Back

ⓘ Kazakhstan pia: Kazakistan ni nchi ambayo kwa kiasi kikubwa iko katika Asia ya Kati. Imepakana na Urusi, China, Kyrgyzstan, Uzbekistan na Turkmenistan. Mji mkuu ..
Kazakhstan
                                     

ⓘ Kazakhstan

Kazakhstan pia: Kazakistan ni nchi ambayo kwa kiasi kikubwa iko katika Asia ya Kati.

Imepakana na Urusi, China, Kyrgyzstan, Uzbekistan na Turkmenistan.

Mji mkuu ni Astana mwaka 2019 jina lake limekuwa Nursultan; Almaty ilishika nafasi hiyo hadi 1996.

                                     

1. Jiografia

Kazakhstan ina eneo la km² 2.717.300; ni nchi kubwa ya tisa duniani. Sehemu kubwa iko upande wa Asia na nyingine ndogo upande wa Ulaya.

Upande wa magharibi inaanza katika tambarare za mto Volga pamoja na Bahari ya Kaspi na kuelekea hadi milima ya Altai upande wa China. Kusini iko milima ya Tienshan yenye kimo cha mita 7.000 na ziwa Aral. Upande wa kaskazini hakuna mpaka asilia na Siberia.

                                     

2. Historia

Jina la nchi limetokana na Wakazakhi ambao ni taifa la watu wanaotumia Kikazakhi, mojawapo ya lugha za Kiturki.

Eneo liliwahi kuwa sehemu ya milki mbalimbali lakini tangu karne ya 15 Wakazakhi walijaribu kuungana mata kadhaa bila mafanikio ya kudumu.

Tangu karne ya 17 milki ya Urusi ilianza kuenea katika Asia ya Kati na hadi mwaka 1865 eneo lote la Kazakhstan lilitawaliwa na Urusi.

Baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917 Wakomunisti walichukua nafasi ya Matsar wa awali wakafanya nchi kuwa jamhuri yenye kiwango cha kujitawala ndani ya Jamhuri ya Kirusi ya Umoja wa Kisovyeti.

Mwaka 1936 nchi ilipewa cheo cha jamhuri kamili ndani ya Umoja wa Kisovyeti, ikijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikazakhi". Katika miaka iliyofuata Warusi na watu wa mataifa mengine ya Umoja huo walihamishwa nchini hadi Wakazakhi kubaki kuwa chini ya nusu ya wakazi wote.

Miaka 1990/1991 wakati wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti jamhuri ilijiondoa polepole. Kiongozi wa chama cha kikomunisti cha Kazakhstan Nursultan Nasarbajew alitangaza uhuru na kuwa rais wa kwanza akiendelea kutawala hadi mwaka 2019.

                                     

3. Wakazi

Wakazi wengi 65.5% ni Wakazakhi wanaozungumza Kikazakhi, lugha ya jamii ya Kituruki, wakifuatwa na Warusi wanaozungumza lugha yao ya jamii ya Kislavoni 21.5%. Ya kwanza ndiyo lugha ya taifa, ya pili ni pia lugha rasmi. Kuna makabila mengine 30, kama vile Wauzbeki 3.0%, Waukraina 1.8% n.k.

Upande wa dini, 70.2% ni Waislamu hasa Wasuni na 26.3% Wakristo. Baada ya uhuru, dini zote zimepata uhai mpya na kujenga maabadi mengi. Serikali haina dini, lakini inaziheshimu zote.

                                     

4. Viungo vya nje

 • Caspian Pipeline Controversy from the Dean Peter Krogh Foreign Affairs Digital Archives
 • The Region Initiative TRI
 • Kazakhstan at 20 years of independence, The Economist, Dec 17th 2011
 • Kazakhstan information from the United States Department of State
 • Portals to the World from the United States Library of Congress.
 • Kazakhstan Archived Machi 4, 2016 at the Wayback Machine. at UCB Libraries GovPubs.
 • Ministry of Foreign Affairs of the Republic of Kazakhstan Archived Septemba 29, 2011 at the Wayback Machine.
 • Kazakhstan katika Open Directory Project
 • Key Development Forecasts for Kazakhstan from International Futures.
 • "Blowing the lid off" – Unrest in Kazakhstan, The Economist, Dec 20th 2011
 • Kazakhstan Internet Encyclopedia
 • Kazakhstan entry at The World Factbook
 • Country Profile from BBC News.
 • World Bank Data & Statistics for Kazakhstan Archived Septemba 29, 2011 at the Wayback Machine.
 • 2008 Human Rights Report: Kazakhstan. Department of State; Bureau of Democracy, Human Rights and Labor
 • Country Facts from Kazakhstan Discovery
 • Wikimedia Atlas of Kazakhstan


                                     

4.1. Viungo vya nje Serikali

 • Ministry of Foreign Affairs of the Republic of Kazakhstan Archived Septemba 29, 2011 at the Wayback Machine.
 • Tovuti rasmi
 • E-Government of the Republic of Kazakhstan
 • Chief of State and Cabinet Members
                                     

4.2. Viungo vya nje Biashara

 • World Bank Summary Trade Statistics Kazakhstan

Majiranukta kwenye ramani: 48°N 68°E

                                     
 • Tajikistan na magharibi ya China Kikazakhi wasemaji milioni 11 nchini Kazakhstan Uzbekistan, China, Urusi Kiuiguri wasemaji milioni 8 hasa katika Shinjiang
 • dunia vikundi vimebaki hasa katika Hungaria, Romania, Uceki, Urusi na Kazakhstan Vikundi vidogo vya watu waliohamia katika karne za 19 na 20 wanaoendelea
 • duniani. Liko katika Asia ya Kati, mashariki mwa Kazakhstan ndani ya beseni linaloshirikiwa na Kazakhstan na China, pamoja na sehemu ndogo ya Kirgizia. Beseni
 • UA au ua ni kifupi cha: Kodi ya IATA ya United Airlines, USA Kodi ya ICAO ya Kazakhstan Kyrgyzstan Kodi ya ISO 3166 - 1 ya nchi ya Ukraini
 • la km² 371, 000 na mjao wa km³ 78, 200. Liko kati ya Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan Turkmenistan na Uajemi. Kimo chake kinafikia mita 1, 025. Huitwa bahari
 • ya chromi huchimbwa hasa Afrika Kusini 50 ya mahitaji yote ya dunia halafu Kazakhstan 15, 2  Uhindi 12, 1  Zimbabwe 3, 7  na Ufini 3 
 • inaungana. Unaendelea kupita kwa km 2, 212 katika Tajikistan, Uzbekistan na Kazakhstan hadi kuishia katika Ziwa Aral. Pamoja na Amu Darya ni mmoja kati ya mito

Users also searched:

...
...
...