Back

ⓘ Joto kutoka ardhi, pia joto ardhi ni chanzo cha nishati kinachotumia joto lililopo chini ya uso wa dunia. ..
Joto kutoka ardhi
                                     

ⓘ Joto kutoka ardhi

Joto kutoka ardhi, pia joto ardhi ni chanzo cha nishati kinachotumia joto lililopo chini ya uso wa dunia.

                                     

1. Joto ndani ya dunia

Kiini cha dunia ni ya moto sana kinafikia maelfu ya sentigredi. Kwa jumla joto kubwa la ndani linapungua hadi uso wa dunia lakini kuna mahali ambako njia za magma mwamba ya moto ulioyeyuka zinafika karibu na uso wa dunia. Kama njia za magma zinafika usoni wa dunia moja kwa moja tunaona volkeno. Lakini mara nyingi zaidi kuna mahali ambako maji chini ya ardhi yanagusana na miamba ya moto iliyopo mita mamia chini ya ardhi.

                                     

2. Matumizi ya joto ndani ya ardhi

Tangu siku za kale watu walijua mahali kadhaa ambako maji ya moto yanatoka kwenye ardhi kama chemchemi. Kama chemchemi hizi za moto zilikuwa karibu na makazi ya watu zilitumiwa kwa kuogelea au hata kupasha moto nyumba kwenye mazigira baridi.

Lakini siku za nyuma watu waligundua mbinu kulitumia joto kutoka ardhi kwa kuzalisha umeme. Mwaka 2007 takriban gigawati 10 za umeme zilipatikana kutokana na matumizi ya jotoa kutoka ardhini ambazo zilikuwa 0.3% ya mahitaji yote ya umeme duniani lakini katika nchi kadhaa kama Iceland au Kenya asilimia ilikuwa kubwa zaidi.

Katika mazingira ya kivolkeno joto kutoka ganda linafikia uso wa dunia na hapa ni rahisi kutumia mvuke unaotoka au akiba za maji moto zilizopo mita chache chini ya uso wa ardhi kuendesha rafadha za kutengeneza umeme. Nafasi hii iko pia katika sehemu za Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki nchini Kenya ambako hadi sasa kuna vituo 3 vya joto ardhi katika Olkaria.

Katika mazingira ya kawaida pasipo na volkeno au njia za magma zinazokaribia uso wa dunia kuna uwezekano kupeleka mabomba ardhini na kupitisha kiowevo kwa pampu katika mabomba haya chini ya ardhi. Tofauti ya joto kati ya kina ambako mabomba yanafikia na uso wa dunia hutumiwa kwa kupashaia nyumba joto au baridi.

Kama kiwango cha joto kinachotolewa ardhini hakizidi kiwango kinachozalishwa katika kina ya ardhi nishati inayopatikana hapa ni kama nishati mbadala.

                                     

3. Viungo vya Nje

 • Alliant Geothermal Energy
 • Energy Efficiency and Renewable Energy - Geothermal Technologies Program
 • International Energy Agency Geothermal Energy Homepage
 • Geothermal Energy Association
 • Bassfeld Technology Transfer - Introduction to Geothermal Power Generation 3.6 MB PDF file
 • MIT-led panel backs geothermal energy source
 • MIT - The Future of Geothermal Energy 14 MB PDF file Archived 2011-03-10 at Archive-It
                                     
 • Pangaia pia: Pangaea kutoka Kigiriki πᾶν pan yote na γαῖα gaia ardhi dunia ni neno linalomaanisha dunia yote, dunia nzima Katika nadharia ya sayansi
 • kitropiki. Kutoka kaskazini kuelekea kusini kuna kanda zifuatazo zinazofuatana katika nchi kwa jumla: tundra au maeneo baridi ambako ardhi imeganda mwaka
 • Metali kutoka Kiingereza metal ni kundi la elementi zenye tabia za pamoja kama vile zinapitisha umeme kwa urahisi zinapitisha joto zinang aa ni wayaikaji
 • ozoni iliyoko. Ozoni hufyonza mnururisho wa urujuanimno kutoka nuru ya Jua na kuibadilisha kuwa joto Hii ni tofauti na tabakatropo iliyoko chini yake. Huko
 • hakitoshi kila mahali kutofautisha maeneo makavu. Mm 200 za mvua katika eneo la joto zitasababisha eneo kuonekana kama jangwa kabisa kwa sababu kiasi kikubwa
 • kwenye kusini au kaskazini ya jangwa iliyotumia maji chini ya ardhi yaliyoshuka kutoka milima. Miji muhimu ya oasisi ilikuwa Kashgar, Marin, Niya, Yarkand
 • kuingia katika vilindi vyenye joto kubwa inayeyushwa tena na kujiunga na magma ya koti la Dunia. IPA: lith usfēr, kutoka maneno ya Kigiriki λίθος líthos
 • kama tabaka juu ya uso wa ardhi yalifunikwa kwa udongo na kubadilishwa kwa shindikizo na joto Makaa yote yaliyopo chini ya ardhi ni matokeo ya mchakato
 • Gesi asilia ni gesi inayopatikana katika ardhi na inayotumiwa na binadamu kama fueli. Kikemia ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali kama methani zilizotokana

Users also searched:

magma,

...
...
...