Back

ⓘ Jina takatifu la Yesu. Katika Kanisa Katoliki ibada hiyo ilistawi hasa mwishoni mwa karne za kati, sambamba na ile kwa Moyo mtakatifu wa Yesu. Litania ya Jina T ..




Jina takatifu la Yesu
                                     

ⓘ Jina takatifu la Yesu

Katika Kanisa Katoliki ibada hiyo ilistawi hasa mwishoni mwa karne za kati, sambamba na ile kwa Moyo mtakatifu wa Yesu.

Litania ya Jina Takatifu ilitungwa na Wafransisko wa karne ya 15 Bernardino wa Siena na Yohane wa Capistrano walioeneza sana ibada hiyo.

Sikukuu ya Jina Takatifu ilikubaliwa mwaka 1530. Siku hizi inaadhimishwa na Kanisa la Kilatini kama kumbukumbu tarehe 3 Januari.

Hata hivyo heshima kwa jina hilo takatifu ilianza na Ukristo wenyewe taz. Mdo 4:10. Karne hata karne, Wakristo wamelitumia wakiamini lina uwezo wa pekee sana.

Heshima hiyo ilisisitizwa na Mtume Paulo kwa ajili ya wokovu Fil 2:10; taz. Rom 10:3. Kwa kuwa yeye alidai kwa jina la Yesu kila goti lipigwe mbinguni, duniani na kuzimu, imekuwa desturi ya wengi walau kuinamisha kichwa katika kulitaja, kama anavyotakiwa kufanya padri wa Kanisa la Kilatini wakati wa Misa.

Ibada ya namna hiyo ipo katika Ukristo wa mashariki pia k.mf. Sala ya Yesu. Vilevile madhehebu mbalimbali yanaadhimisha sikukuu hiyo kwa jina lilelile la Wakatoliki au kama Tohara ya Yesu, kwa kuwa ndipo alipopatiwa jina, siku ya nane baada ya kuzaliwa.

                                     
  • alikuwa mume wa Bikira Maria na baba mlishi wa Yesu Kristo ambao pamoja naye waliunda Familia takatifu Katika Injili ya Mathayo 13: 5 anatajwa kama
  • Yesu kutolewa hekaluni ni tukio la utoto wake, siku arubaini baada ya kuzaliwa, iliyopangwa na Torati kuwa siku ya kumtakasa mama yeyote aliyemzaa mtoto
  • Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu ya Jina takatifu la Yesu lakini pia za watakatifu Papa Antero, Teopempto na Teona, Gordio
  • Waprotestanti wa wakati huo kuhusu daraja takatifu na ekaristi ulitosha kushirikisha kweli mamlaka ya Mitume wa Yesu Hivyo Kanisa hilo kwa jumla halitambui
  • yake, yaani, Yesu Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu Mdo 19: 3 - 5 Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni kwamba sakramenti
  • Kanisa Katoliki. Kwa kuwa hilo jina ni la pekee kwa Kanisa takatifu mama yetu sote, ambaye ni bibi arusi wa Bwana wetu Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu
  • Walutheri ni jina linalotumika kuwataja kwa jumla wafuasi wa Yesu Kristo wanaozingatia mafundisho yaliyotolewa na Martin Luther katika karne ya 16. Madhehebu
  • 16: 18 na Injili ya Yohane 1: 42 ni Yesu Kristo aliyembadilishia jina akamuita Kefa kwa Kiaramu mwamba jina ambalo lilitafsiriwa kwa Kigiriki Petros

Users also searched:

...
...
...