Back

ⓘ Kichaa cha mbwa ni ugonjwa hatari unaoathiri ubongo na kwa kawaida unamwua aliyeambukizwa nao. Inatokana na ambukizo la virusi vinavyosababisha uvimbe wa ubongo ..
Kichaa cha mbwa
                                     

ⓘ Kichaa cha mbwa

Kichaa cha mbwa ni ugonjwa hatari unaoathiri ubongo na kwa kawaida unamwua aliyeambukizwa nao.

Inatokana na ambukizo la virusi vinavyosababisha uvimbe wa ubongo encephalytis. Virusi hivi vinaweza kutokea kwa binadamu na wanyama wa aina za mamalia na ndege lakini ni mara chache kati ya wanyama wala majani. Mnyama mgugunaji ni nadra sana kuambukizwa na kichaa cha mbwa.

                                     

1. Jina na njia za kuambukizwa

Jina la ugonjwa linatokana na hali ya mbwa wanaoambukizwa na kuwa hatari kwa binadamu kutokana na maisha ya karibu naye. Asilimia 99 za watu huambukizwa na mbwa. Lakini inatokea pia mara kwa mara kwa paka, mbweha, mbwa mwitu na wanyama wala nyama wengine, pia aina za popo, hasa huko Amerika. Habari za maambukizo kutoka mtu mgonjwa kwenda mtu mwingine ni chache sana.

Njia za maambukizo ni mate na damu kwa hiyo hasa kwa njia ya kungatwa na mnyama mgonjwa. Mate kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa anaweza pia kusambaza kichaa cha mbwa kama mate inakuja kukutana na utando telezi wa mnyama mwingine au binadamu.

                                     

2. Dalili za ugonjwa

Ugonjwa huo inaweza tu kukutwa baada ya kuanza kwa dalili. Zile za kwanza za kuambukizwa ni pamoja na homa na kuhisi mchonyoto katika eneo la mwili ambako mtu alingatwa.

Dalili hizi zinafuatwa na nyingine:

  • kupoteza fahamu.
  • kukosa uwezo wa kutawala mwendo wa viungo vya mwili
  • miendo kali ya mwili,
  • kukasirika au kuogopa sana kwa ghafla,
  • hofu ya maji,

Mara dalili hizi zinapoonekana maana yake ugonjwa umeshaanza kuharibu ubongo na neva na mgonjwa hawezi kupona tena. Kifo kinafuata.

Muda kati ya kuambukizwa ugonjwa na mwanzo wa dalili ni kawaida mwezi mmoja hadi miezi mitatu. Hata hivyo, kipindi hiki kinaweza kutofautiana kutoka chini ya wiki moja hata zaidi ya mwaka mmoja. Muda unategemea umbali, kwa sababu virusi lazima kusafiri kufikia mfumo mkuu wa neva kwa kufuata mishipa ya pembeni.

                                     

3. Tiba na kinga

Watu wanaotibiwa mara moja baada ya kuambukizwa wanaweza kupona. Lakini tiba inahitaji kutekelezwa kabla virusi havijafikia ubongo, kwa hiyo katika muda wa saa za kwanza baada ya kungatwa. Wanyama wa kaya wanapewa chanjo dhidi ya ugonjwa huu katika nchi nyingi.

Kudhibiti wanyama na mipango ya chanjo vimepungua hatari ya kichaa cha mbwa kutoka mbwa katika nchi kadhaa. Kuchanja watu kulipendekeza kwa wale walio katika hatari kubwa. Kundi hatarishi pamoja na watu wanaofanya kazi na popo au ambao hutumia muda mrefu katika maeneo ya dunia ambapo kichaa cha mbwa ni ya kawaida. Katika watu hao chanjo ya kichaa cha mbwa na wakati mwingine kichaa cha mbwa immunoglobulini ina ufanisi katika kuzuia ugonjwa kama mtu anapata matibabu kabla ya kuanza kwa dalili za kichaa cha mbwa.

Kuosha palipoumwa na mchukubo kwa dakika 15 kwa maji na sabuni, povidoni iodini, au sabuni vinaweza kuua virusi pia na kuwa na ufanisi fulani katika kuzuia maambukizi ya kichaa cha mbwa. Ni watu wachache walionusurika maambukizi ya kichaa cha mbwa na hii ilikuwa kwa matibabu ya kina, inayojulikana kama ifataki ya Milwaukee.                                     

4. Uenezi

Kichaa cha mbwa husababisha vifo vya watu wapatao 26.000 hadi 55.000 duniani kote kwa mwaka. Zaidi ya 95% ya vifo hivi hutokea katika Asia na Afrika. Kichaa cha mbwa kipo sasa katika nchi zaidi ya 150 na katika mabara yote ila Antaktika. Zaidi ya watu bilioni 3 huishi katika nchi ambapo kichaa cha mbwa hutokea.

                                     
  • kugundua njia za kuongeza kinga cha mwili dhidi ya magonjwa kwa njia ya chanjo, akagundua chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa na kimeta. Aligundua pia mbinu
  • binadamu mfano: kichaa cha mbwa kinapitishwa pale ambako virusi vyake vinaingia mwilini mwa binadamu, kwa kawaida mtu aking atwa na mbwa mgonjwa kupitia
  • Cushing hazipatikani kwa binadamu pekee na bali pia ni hali ya kawaida katika mbwa na farasi waliofugwa. Dalili ni pamoja na kuongeza uzito haraka, hasa wa

Users also searched:

...
...
...