Back

ⓘ Iraq kwa Kiarabu العراق, al-ʿIrāq ni nchi ya Asia ya Magharibi inayokaliwa hasa na Waarabu 75-80% lakini pia na wengine, hasa Wakurdi 15%. Inajumlisha eneo la M ..
Iraq
                                     

ⓘ Iraq

Iraq kwa Kiarabu العراق, al-ʿIrāq ni nchi ya Asia ya Magharibi inayokaliwa hasa na Waarabu 75-80% lakini pia na wengine, hasa Wakurdi 15%).

Inajumlisha eneo la Mesopotamia pamoja na sehemu ya jangwa la Shamu na ya milima ya Zagros.

Imepakana na Kuwait, Saudia, Yordani, Syria, Uturuki na Uajemi. Kuna pwani fupi kwenye Ghuba ya Uajemi.

                                     

1. Jiografia

Sehemu kubwa ya Iraq ni jangwa lakini kuna eneo lenye rutuba kati ya mito ya Frati na Hidekeli.

Kaskazini ni hasa nchi ya milima inayopanda hadi ya kimo cha m 3.611 juu ya UB.

Hali ya hewa inalingana na mazingira. Kipindi cha kiangazi kuna joto kali. Majira ya Desemba-Februari kuna halijoto ya kupoa kusini na baridi kali mlimani.

                                     

2. Historia

Iraq ni nchi yenye historia ndefuː ilikuwa kitovu cha ustaarabu wa binadamu, mahali pa miji ya kwanza duniani katika Sumeri na Babeli.

Baada ya kusambaratika kwa milki ya Waturuki Waosmani walioitawala muda mrefu, Iraq ilikubaliwa kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mataifa mwaka 1932 ingawa hali halisi ilikuwa nchi lindwa chini ya athira ya Uingereza hadi mwaka 1958.

Miaka ya hivi karibuni imejulikana hasa kutokana na vita mbalimbaliː kwanza vita dhidi ya Uajemi chini ya serikali ya Saddam Hussein tangu 1981, baadaye vita dhidi ya Kuwait na Marekani.

Vita vya pili vya ghuba ya 2003 iliyoleta uvamizi wa Marekani ilizidi kuleta vifo na uharibifu.

Hatimaye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoingiliwa na DAESH iliyoteka sehemu kubwa ya nchi, hasa kaskazini na magharibi, hadi mwishoni mwa mwaka 2017.

                                     

3. Watu

Lugha rasmi na ya kwanza ni Kiarabu, ikifuatwa na Kikurdi ambayo pia imekuwa lugha rasmi, halafu lugha nyingine za jamii mbalimbali ambazo pengine zinatambulika kieneo.

Wakazi wengi 95%, hasa baada ya vita vya hivi karibuni, ni Waislamu, wakiwemo kwanza Washia halafu na Wasuni. Wakristo waliobaki ni 5%, wakiwemo hasa waamini wa Kanisa Katoliki la Wakaldayo na Waashuru wa Kanisa la Mashariki.

                                     

4. Uchumi

Iraq ina akiba kubwa za mafuta ya petroli ardhini. Mapato kutokana na mafuta yalileta maendeleo makubwa nchini hadi mwanzo wa kipindi cha vita vilivyoharibu sana nchi pamoja na uchumi wake.

                                     

5. Marejeo

 • By Desert Ways to Baghdad, by Louisa Jebb Mrs. Roland Wilkins With illustrations and a map, 1908 1909 ed. a searchable facsimile at the University of Georgia Libraries; DjVu & layered PDF format
 • Hanna Batatu, "The Old Social Classes and the Revolutionary Movements of Iraq", Princeton: Princeton University Press, 1978
 • Shadid, Anthony 2005. Night Draws Near. Henry Holt and Co., NY, U.S. ISBN 0-8050-7602-6
 • A Dweller in Mesopotamia, being the adventures of an official artist in the garden of Eden, by Donald Maxwell, 1921. a searchable facsimile at the University of Georgia Libraries; DjVu & layered PDF format
 • Charles Glass, "The Northern Front: A Wartime Diary" Saqi Books, London, 2004, ISBN 0-86356-770-3
 • Benjamin Busch, "Today is Better than Tomorrow. A Marine returns to a divided Iraq", Harpers Magazine, October 2014, pp. 29–44.
 • Iraqi Constitution. Ministry of Interior – General Directorate For Nationality 2006-01-30. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-11-28. Iliwekwa mnamo 18 February 2013.


                                     

6. Viungo vya nje

Serikali
 • Cabinet of Iraq
 • Presidency of Iraq
Taarifa za jumla
 • Iraq entry at The World Factbook
 • Iraq profile from the BBC News
 • Iraq katika Open Directory Project
                                     
 • Historia ya Iraq inahusu eneo ambalo leo linaunda Jamhuri ya Iraq Mesopotamia ina historia ndefuː ilikuwa kitovu cha ustaarabu wa binadamu, mahali pa
 • Baghdad Kar.: بغداد ni mji mkuu pia mji mkubwa nchini Iraq Iko kando la mto Tigris. Baghdad iliundwa na Waarabu badala ya mji mkuu wa kale Ktesiphon
 • Iraq Baada ya kuvuka milima ya Kurdistan inapita mji wa Mossul na kuingia katika tambarare ya Mesopotamia. Inafika Baghdad na kuendelea katika Iraq ya
 • Utajiri huo umesababisha pia vita kadhaa kama vile vita ya Iran - Iraq vita ya Iraq - Kuwait, vita ya ghuba. Eneo lote la ghuba ni 233, 000 km². Maji matamu
 • Uturuki unaingia katika tambarare ya jangwa la Shamu na kuendelea katika Iraq unapopita kwenye maghofu ya Babeli. Pamoja na Hidekeli Tigri ambao pia
 • kama zifuatazo: Armenia Bahrain Kupro Sinai rasi Misri Palestina Iran Iraq Israel Jordan Kuwait Lebanon Oman Pakistan Baluch pekee Qatar Saudia Syria
 • ad - Dawlah al - Islāmiyah fīl - ʿIrāq wash - Shām yaani Dola la Kiislamu katika Iraq na Shamu maarufu pia kama IS, na awali ISIL au ISIS kutokana na tafsiri
 • uliofuata Bush aliuamua kwa sababu zisizoeleweka vema kushambulia pia Iraq ingawa Iraq haikushiriki katika mashambulio ya 11 Septemba wala kuwa na uhusiano
 • watumwa wa Zanj nchini Iraq unakandamizwa na jeshi la khalifa wa Waabbasi Agosti - Ali bin Muhammad kiongozi wa watumwa wa Zanj katika Iraq aliyejitangaza kuwa
 • Kiazeri - Kusini ni lugha ya Kiturki nchini Azerbaijan, Uajemi, Uturuki, Iraq na Syria inayozungumzwa na Waazeri. Ni lugha tofauti na Kiazeri - Kaskazini ambayo

Users also searched:

passport application online tanzania,

...
...
...