Back

ⓘ Kaunti ya Mombasa imeshika nafasi ya wilaya ya Mombasa baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010. Kaunti hii ni mojawapo ya kaunti mbili am ..
Kaunti ya Mombasa
                                     
ⓘ Kaunti ya Mombasa

Kaunti ya Mombasa imeshika nafasi ya wilaya ya Mombasa baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010. Kaunti hii ni mojawapo ya kaunti mbili ambazo pia ni jiji na ndio kaunti ndogo kabisa kati ya kaunti zote. Makao makuu ya serikali ya kaunti yako katika Jiji la Mombasa. Inapakana na kaunti za Kwale na Kilifi ambazo pamoja na kaunti za Mombasa, Lamu, Tana River na Taita Taveta zilitengeneza Mkoa wa Pwani.

1. Jiografia

Kaunti ya Mombasa inapakana na Bahari Hindi. Ina kisiwa cha Mvita ambacho huwa kati mwa Jiji la Mombasa. Kimetenganishwa na bara na Kijito cha Tudor na Kijito cha Port Reitz. Vijito hivi hugawanywa na Makupa Causeway. Maeneo hayo mengine ya bara yameunganishwa kwa feri na daraja. Ardhi yake ni bapa.

Lindi la Bandari ya Kilindini, lenye kina cha mita 45-55, huiwezesha kuegeshwa meli kubwa.

Mombasa ina misitu asilia mitatu ambayo ni 6% ya misitu ya mikoko ya Kenya. Misitu hii ni mojawapo ya makazi ya wanyamapori katika kaunti hii. Hata hivyo, uvunaji kupindukia wa miti, maeneo taka na kupanua ardhi baharini kumeharibu misitu hii na kuathiri wanyamapori wa majini na ardhini.

Kaunti ya Mombasa ina tabianchi ya tropiki. Kwa kuwa iko kando na bahari, kiwango cha unyevuanga huwa juu. Hali ya hewa hutegemea pepo za monsuni. Kaunti hupata misimu miwili ya mvua: Aprili hadi Juni na Oktoba hadi Disemba.

Kubadilika kwa wastani wa hali ya hewa kumesababisha kiwango cha upwaji wa bahari kupanda na kuongezeka kwa halijoto, mambo ambayo yanatishia jiji la Mombasa na turathi ya Fort Jesus. Pia, mafuriko ya pwani, mmomonyoko katika fuko na kutoweka kwa mwamba tumbawe kumesababishwa na mabadiliko haya.

2. Uchumi

Uchumi wa Mombasa na nchi ya Kenya kwa jumla hutegemea sana bandari ya Mombasa. Bandari ya Mombasa ndio bandari kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Bidhaa nyingi hupitia hapo kutoka na kuingia ndani ya nchi. Bandari hii pia hutegemewa na nchi ya Uganda, Burundi, Sudani Kusini, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda kupitisha bidhaa kama vile, mafuta.

Mombasa pia ni kituo kikuu cha utalii kwa sababu ya fuko zake zenye mchanga, Fort Jesus na Mji wa Kale. Baada ya mashambulizi kadhaa ya kigaidi katika miaka ya awali ya mwongo wa 2010 na Al Shabaab na vikundi vingine, utalii ulidorora. Nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa pamoja na nchi zingine za magharibi zilianza kutoa tahadhari za safari. Baada ya Operesheni Linda Nchi, na juhudi za polisi kukumbana na ugaidi, juhudi zinaelekezwa kuimarisha utalii tena. Pia, kuanzishwa kwa huduma ya reli mpya ya SGR kati ya Jiji la Mombasa na Nairobi, kumeongeza idadi ya watalii wa ndani.

Mnada wa Chai wa Mombasa ni mojawapo ya vituo vya unadi wa chai katika dunia. Mnada huu hunadi chai kutoka nchi za Kenya, Tanzania, Uganda Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Madagaska, Zambia na Zimbabwe. Kufikia mwaka wa 2017, ulikuwa soko ya pili kwa ukubwa ya uuzaji wa chai katika dunia.

3. Maeneo bunge

Kaunti ya mombasa ina maeneo bunge yafuatayo:

Mratibu wa Pwani huketi katika kaunti ya Mombasa. Ana jukumu za kuratibu na kuendesha shughuli, k.v. usalama, kwa niaba ya serikali kuu.

  • unapatikana katika kaunti ya Mombasa kusini mashariki mwa Kenya kwenye bahari ya Hindi Mito ya Kenya Orodha ya mito ya kaunti ya Mombasa Geonames.org

  • mojawapo ya Majimbo 210 ya Uchaguzi nchini Kenya. Jimbo hili linapatikana katika Kaunti ya Mombasa likiwa miongoni mwa majimbo sita ya kaunti hiyo. Jimbo
  • moja kati ya Majimbo 210 ya uchaguzi Nchini Kenya. Jimbo hili linapatikana katika Kaunti ya Mombasa miongoni mwa majimbo manne katika kaunti hiyo. Lina
  • Jimbo hili ni mojawapo ya Majimbo manne katika Kaunti ya Mombasa Eneo lote la Jimbo hili iko chini ya Baraza la munisipali ya Mombasa Jimbo hili lilianzishwa

Users also searched:

...
...
...