Back

ⓘ Khanga ni vazi au nguo nyepesi pia ndefu ya rangi ambayo hupendwa kuvaliwa na wanawake, hasa nchi za Afrika Mashariki na Afrika Magharibi. Kanga inafanana na ki ..
Khanga
                                     

ⓘ Khanga

Khanga ni vazi au nguo nyepesi pia ndefu ya rangi ambayo hupendwa kuvaliwa na wanawake, hasa nchi za Afrika Mashariki na Afrika Magharibi. Kanga inafanana na kikoi ambacho kawaida huvaliwa na wanaume.

Kwa kawaida kanga huwa na upana wa sentimita 150 na urefu wa sentimita 110. Kanga huweza kutumiwa kama vazi rasmi, kitambaa cha kichwani, taulo, kitambaa cha mezani na kwa shughuli mbalimbali kama kubeba watoto au kubeba mizigo kichwani.

Hutumiwa pia kama zawadi kwenye sherehe za kuzaliwa, harusi, n.k. Hutolewa pia kwa familia iliyofiwa na ndugu yao nchini Tanzania.

Mwanzoni kanga ilikuwa ikirembwa kwa vitone vidogo ambavyo vilionekana na manyonya ya ndege aina ya kanga. Ndiyo sababu ilipewa jina hili.

Kanga huwa na sehemu tatu: pindo, mji sehemu ya kati, na ujumbe. Ujumbe mara nyingi huwa ni kitendawili au fumbo.

Hii ni mifano ya ujumbe wa kwenye kangaː

 • Leo ni siku ya shangwe na vigelegele
 • Majivuno hayafai f
 • Fimbo la mnyonge halina nguvu
 • Wazazi ni dhahabu kuwatunza ni thawabu
 • Mkipendana mambo huwa sawa
 • Sisi sote abiria dereva ni Mungu
 • Japo sipati tamaa sikati
 • Naogopa simba na meno yake siogopi mtu kwa maneno yake.
 • Mwanamke mazingira tunataka, usawa, amani, maendeleo
                                     
 • linatokana na Kiarabu جوزاء jawza inayomaanisha pia mapacha Mifano ya jozi za kawaida ni viatu, soksi, macho. Khanga zinauzwa mara nyingi kwa jozi.
 • Miscounted Dreams Oil On Water Shattered Dreams Stupid Women Stains on My Khanga Mkusanyiko wa hadithi fupi Hadithi Media, Centurion Gauteng, South Africa
 • Kidemokrasia ya Kongo - Tanzania. Pia alifahamika sana kwa wimbo wake Kesi ya Khanga Freddy alianza kufundishwa gitaa na baba yake wakati akiwa na umri wa
 • mchepuko kamwingiza nyumbani kwa mumewe. Alifumwa na Cheusi wakati anatafuta khanga ya kumsitiri mtoto wake. Jambo hili lilimuumiza sana Cheusi. Tangu hapa
 • Mwafrika. Makihiyo anaonekana kushiriki katika michezo ya ngoma na vazi la khanga Mzungu Kichaa Ni Wako Makihiyo na Ben Pol sasa Ni Wako ingizo la tarehe

Users also searched:

...
...
...