Back

ⓘ Kanisa Katoliki la Kimelkiti ni mojawapo kati ya madhehebu ya Kanisa Katoliki yanayoongozwa na Patriarki wake akisaidiwa na sinodi yake na akiwa na ushirika kam ..
Kanisa Katoliki la Kimelkiti
                                     

ⓘ Kanisa Katoliki la Kimelkiti

Kanisa Katoliki la Kimelkiti ni mojawapo kati ya madhehebu ya Kanisa Katoliki yanayoongozwa na Patriarki wake akisaidiwa na sinodi yake na akiwa na ushirika kamili na Papa wa Roma tangu mwaka 1729.

Makao makuu yako Damasko, Siria, lakini Patriarki anatumia jina la Antiokia na mashariki yote, Aleksandria na Yerusalemu.

Kwa sasa tangu tarehe 21 Juni 2017 Patriarki ni Youssef Absi, S.M.S.P., anayetokea Damasko.

Kwa asili waamini wake wengi milioni 1.6 wanazungumza Kiarabu, lugha rasmi ya Kanisa hilo, ingawa hasa siku hizi wana mchanganyiko mkubwa wa damu.

                                     

1. Asili ya jina

Melkiti ni neno linalotokana na malkā, yaani mfalme kwa Kiaramu, na awali lilimaanisha Wakristo wa Mashariki ya Kati waliokubali maamuzi ya Mtaguso wa Kalsedonia 451 uliokuwa unaungwa mkono na kaisari wa Konstantinopoli. Jina hilo linaendelea kutumiwa na Wakatoliki tu.

Pamoja na kwamba kwa asili Wakristo hao walikuwa wanafuata mapokeo ya Antiokia, au pengine wa Aleksandria au wa Yerusalemu, walikuja kupokea liturujia ya Ugiriki kama Waorthodoksi wengine, wakati waliokataa mtaguso huo waliendelea na liturujia zao.

                                     

2. Uenezi

Katika nchi za Kiarabu, Kanisa hilo lina majimbo kama ifuatavyo:

 • Misri na Sudan
 • Jimbo la Kipatriarki la Aleksandria, likisimamiwa na protosyncellus.
 • Israel
 • Jimbo la Kimelkiti la Akka
 • Jimbo kuu la Petra, Philadelphia Amman na Transjordan yote
 • Jordan
 • Jimbo kuu la Tripoli
 • Jimbo kuu la Baalbek
 • Jimbo kuu la Saida na Deir el-Kamar
 • Jimbo kuu la Forzol, na Zahlé na Bekaa yote
 • Jimbo kuu la Tyre
 • Jimbo kuu la Baniyas na Marjeyoun
 • Jimbo kuu la Kimelkiti la Beirut na Byblos
 • Lebanon
 • Jimbo kuu la Kimelkiti la Yerusalemu
 • Palestina
 • Syria
 • Jimbo kuu la Homs, Hama na Yabroud
 • Jimbo kuu la Latakia na Bonde la WAkristo
 • Jimbo la Kipatriarki la Antiokia, likiwa na makao Damasko
 • Jimbo kuu la Aleppo
 • Jimbo kuu la Bosra na Hauran Jimbo kuu la Khabab

Katika nchi nyingine duniani, Kanisa lina majimbo kama ifuatavyo:

 • Esarkia ya Kitume ya Argentina
 • Argentina
 • Jimbo la Mt. Mikaeli la Sydney
 • Australia na New Zealand
 • Brazil
 • Jimbo la Kimelkiti la Nossa Senhora do Paraíso em São Paulo.
 • Jimbo la Saint-Sauveur de Montréal.
 • Canada
 • Jimbo la Nuestra Señora del Paraíso en México.
 • Mexiko
 • Marekani
 • Jimbo la Kimelkiti la Newton
 • Venezuela
 • Esarkia ya Kitume ya Venezuela, Caracas.
                                     

3. Marejeo

 • Parry, Ken; David Melling editors 1999. The Blackwell Dictionary of Eastern Christianity. Malden, Massachusetts.: Blackwell Publishing. ISBN 0-631-23203-6.
 • Descy, Serge 1993. The Melkite Church. Boston: Sophia Press.
 • Zoghby, Elias 1998. Ecumenical Reflections. Fairfax, Virginia.: Eastern Christian Publications. ISBN 1-892278-06-5.
 • Faulk, Edward 2007. 101 Questions and Answers on Eastern Catholic Churches. New York: Paulist Press. ISBN 978-0-8091-4441-9.
 • Roccasalvo, Joan L. 1992. The Eastern Catholic Churches: An Introduction To Their Worship and Spirituality. Collegeville, Minnesota.: The Liturgical Press. ISBN 0-8146-2047-7.
 • Raya, Joseph 1992. Byzantine Church and Culture. Allentown, New Jersey: Alleluia Press. ISBN 0-911726-54-3.
 • Tawil, Joseph 2001. The Patriarchate of Antioch Throughout History: An Introduction. Boston: Sophia Press.
 • Dick, Ignatios 2004. Melkites: Greek Orthodox and Greek Catholics of the Patriarchates of Antioch, Alexandria and Jerusalem. Boston: Sophia Press.


                                     

4. Viungo vya nje

 • Hati Orientalium Ecclesiarum ya Mtaguso wa pili wa Vatikano
 • Orientale Lumen - Hati ya Papa Yohane Paulo II kuhusu Makanisa ya Mashariki
 • LÉglise Melkite/The Melkite Church Archived Oktoba 13, 2008 at the Wayback Machine.
 • Codex Canonum Ecclesiarum Orientalium - Mkusanyo wa Sheria za Makanisa ya Mashariki katika Kilatini pamoja na sehemu sambamba
 • Eparchy of Newton, the Melkite Church in the US
 • Ujuzi wa msingi kuhusu Makanisa hayo
 • Melkite Catholic Web Ring Archived Septemba 27, 2008 at the Wayback Machine.
 • Takwimu za Makanisa hayo
 • Instruction for Applying the Liturgical Prescriptions of the Code of Canons of the Eastern Churches Archived Aprili 25, 2009 at the Wayback Machine. - Hati ya Idara ya Papa kwa Makanisa ya Mashariki kuhusu liturujia
 • Melkite Greek Catholic Patriarchate of Antioch, Alexandria and Jerusalem Archived Oktoba 8, 2008 at the Wayback Machine.
 • Extensive history of the Melkite Church
 • CNEWA Idara ya Papa inayosaidia Makanisa hayo
 • Hati Orientales omnes Ecclesias ya Papa Pius XII
 • Sura ya Idara ya Papa kwa Makanisa hayo
 • Article on the Melkite Catholic Church by Ronald Roberson on the CNEWA website.
 • Melkite Ambassadors Young Adult Website Archived Septemba 27, 2007 at the Wayback Machine.
                                     
 • mfano Misri kuna Kanisa Katoliki la Wakopti, Kanisa Katoliki la Kimelkiti Kanisa Katoliki la Armenia, Kanisa Katoliki la Wakaldayo na la Kilatini. Mapadri
 • Uturuki waamini 6, 025. Kanisa Katoliki la Kigiriki la Masedonia Macedonia waamini 14, 937. Kanisa Katoliki la Kigiriki la Kimelkiti Siria, Lebanon, Israel
 • Israeli, 26 Agosti 1878 alikuwa mmonaki wa Kanisa Katoliki la Kimelkiti katika shirika la Wakarmeli Peku.. Baada ya kufiwa wazazi alihamia Aleksandria
 • Divine Kanisa Katoliki la Kimelkiti The Divine Liturgy of the Melkite Greek Catholic Church Archived Februari 5, 2012 at the Wayback Machine. Kanisa Katoliki
 • Mukasa Kiriwawanvu Mariam Baouardy, bikira wa Wakarmeli Peku, Kanisa Katoliki la Kimelkiti 1854 - 1859, Misri Onesimo Nesib, mmisionari Mlutheri wa Waoromo

Users also searched:

...