Back

ⓘ Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar ni mojawapo kati ya madhehebu ya Ukristo wa mashariki yenye ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote. Linafuata map ..
Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar
                                     

ⓘ Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar

Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar ni mojawapo kati ya madhehebu ya Ukristo wa mashariki yenye ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote.

Linafuata mapokeo ya Mesopotamia na kutumia liturujia ya Mesopotamia, lakini linapatikana hasa India na katika nchi mbalimbali ambapo waamini wake wamehamia, kama vile Marekani, ambako lina majimbo mawili, na Kanada, Australia na Britania ambako kuna jimbo mojamoja.

Kwa jumla lina waumini milioni 4-5, wakiongozwa na askofu mkuu kabisa wa Ernakulam-Angamaly na maaskofu wengine 56, mapadri 9.121 katika parokia 3.224.

Kanisa hilo ndiyo madhehebu kubwa kuliko yale yote yanayosisitiza kuwa yametokana na kazi ya Mtume Thoma.

Kati ya waamini wake, sista Mfransisko Alfonsa Matathupadathu alitangazwa mtakatifu na Papa Benedikto XVI tarehe 12 Oktoba 2008. Baada yake wametangazwa watakatifu wengine wawili: padri Kuriakose Elias Chavara na sista Eufrasia Eluvathingal.

Kwa sasa Kanisa hilo lina masista 35.000 hivi na mabruda 6.836.

Kanisa hilo lina kalenda maalumu kwa mwaka wa liturujia inayofuata mwendo wa historia ya wokovu na kiini chake kikiwa maisha ya Yesu. Majira ya pekee ni tisa:

 • Majira ya joto Qaita
 • Mitume Slihe
 • Epifania Denha
 • Ufufuko Qyamta
 • Eliya-Msalaba-Mose Elijah-Sliba-Muse
 • Mfungo Mkuu Sawma Rabba
 • Kutabarukiwa kwa Kanisa Qudas-Edta
 • Kupashwa habari Suvara
 • Kuzaliwa kwa Yesu
                                     

1. Viungo vya nje

 • The website for Synod of Diamper
 • Orientale Lumen - Hati ya Papa Yohane Paulo II kuhusu Makanisa ya Mashariki
 • Archdiocese of Kottayam
 • Syro Malabar Church in Australia
 • Syro malabar mission in Chennai Archived Novemba 28, 2020 at the Wayback Machine.
 • Nazraney Heritage
 • Hati Orientales omnes Ecclesias ya Papa Pius XII
 • Sura ya Idara ya Papa kwa Makanisa hayo
 • Indian Christianity: Books by Geddes, Mackenzie, Medlycott, &c.
 • Codex Canonum Ecclesiarum Orientalium - Mkusanyo wa Sheria za Makanisa ya Mashariki katika Kilatini pamoja na sehemu sambamba
 • Instruction for Applying the Liturgical Prescriptions of the Code of Canons of the Eastern Churches Archived Aprili 25, 2009 at the Wayback Machine. - Hati ya Idara ya Papa kwa Makanisa ya Mashariki kuhusu liturujia
 • CNEWA Idara ya Papa inayosaidia Makanisa hayo
 • Archdiocese of Ernakulam-Angamaly
 • Archdiocese of Changanacherry
 • Ujuzi wa msingi kuhusu Makanisa hayo
 • Syro Malabar Church in Qatar Archived Julai 8, 2020 at the Wayback Machine.
 • Syro Malabar Matrimony
 • Syro-Malabar Church
 • Takwimu za Makanisa hayo
 • Archdiocese of Thrissur
 • Hati Orientalium Ecclesiarum ya Mtaguso wa pili wa Vatikano
 • Archdiocese of Tellicherry
                                     
 • makubwa zaidi ni: Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraina Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar Kanisa la Wamaroni Kanisa Katoliki la Kigiriki la Wamelkiti Katika
 • Agosti 1910 - 28 Julai 1946 alikuwa mtawa Mfransisko wa Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar nchini India. Alitangazwa mwenye heri na Papa Yohane Paulo
 • katika harusi ya Wahindu Wanaharusi kutiwa taji katika Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar India Wanaharusi huko Japani Wanaharusi huko Armenia Wanaharusi

Users also searched:

...