Back

ⓘ Johann Bayer alikuwa mwanasheria na mwanaastronomia kutoka nchi ya Ujerumani. Alianzisha mfumo unaotumika hadi leo wa kutaja mahali pa nyota angani kufuatana na ..
Johann Bayer
                                     

ⓘ Johann Bayer

Johann Bayer alikuwa mwanasheria na mwanaastronomia kutoka nchi ya Ujerumani. Alianzisha mfumo unaotumika hadi leo wa kutaja mahali pa nyota angani kufuatana na kundinyota na mwangaza unaoonekana. Majina ya Bayer hutumiwa kwa nyota angavu zinazoonekana vema kwa macho matupu.

                                     

1. Maisha

Alizaliwa mwaka 1572 mjini Rain katika Bavaria.

Alipokuwa na miaka 20 alianza masomo yake ya falsafa na sheria katika chuo kikuu cha Ingolstadt.

Baada ya kumaliza masomo yake alihamia Augsburg alipofanya kazi ya mwanasheria akawa mshauri wa kisheria wa halmashauri ya mji kuanzia mwaka 1612.

Nje ya kazi yake alijisomea elimu katika fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na akiolojia, hisabati na astronomia.

Hakuunda familia yake, bali alibaki kapera bila kuoa akafa mwaka 1625.

                                     

2. Kazi

Bayer amekuwa maarufu kwa atlasi yake ya nyota ya Uranometria Omnium Asterismorum" - "Ramani ya anga ya makundinyota yote" iliyochapishwa mara ya kwanza mjini Augsburg mwaka 1603.

Hii ilikuwa ramani ya nyota ya kwanza iliyoonyesha pia nyota zinazoonekana tu kwenye angakusi ya Dunia, kazi iliyowezeshwa na safari za upelelezi tangu meli za Ferdinand Magellan kuzunguka Dunia yote mara ya kwanza mwaka 1521.

Hii ilikuwa atlasi ya kwanza ya nyota yenye ramani 51: moja-moja kwa ajili ya kila kundinyota lilojulikana tangu zamani za Ptolemaio ukurasa unaoonyesha kundinyota mpya kwenye nusutufe ya kusini zilizobuniwa na Petrus Plancius na ramani mbili za angakusi na angakaskazi. Kila ramani ina alama za kuonyesha longitudo na latitudo alizochukua kutoka orodha ya nyota ya Tycho Brahe ambayo haikuchapishwa bado wakati wa kutolewa kwa Uranometria.

Bayer alitumia kazi ya Tycho Brahe, inawezekana alitumia pia atlasi ya nyota ya Alessandro Piccolomini ya mwaka 1540 ingawa Bayer aliongeza zaidi ya nyota 1.000 kwa orodha za watangulizi wake.

Katika kitabu cha Uranometria alianzisha mfumo mpya wa kutaja nyota inayojulikana kama "majina ya Bayer". Humo alipanga kila nyota katika kundinyota fulani. Ndani ya kundinyota aliipa kila nyota herufi ya Kigiriki kufuatana na uangavu: nyota angavu zaidi iliitwa Alfa, iliyofuata Beta, halafu Gamma na kadhalika.

Katika atlasi yake aliingiza makundinyota 12 mpya zilizobuniwa miaka michache iliyopita kutaja nyota za angakusi ambazo hazikujulikana na wataalamu wa Ugiriki ya Kale na Roma ya Kale.

                                     
 • Jina la Bayer kwa Kiingereza Bayer designation ni utaratibu wa kutaja nyota ulioanzishwa na mwanaastronomia Mjerumani Johann Bayer katika karne ya 17
 • ya nyota kilichotolewa mnamo mwaka 1603 na mwanaastronomia Mjerumani Johann Bayer Kwa jumla kulikuwa na ramani 51 zilizoonyesha makundinyota yote yaliyojulikana
 • kwenye ikweta ya anga. Baadaye makundinyota yake yalipokewa vile na Johann Bayer katika orodha yake na kutumiwa hadi leo katika orodha ya Umoja wa Kimataifa
 • yake na mwaka 1603 katika Uranometria atlasi ya nyota iliyotolewa na Johann Bayer iliyoendelea kuwa msingi wa utaratibu wa kutaja nyota unaotumiwa hadi
 • nyota ya Petrus Plancius. Baadaye ilipokelewa katika Uranometria ya Johann Bayer Keyser alitumia jina la Kiholanzi la Het Chameljoen Kinyonga iliyotajwa
 • nyota ya Petrus Plancius na kuingizwa baadaye katika ramani ya nyota ya Johann Bayer iliyokuwa muhimu kwa elimu ya nyota. Keyser alitumia jina la Kiholanzi
 • makundinyota mapya 12 kwenye globu ya nyota yake. Mnamo mwaka 1603 Mjerumani Johann Bayer alibuni mfumo wa kutaja nyota ambao kimsingi unaendelea kutumiwa hadi
 • η Ursae Maioris ni jina la Bayer kufuatana na utaratibu ulioanzishwa na Mjerumani Johann Bayer katika karne ya 17. Bayer aliiona kuwa nyota angavu ya
 • Ilikuwa pia msingi kwa atlasi ya nyota ya Uranometria iliyotolewa na Johann Bayer mnamo 1603. Mwaka 1572 aliona nyota mpya iliyoonekana kwa muda wa mwaka
 • jina la Kilatini Musca Baadaye ilipokelewa katika Uranometria ya Johann Bayer aliyetumia njia ya Apis nyuki na hivyo kuna vitabu vya zamani vinavyotumia
 • globu ya nyota ya Petrus Plancius na kupokelewa katika Uranometria ya Johann Bayer Keyser alitumia jina la Kiholanzi Reygher ndege kama Kingoyo iliyochukuliwa
 • mhimili wa Dunia nyota zake hazionekani tena katika nusutufe ya kaskazini. Johann Bayer alipotunga orodha yake ya nyota bado alizieleza kama sehemu za Kantarusi

Users also searched:

...
...
...