cha Nyota Ensemble ambacho kilikuwa kikionyesha ucheshi katika kituo cha ITV. Hata
 • fupi kuliko siku ya dunia yetu, chini ya nusu yake. Kuna tofauti katika kasi ya mzunguko huu kati ya kanda tofauti za Zohali. Kanda ya ikweta linazunguka
 • Kikikaribia Dunia yetu kinaingia katika angahewa na kuanguka chini kwa kasi kubwa sana. Njiani kinapashwa moto kutokana na msuguano wa hewa dhidi yake
 • cha siku saba angalia Juma Wiki kutoka neno la Kihawaii linanomaanisha kasi Wiki imetafsiriwa na watu kimzaha What I Know Is yaani, ninachojua
 • yao. Wakiruka angani, panzi - bahari huwaepuka mbuai wao. Ongezeko hili la kasi na uwezo wa kugeuka haraka ni faida ya kuokoka kwa panzi - bahari ikilinganishwa
 • Alipokea tuzo ya Distinguished Flying Cross yenye nyota mbili za dhahabu, Air Medal yenye nyota tatu za dhahabu, Commendation yenye Combat V kwa ndege

Users also searched:

selh jembe,

...
...
...