Back

ⓘ Karolo wa Sezze, alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Wareformati aliyeandika vizuri sana kuhusu maisha ya kiroho. Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mta ..
Karolo wa Sezze
                                     

ⓘ Karolo wa Sezze

Karolo wa Sezze, alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Wareformati aliyeandika vizuri sana kuhusu maisha ya kiroho.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Alitangazwa kwanza mwenye heri na Papa Leo XIII mwaka 1882, halafu mtakatifu na Papa Yohane XXIII tarehe 12 Aprili 1959.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake, 6 Januari, au kesho yake.

                                     

1. Maisha

Jina la kuzaliwa lilikuwa Giancarlo Marchioni. Alipokuwa kijana alitamani kwenda India kama mmisionari.

Kisha kuvutwa na maisha ya watakatifu mabradha Wafransisko Paskali Baylon na Salvador wa Horta, aliamua kujiunga na shirika lao, alipokubaliwa mwaka 1635.

Baadaye alieleza kuwa alifanya hivyo ili kuishi kifukara na kuombaomba "kwa upendo wa Kristo".

Karolo aliishi katika jumuia mbalimbali kama bradha, asiombe kamwe upadrisho: alikuwa mpishi, bawabu, mtunzasakristia, mtunzabustani na ombaomba. Kwa kukosa ufundi katika kazi hizo zote, alijulikana kwa sababu ya kuuunguza jiko zima.

Akiwa bawabu, siku moja alikatazwa na mlinzi wa jumuia asitoe chakula kwa wasio watawa. Karolo alitii, lakini mara moja misaada iliyotolewa kwa jumuia ilipungua sana. Hapo alimsaidia mlinzi kutambua uhusiano kati ya mambo hayo mawili. Aliporuhusiwa tena kusaidia maskini, misaada kwa jumuia iliongezeka tena.

Ingawa hakuwa padri, Karolo aliagizwa na muungamishi wake kuandika habari za maisha yake. Ndivyo kilivyopatikana kitabu Makuu ya Rehema za Mungu ambacho kilienea na kusomwa sana.

Vilevile alipaswa kutoa mashauri ya kiroho kwa watu mbalimbali akaandika vitabu vya namna hiyo. Papa Klementi IX alipokuwa mahututi alimuita ili kupata faraja na baraka yake.

                                     
  • Mtakatifu Karolo wa Sezze bradha wa shirika la Ndugu Wadogo kutoka Italia 1919 - Theodore Roosevelt, Rais wa Marekani, na mshindi wa Tuzo ya Nobel
  • Baada ya Kristo 29 Aprili - Uchaguzi wa Papa Klementi X 6 Januari - Mtakatifu Karolo wa Sezze bradha wa shirika la Ndugu Wadogo kutoka Italia Desemba
  • Oktoba - Mtakatifu Karolo wa Sezze bradha wa shirika la Ndugu Wadogo kutoka Italia bila tarehe Bartholomeus van der Helst, mchoraji wa Uholanzi 6 Desemba
  • 73. 1613 - Mtakatifu Karolo wa Sezze bradha wa shirika la Ndugu Wadogo kutoka Italia 1669 - Mtakatifu Anjelo wa Acri, padri wa shirika la Ndugu Wadogo
  • 1637 26 Novemba Yosefu wa Copertino, padri 1663 18 Septemba Bernardo wa Corleone 1667 12 Januari Karolo wa Sezze 1670 6 Januari Yohane Wall
  • 1589 mtoto wa watumwa huko Italia, Mnegro wa kwanza kutangazwa mtakatifu, Umile wa Bisignano 1637 mnyenyekevu ajabu, na Karolo wa Sezze 1670 aliyeandika

Users also searched:

...