Back

ⓘ Imhotep na Wagiriki wa Kale; kwa hieroglifi ỉỉ-m-htp anayekuja kwa amani; takriban karne ya 27 KK alikuwa mwandishi na mtaalamu wa Misri ya Kale. Chini ya Farao ..
Imhotep
                                     

ⓘ Imhotep

Imhotep na Wagiriki wa Kale; kwa hieroglifi ỉỉ-m-htp "anayekuja kwa amani"; takriban karne ya 27 KK) alikuwa mwandishi na mtaalamu wa Misri ya Kale.

Chini ya Farao Djoser wa nasaba ya tatu ya Misri Imhotep alikuwa afisa mtendaji mkuu. Anajulikana kama mhusika katika ujenzi wa piramidi ya Djoser.

Mara nyingi anatajwa kama msanifu wa kwanza anayejulikana na pia mhandisi, na tabibu katika historia anayejulikana kwa jina.

Hali halisi hatuna habari kamili juu yake isipokuwa maandishi ya kumsifu yaliyowekwa baada ya kifo chake. Hapo aitajwa kuwa "Mtendaji mkuu wa Farao, tabibu, mwakilishi wa kwanza wa mfalme wa Misri ya Juu, afisa mtawala wa Ikulu Kubwa, Kuhani Mkuu wa Heliopolis, Mjenzi Mkuu, Seremala Mkuu, Mchongaji Mkuu, Mfinyanzi Mkuu"

Baada ya kifo chake aliheshimiwa kama mungu katika hekalu ya Memphis, baadaye pia kama mshairi na mwanafalsafa. Maneno yake yalinukuliwa mara nyingi.

Kaburi lake lilifichwa vema haikujulikana hadi leo hii lakini wengi wanadhani iko mahali fulani huko Saqqara.

                                     

1. Kujisomea

  • Hurry, Jamieson B. 1978. Imhotep, 2nd, New York: AMS Press. ISBN 0-404-13285-5.
  • Risse, Guenther B. 1986. "Imhotep and Medicine - A Reevaluation". Western Journal of Medicine 144: 622–624.
  • Dawson, Warren R. 1929. Magician and Leech: A Study in the Beginnings of Medicine with Special Reference to Ancient Egypt. London: Methuen.
  • Cormack, Maribelle 1965. Imhotep: Builder in Stone. New York: Franklin Watts.
  • Asante, Molefi Kete 2000. The Egyptian philosophers: ancient African voices from Imhotep to Akhenaten. Chicago: African American Images. ISBN 0-913543-66-7.
  • Garry, T. Gerald 1931. Egypt: The Home of the Occult Sciences, with Special Reference to Imhotep, the Mysterious Wise Man and Egyptian God of Medicine. London: John Bale, Sons and Danielsson.
  • Wildung, Dietrich 1977. Egyptian Saints: Deification in Pharaonic Egypt. New York University Press. ISBN 0-8147-9169-7.
                                     
  • elimu jamii na historia. Msanifu wa kwanza anayejulikana kwa jina ni Imhotep wa Misri ya Kale. Mbinu za usanifu hutegemea teknolojia inayopatikana
  • kwa mawe ya gange. Msanifu aliyesimamia ujenzi wa piramidi hiyo aliku wa Imhotep waziri wake na mtendaji mkuuwa farao. Ndani kuna chumba kidogo kinachofikiwa
  • mara nyingi kwa sanamu za kuchongwa zilizohifadhiwa hadi leo. Mwandishi Imhotep aliyekuwa afisa mtendaji mkuu wa farao Djoser alipewa heshima ya kimungu

Users also searched:

...
...
...