Back

ⓘ Injili ya Yakobo ni kitabu cha dini ya Ukristo kilichoandikwa kwa Kigiriki miaka 140-170 hivi BK. Pengine kinaitwa majina mengine, mojawapo Kuzaliwa kwa Maria. ..
                                     

ⓘ Injili ya Yakobo

Injili ya Yakobo ni kitabu cha dini ya Ukristo kilichoandikwa kwa Kigiriki miaka 140-170 hivi BK.

Pengine kinaitwa majina mengine, mojawapo "Kuzaliwa kwa Maria". Hii ni kwa sababu kinasimulia hasa uzazi sura 1-8 na utoto wa Bikira Maria sura 9-16, mbali ya utoto na uzazi wa Yesu sura 17-24.

Ni cha kwanza kusema juu ya ubikira wake wakati wa kumzaa Yesu na baada ya hapo.

Ingawa mwandishi anajidai kuwa Yakobo Mdogo, wataalamu wanapinga neno hilo. Ingawa kitabu kilienea sana na kubaki hadi leo katika nakala nyingi za tafsiri mbalimbali, hakikukubaliwa kama sehemu ya Biblia ya Kikristo. Sababu kuu inaweza kuwa ile ya kuchelewa kutungwa, baada ya wakati wa Mitume wa Yesu kwisha.

Baadhi ya masimulizi ya kitabu hicho yameingia katika Kurani na katika desturi za Kikristo, kama vile Pango la Noeli wakati wa Kuzaliwa kwa Yesu ambalo kwa kawaida linaonyesha uwepo wa ngombe na punda kama inavyosimuliwa na Injili ya Yakobo 18.

                                     
  • ushuhuda wa Mitume wa Yesu na maandiko ya Agano Jipya, hususan Injili hadi leo. Kadiri ya imani hiyo, siku ya tatu baada ya kuuawa msalabani Ijumaa kuu, Yesu
  • Yesu kadiri ya mapokeo ya Ukristo na Uislamu, ingawa hatajwi katika Biblia isipokuwa katika kitabu cha karne ya 2 kinachoitwa Injili ya Yakobo na vingine
  • mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambaye alipendwa na mwalimu wao kuliko wenzake wote. Mapokeo ya Kikristo yanamuona kuwa mwandishi wa Injili ya Yohane, wa
  • anasifiwa na Barua ya Yakobo 2: 25 kama kielelezo cha mtu anayetenda mema. Rahabu kwa Kigiriki Ῥαχάβ, Rakhab anatajwa na Injili ya Mathayo 1: 5 katika
  • uliacha athari yake ya kudumu katika Kanisa hasa kupitia Injili ya Mathayo na Barua ya Yakobo Kati ya Wainjili, Luka hakuishia kuandika habari za Yesu tu
  • baada ya Injili nne. Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo
  • heshima ya mama wa Yesu. Mwenyewe anatajwa kwa kawaida kwa kutanguliza sifa yake mojawapo, hasa Bikira. Mapokeo ya karne ya 2 Injili ya Yakobo kuhusu
  • wa karne ya 1, alikuwa mmojawapo wa Mitume wa Yesu, maarufu kwa kuwa alimsaliti mwalimu wake apate vipande thelathini vya fedha Injili ya Mathayo 26: 14 - 16
  • vinalingana na vile vya Injili ya nne Injili ya Yohane Barua ya tatu na ya pili hazina mafundisho muhimu, tofauti na ile ya kwanza inayodai imani sahihi
  • Zawadi ya Mungu kwa Kigiriki Ματθαῖος, Matthaios alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa hasa kutokana na Injili yenye

Users also searched:

...
...
...