Back

ⓘ Ketusi, kundinyota. Ketusi linaenea kwenye pande zote mbili za ikweta ya anga na iko pia karibu na mstari wa ekliptiki. Kundinyota jirani zake ni Samaki, zamani ..
Ketusi (kundinyota)
                                     

ⓘ Ketusi (kundinyota)

Ketusi linaenea kwenye pande zote mbili za ikweta ya anga na iko pia karibu na mstari wa ekliptiki. Kundinyota jirani zake ni Samaki, zamani Hutu, lat. Pisces, Kondoo zamani Hamali, lat. Aries na Nahari Eridanus au mto wa angani.

                                     

1. Jina

Ketusi lilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota kutafuta njia baharini wakati wa usiku.

Jina la Ketusi linatokana na Kiarabu قيطس qaitus ambalo ni umbo la jina asilia la Kigiriki Κήτος Ketos baadaye Cetus kwa tahajia ya Kilatini.Wagiriki wa Kale walitumia jina hili kwa kutaja samaki kubwa sana pamoja na dubwana walioaminiwa kukaa baharini. Jina hili kwa umbo la Kilatini limeendelea kuwa jina la kisayansi kwa oda ya Cetacea nyangumi.

Katika mitholojia ya Kigiriki Ketusi alikuwa dubwana aliyetake kumeza Andromeda kutokana na fitina na Poseidon mungu wa bahari. Shujaa Farisi Perseus aliingia kati akamwokoa Andromeda. Baadaye wote pamoja na mfalme Kifausi na malkia Cassiopeia waliinuliwa angani kama nyota

Ketusi ni kati ya kundinyota lililotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK kwa jina Kassiopeia. Iko pia katika orodha ya kundinyota 88 ya Umoja wa kimataifa wa astronomia kwa jina la Cetus. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni Cet.

                                     

2. Nyota

Ketusi ni kundinyota kubwa lakini halina nyota angavu sana. Nyota angavu zaidi ni β Beta Ceti iliyoitwa Chura lat. Diphda na mabaharia Waswahili. Ina uangavu unaoonekana wa 2.0 ikiwa umbali wa miakanuru 96 kutoka Dunia.

Omikron Ceti inaitwa pia Mira" ajabu” kwa sababu ilikuwa nyota badilifu ya kwanza iliyotambuliwa kuwa vile na wanaastronomia wa Ulaya.

                                     

3. Marejeo

  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 75 ff online hapa kwenye archive.org
                                     
  • kwa hiyo tunaona Kifausi Cepheus jirani na kundinyota za Mke wa Kurusi Cassiopeia na Mara, halafu Ketusi na Farisi aliyekuja kumwokoa Mara katika simulizi
  • upande wa mashariki. Inapaka na kundinyota jirani za Hudhi Auriga Farisi Perseus Hamali Kondoo Aries Ketusi Cetus Nahari Eridanus Jabari
  • nyota angavu Kinywa cha Hutu Formalhaut Linapakana na Dalu Aquarius na Ketusi Cetus upande wa kaskazini, Tanuri Fornax upande wa mashariki, Zoraki
  • kwa Kilatini na Kiingereza ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia yetu. Kundinyota hili ni maarufu kwa umbo lake la M au W
  • jina. Katika mitholojia ya Kigiriki Farisi alikuwa shujaa aliyeua dubwana Ketusi na kumwokoa Andromeda. Baadaye wote pamoja na wazazi wa Andromeda mfalme
  • makundinyota ya Nahari Eridanus upande wa mashariki, kaskazini na kusini, ilhali Ketusi Cetus Najari Sculptor na Zoraki Phoenix ziko upande wa magharibi
  • Beta Ceti, kifupi Beta Cet, β Cet ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Ketusi Cetus Ni pia nyota angavu ya 14 kwenye anga ya usiku. Mwangaza

Users also searched:

...