Back

ⓘ Kiiraqw ni mojawapo kati ya lugha za Kiafrika-Kiasia. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiiraqw iko katika kundi la lugha za Kikushi. Inatumika ..
Kiiraqw
                                     

ⓘ Kiiraqw

Kiiraqw ni mojawapo kati ya lugha za Kiafrika-Kiasia. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiiraqw iko katika kundi la lugha za Kikushi.

Inatumika nchini Tanzania na kuzungumzwa hasa na kabila la Wairaqw kaskazini mwa Tanzania kutokana na kuwepo kwao katika mkoa wa Manyara na mkoa wa Arusha kama wenyeji wa karne nyingi.

Baadhi ya watu husema Kiiraqw ni sawa na "Kimbulu", kumbe siyo. Hakuna lugha inayoitwa Kimbulu. Mbulu ni jina la wilaya ambayo ina idadi kubwa ya Wairaqw kuliko eneo lingine lolote nchini Tanzania. Lakini ikumbukwe kuwa Mbulu si eneo pekee wanakopatikana Wairaqw, kitu ambacho kingesababisha watu wengine kuita lugha ya Kiiraqw kuwa Kimbulu.

Mwaka 2001 idadi ya wasemaji wa Kiiraqw ilihesabiwa kuwa watu 462.000. Kwa sasa wanakadiriwa kuwa milioni 1 hivi.

                                     

1. Marejeo

 • Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. Orientalia et africana gothoburgensia, no 17. Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346

Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:

 • Desdery Sulle; 2014 Short research on Kiiraq; as a Cushitic Language speaker.
 • Mous, Maarten. 1993. A grammar of Iraqw. Cushitic language studies/ Kuschitische Sprachstudien, vol 9. Hamburg: Helmut Buske Verlag. Kurasa xvi, 361.
 • Maghway, Josephat B. 1995. Annotated Iraqw lexicon. African language study series, vol 2. Tokyo: Institute for the Study of Languages and Cultures of Asia and Africa ILCAA, Tokyo University of Foreign Studies. Kurasa 210.
                                     

2. Viungo vya nje

 • Archived Oktoba 4, 2006 at the Wayback Machine.
 • makala za OLAC kuhusu Kiiraqw
 • lugha ya Kiiraqw katika Glottolog
 • Lugha ya Kiiraqw kwenye Multitree
                                     
 • mkoa wa Manyara na mkoa wa Arusha kusini kwa Ngorongoro. Lugha yao ni Kiiraqw jamii ya lugha za Kikushi za kusini. Mwaka 2001 walikuwa 462, 000 hivi
 • ya lugha za Kiafrika - Kiasia, si ya Kibantu, kwani huendana na Kifyomi, Kiiraqw na Kiburunge ambazo zote hizi ni lugha za Kikushi. Kabila hili sehemu zote
 • wazazi wao waliowakuta. Lugha hii si ya Kibantu, kwani huendana na Kifiomi, Kiiraqw na Kiburunge. Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kialagwa imehesabiwa kuwa
 • Kihangaza Kihaya Kihehe Kiikizu - Sizaki Kiikoma - Nata - Isenye Kiingereza Kiiraqw Kiisanzu Kijita Kikabwa Kikachchi Kikagulu Kikahe Kikami Kikara Kikerewe

Users also searched:

...
...
...