Back

ⓘ Kimelea ni kiumbehai ambaye anaishi ndani au juu ya kiumbehai mwingine wa spishi tofauti na kupata virutubishi kutokana na mwili wa kiumbe huyo, ambaye kwa kawa ..
Kimelea
                                     

ⓘ Kimelea

Kimelea ni kiumbehai ambaye anaishi ndani au juu ya kiumbehai mwingine wa spishi tofauti na kupata virutubishi kutokana na mwili wa kiumbe huyo, ambaye kwa kawaida ni mkubwa zaidi, bila kumpa kiumbe mwenyeji faida yoyote. Kinyume chake, mara nyingi analeta hasara au kusababisha ugonjwa.

Vimelea vingi ni vidogo sana vikiishi ndani ya wanyama au binadamu.

                                     

1. Aina za vimelea

Vimelea vingine ni vikubwa kiasi cha kuonekana kwa jicho:

 • chawa na viroboto vinavyokaa juu ya ngozi na kunyonya damu
 • minyoo inayoishi ndani ya utumbo kama mategu na nematodi nyingine

Vimelea vingine ni vidogo mno, vinaonekana kwa hadubini tu:

 • bakteria na protozoa nyingine, kwa mfano plasmodia zinazosababisha homa ya malaria
 • lava za minyoo kama schistosoma zinazosababisha kichocho baada ya kukua na kuwa minyoo wazima
                                     

2. Vimelea kati ya mimea na wanyama

Kuna pia wanyama wakubwa zaidi wanaotumia mbinu za kimelea kwa mfano ndege kama vile kekeo, fumbwe au kinili wanaotega mayai katika matego ya spishi nyingine.

Kuna mimea inayopata lishe kwa kutumia moja kwa moja majimaji ya mimea mingine na aina kadhaa kati ya hizi zinaendelea bila kutumia usanisinuru kabisa.

                                     

3. Vimelea na wenyeji wao

Vimelea mara nyingi hudhoofisha viumbehai wenyeji wao vinamoishi na vinaweza kusababisha magonjwa; kwa kawaida haviwaui mara moja, maana kimelea kinachomwua mwenyeji wake kitakosa mahali pa kuishi.

Vimelea vingi vinahitaji mazingira ya mwili wa spishi fulani vikiweza kuishi hapo tu.

                                     

4. Vimelea nje ya mwili wa mwenyeji

Vimelea hawa ni kama chawa, kunguni na kupe ambao huishi nje ya mwili wa mwenyeji ecto-parasites na hufyonya damu na kutaga mayai juu yake. Huenda wakasambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Wao hungojea mwenyeji aje karibu nao ambapo wanamnata na kuanza kumtegemea kwa lishe na pia kwa pahala pa kuzalisha.

                                     

5. Viungo vya nje

 • Toxoplasmosis
 • Parasitic and Parasitoid Alien Species in Science Fiction Movies
 • Parasitology Parasites Zoonoses - Polish/English over 50 movies Filmoteka and over 250 photos Fotogaleria/Photogallery with human and animal parasites.
 • Parasites World Archived Agosti 3, 2019 at the Wayback Machine. - Parasites articles and links.
 • VCU Virtual Parasite Project - Virtual Parasite Project at Virginia Commonwealth Universitys Center for the Study of Biological Complexity
 • KSU: Parasitology Research - parasitology articles and links.
 • Parasitism Archived Januari 18, 2012 at the Wayback Machine. - Knol
 • Aberystwyth University: Parasitology Archived Agosti 1, 2011 at the Wayback Machine. - class outline with links to full text articles on parasitism and parasitology.
 • Toxoplasma gondii in the Subarctic and Arctic
 • Division of Parasitic Diseases, Centers for Disease Control and Prevention
 • Medical Parasitology - online textbook.


                                     
 • zaidi kutegemea na kama kinga imesababishwa katika kimelea au ilihamishwa kimyakimya kutoka kwa kimelea mwenye kingamaradhi. Kinga tulivu inapatikana kwa
 • Maradhi ya Robles ni maradhi yasababishwayo na ambukizo la kinyoo wa kimelea Onchocerca volvulus. Dalili ni pamoja na mwasho mkali, manundu chini ya
 • Kuvu kiuawadudu ni kuvu inayokua kama kimelea ndani ya kiwiliwili cha mdudu na kumwua mwishowe. Nyingine ni vimelea vya faradhi nyingine ni vimelea vya
 • kwenye mashina ya miti. Ikiwa mti ni wa spishi sahihi, basi mbegu huota na kimelea hulowea mti huo. Inapendekezwa kutumia mlimbo maridadi kwa vimelea - nusu
 • unaoleta kuwaka kwa mishipa ya limfu. Asili yake ni mara nyingi minyoo kimelea aina ya filaria. Mifano mingi ya maradhi hayo hayana dalili. Angalau nyingine
 • katika mazingira bila kimelea hicho na kwa hivyo hawakuwa na kinga yoyote dhidi yake. Kimelewa cha msingi mahsusi cha kimelea hicho na njia ya uenezi
 • usingizi wa mang amung amu. Mkakati wa utambuzi ni pamoja na utafutaji wa kimelea unaobainika katika damu iliyoganda ama katika majimaji ya kivimbe cha kiowevu
 • kuu ya maambukizo ya matumbo huwa ni kwa sababu ya kvirusi, bakteria, kimelea au hali inayojulikana kama gastroenteritis. Maambukizo haya kwa kawaida
 • Ekinokokasi maradhi ya hiadatidi ni maradhi yenye kusababishwa na kimelea parasiti. Hiadatidi ni sisti za kiluwiluwi cha tegu Taaenia echinococcus
 • acridum inaambukiza panzi na nzige tu. Wanasayansi walitaka kujua kwa nini kimelea hiki ni mahususi kwa shabaha yake. Wanafikiri kwamba sababu ni ukosa wa
 • kipindupindu, magonjwa yanayotokana na chakula, ukoma na kifua kikuu. Kimelea kinachojulikana kwa kusababisha magonjwa kinaweza kujulikana baada ya miaka

Users also searched:

...
...
...