Back

ⓘ Jamaika ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi. Iko km 150 kusini kwa Kuba na 150 upande wa magharibi wa Haiti na ni kisiwa kikubwa cha tatu kati ya Antili ..
Jamaika
                                     

ⓘ Jamaika

Jamaika ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi. Iko km 150 kusini kwa Kuba na 150 upande wa magharibi wa Haiti na ni kisiwa kikubwa cha tatu kati ya Antili Kubwa. Katika lugha ya Kiingereza visiwa hivyo huitwa "West Indies" visiwa vya Uhindi wa Magharibi.

Jina limetokana na neno la Kiarawak "Xaymaca" au "Chaymaka" linalomaanisha "nchi ya chemchemi" yaani kisiwa chenye maji matamu.

Mji mkuu ni Kingston.

                                     

1. Jiografia

Kisiwa kina urefu wa km 240 na upana hadi km 85. Eneo lake ni km² 10.991.

Visiwa vidogo vya Pedro Cays vyenye eneo la ha 23 jumla ni sehemu ya nchi ya Jamaika.

Mashariki mwa kisiwa kuna safu ya milima ya buluu yenye urefu wa km 100 penye kilele cha Blue Mountain Peak m 2256 juu ya UB.

Katikati kuna nyanda za juu zilizojengwa kwa mawe ya chokaa yenye mabonde marefu.

Upande wa kusini nyanda za juu zina mtelemko mkali hadi mwambao wa bahari.

Iko mito mingi mifupi; mto mrefu ni Black River yenye km 53.4. Mto wa Hectors River una mwendo wa km 6 chini ya ardhi.

                                     

2. Hali ya hewa

Hali ya hewa ni ya kitropiki. Hakuna tofauti kubwa ya halijoto mwaka wote. Halijoto ya wastani katika Kingston ni 25 °C wakati wa Januari na 27 °C wakati wa Julai.

Usimbishaji hutofautiana katika kanda mbalimbali ya kisiwa. Milima ya kaskazini-mashariki hupokea zaidi ya mm. 5.000 lakini Kingston ina mm 813 pekee. Mvua inanyesha hasa Mei, Juni, Oktoba na Novemba. Miezi ya Septemba na Oktoba inaona dhoruba kali za tufani mara kwa mara.

                                     

3. Miji

Miji muhimu iko mwambaoni kwa sababu ya milima ya ndani.

 • Kingston ni mji mkubwa wenye wakazi karibu laki sita. Ni mji mkuu na mahali pa chuo kikuu kikubwa cha Jamaika. Mji ulikuwa na matatizo makubwa ya usalama katika miaka ya nyuma.
 • Spanish Town ni mji wa pili wenye wakazi 145.000. Ni kitovu cha eneo la kilimo cha ndizi na miwa.
 • Mji wa Montego Bay upo kaskazini mwa kisiwa karibu na mahali ambako Kristoforo Kolumbus alifika mara ya kwanza. Bandari yake ni mhimili wa biashara ya nje. Ni eneo la utalii.
                                     

4. Historia

Wakazi wa kwanza wa Jamaika walikuwa Wataino ambao ni kabila mojawapo la Waarawak kutoka Amerika Kusini. Walikuwa wakulima na wavuvi. Wamepotea kama utamaduni wa pekee baada ya kufika kwa Wazungu kutokana na magonjwa mageni yaliyofika na Wahispania na mauaji wakati wa vita. Waliobaki waliingia katika ndoa na Wazungu au Waafrika waliofika baadaye na kuwa sehemu ya wakazi chotara kisiwani.

Kristoforo Kolumbus alifika mwaka 1494 na kuweka kisiwa chini ya utawala wa Hispania. Aliamini ya kwamba alifika Uhindi akaita visiwa hivi "Uhindi wa Magharibi" na wenyeji wakaitwa "Indios" kwa Kihispania "Wahindi" na baadaye mara nyingi "Wahindi wekundu".

Mwaka 1655 Waingereza waliteka kisiwa wakaanzisha uchumi wa mashamba makubwa ya miwa. Jamaika imekuwa mahali pakuu pa kutengeneza sukari duniani kote. Watumwa wengi Waafrika walipelekwa kisiwani kama wafanyakazi kwenye mashamba hayo. Ndio mababu wa 90% wa wakazi wa leo wa Jamaika.

Kati ya miaka 1834 na 1838 utumwa ulifutwa.

Mwaka 1958 Jamaika ilianza kuelekea uhuru kama jimbo la "Shirikisho la Uhindi wa Magharibi".

Uhuru kamili ulipatikana mwaka 1962.                                     

5. Wakazi

Mwaka 2012 Jamaika ilikuwa na wakazi 2.889.187. Nusu yao waliishi mjini. Umri wa wastani ni miaka 23, thuluthi moja ni watoto hadi miaka 14.

Takriban 91.4 % ya wakazi ni wa asili ya Afrika. Mababu walikuwa watumwa kutoka Afrika waliofikishwa kisiwani katika karne ya 17 na karne ya 18 au ni machotara au wa asili ya Ulaya na Uchina.

Wakazi asilia walikuwa Waarawak na Wataino ambao hawako tena kama vikundi vya pekee; wengi walikufa kutokana na magonjwa ya Wazungu au vita vya miaka ya kwanza baada ya kufika kwa Wahispania. Wengine walichanganyikana na vikundi vingine.

Mbali ya wakazi, Wajamaika au wenye asili ya kisiwa kama 2.500.000 wanaishi nje ya nchi.

                                     

5.1. Wakazi Lugha

Pamoja na lugha rasmi ambayo ni Kiingereza kuna pia aina ya Krioli yenye asili ya Kiingereza: ndiyo inayotumika kawaida.

                                     

5.2. Wakazi Dini

Wakazi walio wengi hufata Ukristo hasa katika madhehebu ya Uprotestanti kama vile:

 • Wabaptisti 7%
 • Wamoravian 1%
 • Wasabato 11%
 • United Church 2%
 • Wamethodisti 2%
 • Waanglikana 4%
 • Church of God 24%
 • Brethren 1%
 • Wapentekoste 10%

Wakatoliki ni 2%, na vilevile Mashahidi wa Yehova.

Dini iliyoanzishwa Jamaika ni Rastafari ambayo mwaka 2001 ilikuwa na wafuasi 24.000.

                                     

6. Utamaduni

Muziki ni sehemu muhimu sana katika utamaduni wa Jamaika. Hasa muziki ya Reggae umejulikana kote duniani. Mwanamuziki mashuhuri hasa wa Jamaika alikuwa Bob Marley na kikundi chake cha "The Wailers".

Pia Wajamaika wana mafanikio makubwa katika riadha, hasa ya masafa mafupi.

                                     

7. Viungo vya nje

 • Official webpage of Queen Elizabeth as Queen of Jamaica
 • Official website of the Jamaica Information Service
 • Government of Jamaica Archived Februari 20, 2009 at the Wayback Machine.
 • The Cabinet Office of the Government of Jamaica Archived Aprili 29, 2011 at the Wayback Machine.
                                     
 • Popcaan amezaliwa na jina la Andrae Hugh Sutherland mnamo 19 Julai 1988 mjini Saint Thomas, nchini Jamaika ni msanii wa Reggae pamoja na Dancehall.
 • Rastafari wakati mwingine huitwa Urastafari ni dini iliyoanzishwa huko Jamaika miaka ya 1930. Wakati mwingine dini hii hutambuliwa pia kuwa mfumo wa maisha
 • Barbuda Aruba Bahamas Barbados Dominica Jamhuri ya Dominika Grenada Haiti Jamaika Korsou Kuba Saint Kitts na Nevis Saint Lucia Saint Vincent na Grenadini
 • 1948 ni mwimbaji na mwanamuziki mwenye mizizi ya Reggae kutoka nchini Jamaika aliyeshinda tuzo ya Grammy. Kama wengi wa wasanii maarufu wa Reggae, Burning
 • April Jackson amezaliwa tar. 1990, Uingereza ni mwanamitindo kutoka Jamaika Aprili Jackson alikuwa Miss Jamaica Universe mwaka 2008. Yeye kuwakilishwa
 • nafasi ya kwanza mbele ya Jade Bailey wa Barbados na Sherone Simpson wa Jamaika Alikimbia mbio hiyo kwa muda wa sekunde 11.24 na kuhitimu kuingia awamu
 • 1949 19 Agosti 2006 alikuwa mtunzi na mwimbaji wa Reggae toka nchini Jamaika Alianza muziki katika kundi lijulikanalo kama The Soul Defender lililokuwa
 • 1945 - 11 Mei 1981 alikuwa mwimbaji na mwanamuziki muhimu kutoka nchini Jamaika Alivuma hasa kunako miaka ya 1970 na 1980. Ameweza kuifanya staili ya

Users also searched:

...
...
...