Back

ⓘ Karamu ya mwisho inamaanisha mlo wa mwisho wa Yesu Kristo hapa duniani, ambao aliula pamoja na mitume wake kabla hajakamatwa na hatimaye kusulubiwa. Katika Inji ..
Karamu ya mwisho
                                     

ⓘ Karamu ya mwisho

Karamu ya mwisho inamaanisha mlo wa mwisho wa Yesu Kristo hapa duniani, ambao aliula pamoja na mitume wake kabla hajakamatwa na hatimaye kusulubiwa.

Katika Injili, hasa ile ya Luka, Yesu alishiriki mara nyingi karamu alizoandaliwa au alipoalikwa, kama vile ile ya arusi ya Kana. Ingawa jambo hilo lilisababisha aitwe "mlafi na mlevi", kwake ilikuwa nafasi ya kuzidi kujitambulisha kwa matendo na maneno na ya kutoa mafundisho yake.

Habari za karamu ya mwisho zinasimuliwa kirefu zaidi, hasa kwa sababu ndiyo wakati wa Yesu kuweka ukumbusho wake wa kudumu katika sakramenti ya mwili na damu yake.

Wakristo wanafanya ukumbusho huo mara nyingi, lakini hasa Alhamisi Kuu.

Barua ya kwanza kwa Wakorintho ndiyo ushahidi wa zamani zaidi kuhusu ibada hiyo. Baada yake Injili Ndugu pia ziliripoti matendo na maneno ya Yesu juu ya mkate na divai.

Injili ya Yohane haisimulii ekaristi ilivyowekwa, ila katika sura ya 6 inaripoti maneno mazito ya Yesu kuhusu mkate wa uzima, halafu katika karamu ya mwisho, pamoja na mengine, inaeleza Yesu alivyowaosha miguu Mitume na kuwaachia amri mpya ya kupendana kama yeye alivyowapenda, ambayo ndiyo lengo la ekaristi.

                                     

1. Marejeo

 • Linders, Barnabas The Gospel of John Marshall Morgan and Scott 1972
 • Kilgallen, John J. A Brief Commentary on the Gospel of Mark Paulist Press 1989 ISBN 0-8091-3059-9
 • Bultmann, Rudolf The Gospel of John Blackwell 1971
 • Brown, Raymond E. et al. The New Jerome Biblical Commentary Prentice Hall 1990 ISBN 0-13-614934-0
 • Brown, Raymond E. An Introduction to the New Testament Doubleday 1997 ISBN 0-385-24767-2
                                     
 • zakatul - fitri زكاة الفطر na kuswali, baadaye hukutana kwenye karamu Neno Ramadhani linatokana na mizizi ya Kiarabu ramida au ar - ramad, ambayo inamaanisha joto
 • hekalu Hata hivyo kwa namna ya pekee jina hilo linatumika kwa Mwana wa Daudi, mtawala wa Israeli katika wakati wa mwisho ambao utakuwa wa amani duniani
 • makaburi ya Mitume, ambapo anabadilishana nguo na fukara na kuanza kuombaomba. Katikati ya mwaka uongofu wake ulikuwa umekomaa: katika karamu ya mwisho aliyowaandalia
 • wafuasi wake kutumikia, Petro aliagizwa kuandaa pamoja na Yohane karamu ya mwisho ya Yesu na mitume wake kwenye Pasaka, ambapo ilimbidi akubali kuoshwa
 • maisha ya watu yalivyokuwa katika mazingira yake. Hata hivyo wataalamu wanaonyesha kwamba ujumbe wa dhati umefichika hasa katika sehemu ya mwisho ya habari
 • wa karamu ya mwisho Mkate bapa wa Uturuki uliochachuka Mkate wa Kiingereza Kuandaa mkate bapa Mikate midogo Ganda la mkate Mkate dukani Mikate ya fimbo
 • ya wachoraji bora wa historia yote. Amefanya michoro mingi sana. Miongoni mwa picha zake, mbili zilizo maarufu zaidi duniani ni Mona Lisa na Karamu ya
 • Jumamosi Kuu Siku ya Alhamisi Kuu inafanyika ibada ya kumbukumbu ya Yesu kufanya karamu ya mwisho na kuwaosha mitume wake miguu. Baada ya Kwaresima kwisha
 • mwili. Sakramenti mbili za mwisho ni za kuhudumia ushirika katika Kanisa na katika familia iliyo kanisa dogo. Katika karne ya 20, hasa katika Mtaguso wa
 • enzi cha Daudi, baba yake. 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho 34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno
 • yaani tangu Yesu alipozaliwa hadi mwisho wa maisha ya mitume wake, nchi hiyo haikuwa huru, bali chini ya himaya ya Warumi, ingawa pengine hao waliwakabidhi

Users also searched:

...
...
...