Back

ⓘ Kikosi cha wapagazi kilikuwa kitengo cha jeshi la Uingereza wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kiliujumuisha wapagazi Waafrika walioajiriwa au kulazimishwa ..
Kikosi cha wapagazi
                                     

ⓘ Kikosi cha wapagazi

Kikosi cha wapagazi kilikuwa kitengo cha jeshi la Uingereza wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kiliujumuisha wapagazi Waafrika walioajiriwa au kulazimishwa kubeba mizigo ya jeshi la Uingereza kwenye mapigano ya Vita Kuu ya Kwanza katika Afrika ya Mashariki dhidi jeshi la Wajerumani lililoongozwa na Paul von Lettow-Vorbeck.

Waingereza walikuwa na tatizo kusafirisha chakula, risasi na mahitaji mengine kwa ajili ya jeshi kubwa katika maeneo pasipo barabara wala reli.

Jeshi la kikoloni la Uingereza lilitumia wanejeshi Waingereza, Wahindi na Wazungu wa Afrika Kusini hasa miaka ya kwanza ya vita. Wanajeshi hao walizoea kusafiri na kiwango cha mzigo wa binafsi.

Kinyume chake kamanda Mjerumani von Lettow-Vorbeck aliwahi kuandaa jeshi la askari Waafrika walioweza kutumia vyakula vilivyopatikana hata porini na wasiozoea kuwa na mizigo mingi. Hao askari wazalendo walikuwa sehemu kubwa ya jeshi la Schutztruppe la Wajerumani katika Afrika ya Mashariki. Kwa hiyo Wajerumani walitumia wapagazi wachache kuliko Waingereza ingawa hata wao waliajiri au kulazimisha Waafrika kufanya kazi hii kwa ajili ya mahitaji yao.

Upande wa Waingereza wanajeshi wao hawakuzoea vyakula vya mahali. Kwa hiyo kazi ya kusafirisha kilogramu 1 ya mchele kutoka bandari za pwani hadi kufikia wanajeshi barani ilihitaji mara nyingi kilogramu 50 za mchele zilizohitajika kulisha wapagazi waliobeba akiba.

Kwa kazi hii kubwa utawala wa kikoloni wa Waingereza ulianzisha kitengo cha pekee kilichoitwa "Carrier Corps". Ilitumia takriban wanaume 400.000 Waafrika kwa kazi zake, na katika muda wa vita kwa jumla Waafrika takriban milioni 1 walikuwa sehemu ya kikosi cha wapagazi upande wa Uingereza.

Imekadiriwa ya kwamba angalau 95.000 kati ya hao walikufa, wengi kutokana na njaa na magonjwa. Usimamizi wa kazi ya kujenga kikosi hiki kilikuwa chini ya Mwingereza Oscar Ferris Watkins aliyewahi kufika Afrika ya Mashariki ya Kiingereza yaani Kenya kama mtawala wa kikoloni mwenye cheo cha mkuu wa wilaya.

Kuna kumbukumbu ya wapagazi mahali mbalimbali kama vile

 • kwenye sanamu ya Askari huko Dar es Salaam Tanzania
 • kwenye makumbusho ya Vita Kuu huko Mbala jina la kikoloni lilikuwa Abercorn katika Zambia
 • kwenye makumbusho ya Vita Kuu huko Kenyatta Avenue, Nairobi.

Miji mingi ya Afrika Mashariki ina sehemu zinazoitwa kwa majina kama "Kariakoo" kama Dar es Salaam na Dodoma au "Kariakor" huko Nairobi. Ni mahali ambapo wapagazi waliostaafu katika kikosi cha wapagazi walijenga nyumba zao.

                                     

1. Tazama pia

 • History of Tanzania – First World War
 • en:East African Campaign World War I
 • en:Paul von Lettow-Vorbeck
 • en:Oscar Ferris Watkins
 • History of Kenya – Colonial History
                                     
 • corps yaani kikosi cha wapagazi waliobeba mizigo ya jeshi wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Pande zote vitani walitumia malakhi ya wapagazi waliokodishwa
 • alikadiria idadi ya waliokufa kati ya 100, 000 hadi 300, 000 hasa askari ya kikosi cha wapagazi na watu raia kutokana na njaa iliyosababishwa na vita. Paul von Lettow - Vorbeck
 • kilikuwa na kombania 3 zenye maafisa Wajerumani 13, maaskari Waafrika 320 na wapagazi 170 waliobeba mizinga mepesi na bunduki bombomu. Baada ya kuangamiza vijiji
 • kufyatua risasi. Kelele ziliposikika wapagazi wote wakakimbia. Punda waliokuwa wamebeba silaha wakaingia katika Kikosi Namba 5 ambapo askari wengi Wasudani
 • wapagazi wengi. Hivyo maendeleo yao yalikuwa polepole wakahitaji chakula kingi kulisha askari pamoja na wapagazi Askari pamoja na sehemu ya wapagazi

Users also searched:

...
...
...