Back

ⓘ Kaa, kundinyota. Kaa ni kundinyota la zodiaki. Ni moja ya makundinyota yanayotambuliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia Nyota za Kaa huwa haziko pamoja kihal ..
Kaa (kundinyota)
                                     

ⓘ Kaa (kundinyota)

Kaa ni kundinyota la zodiaki. Ni moja ya makundinyota yanayotambuliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia

Nyota za Kaa huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Kaa" linaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Dunia.

                                     

1. Jina

Mabaharia Waswahili walijua nyota hizi tangu miaka mingi kwa jina la Saratani wakizitumia kutafuta njia baharini wakati wa usiku.

Jina la Saratani linatokana na Kiarabu سرطان sartan linalomaanisha kaa. Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale waliosema Καρκίνος karnikos kwa maana hiyohiyo na hao walipokea kundinyota hili tayari kutoka Babeli lakini Wababeli waliiona kama alama ya kobe maji.

Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Saratani" limesahauliwa ikiwa kundinyota linaitwa kwa tafsiri tu "Kaa".

Katika vitabu kadhaa vya shule jina la Saratani limetumiwa kutaja sayari ya Zohali kwa kulichanganya na matamshi ya jina la Kiingereza "Saturn".

Jina la zamani, pia jina la Kilatini, ni sawa na ugonjwa wa saratani unaoitwa pia "kansa". Sababu yake ni ya kwamba matibabu wa kale walifananisha uvimbe wa ugonjwa na mnyama kaa na hili ni pia maana ya neno saratani.

                                     

2. Mahali pake

Kaa iko angani kwenye mstari wa Zodiaki kati ya Mapacha zamani Jauza, lat. Gemini upande wa magharibi na Simba zamani Asadi, lat. Leo upande wa mashariki.

                                     

3. Magimba ya angani

Kaa haina nyota angavu sana si rahisi kuiona. Nyota angavu zaidi ni Beta Cancri yenye mwangaza unaoonekana wa 3.8 mag. Umbali wake na dunia ni miakanuru 230. Kuna fungunyota moja inayoonekana kwa macho matupu hii ni M 44 inayoitwa pia Praesepe yenye mwangaza unaoonekana wa 3.7 ikionekana kama doa dogo angavu.

                                     

4. Viungo vya Nje

  • Star Tales – Cancer, tovuti ya Ian Ridpath, iliangaliwa Oktoba 2017
  • Constellation Guide: Cancer constellation
  • Cancer, "Stars", kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
  • The Deep Photographic Guide to the Constellations: Cancer
                                     

5. Marejeo

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 107 ff online kwenye archive.org
  • Dictionary of Symbols, by Carl G. Liungman, W. W. Norton & Company. ISBN 978-0-393-31236-2
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Ian Ridpath and Wil Tirion 2007. Stars and Planets Guide, Collins, London. ISBN 978-0007251209. Princeton University Press, Princeton. ISBN 978-0-691-13556-4.
                                     
  • kwa kusudi la kulingana na kalenda ya miezi 12. Kwa kufikia idadi hii kundinyota la Hawaa Ophiuchus liliondolewa katika idadi ya Zodiaki. Kwa jumla majina

Users also searched:

nyota ya simba, utabiri wa nyota leo,

...
...
...