Back

ⓘ Jipu ni tatizo la ngozi linalotokana na maambukizi ya kina ya folikuliti au maambukizi ya folikoli za nywele za jasho; mara nyingi unasababishwa na bakteria Sta ..
Jipu
                                     

ⓘ Jipu

Jipu ni tatizo la ngozi linalotokana na maambukizi ya kina ya folikuliti au maambukizi ya folikoli za nywele za jasho; mara nyingi unasababishwa na bakteria Stafilokokasi aureasi, ambayo husababisha kuvimba kwa eneo chungu lililo juu ya ngozi kutokana na mkusanyiko wa usaha na tishu mfu.

Majipu yakijikusanya huitwa kimeta.

                                     

1. Dalili na ishara

Majipu ni vijivimbe vyekundu, ambavyo hujaa na usaha ulioko karibu na vinyweleo ambavyo ni laini, vya moto, na vinanavyouma sana. Yana ukubwa mbalimbali, kuanzia punje hadi ukubwa wa mpira wa golfu. Sehemu ya njano au nyeupe katikati ya uvimbe inaweza kuonekana wakati jipu likiwa tayari kutoa au kutokwa na usaha.

Katika maambukizi makali, mtu anaweza kuhisi homa, kuvimba tezi au mtoki, pamoja na uchovu.

Jipu linalojirudia mara kwa mara linaitwa ngozi-jipu.

                                     

2. Sababu

Kwa kawaida bakteria, kama vile stafilokoki, ndio husababisha jipu kutokea kwenye ngozi. Ukoloni wa bakteria huanza katika vinyweleo na inaweza kusababisha seluli ya chini ya ngozi na kuvimba. Zaidi ya hayo, maiasisi inayosababishwa na wadudu wa kuruka aina ya Tumbu katika Afrika, kawaida huonesha majipu.

Sababu hatarishi za ngozi-jipu ni pamoja na bakteria katika tundu la pua, ugonjwa wa kisukari, fetma, neoplasmi s lymphoproliferative, utapiamlo, na matumizi ya madawa yanayokandamiza kingamwili.

                                     

3. Matatizo yanayojitokeza

Matatizo kawaida yanayotokana na kuambukizwa na majipu ni makovu na maambukizi au usaha wa ngozi, uti wa mgongo, ubongo, figo na viungo vingine. Maambukizi pia huweza kuenea hadi kwenye mfumo wa damu sepsisi na kuwa tishio kwa uhai.

                                     

4. Matibabu

Majipu yote lazima yafyonzwe ili kupona. Kunyonywa kunawezekana kwa kutumia kitambaa kilicholowa kwenye maji moto yenye kutiwa chumvi. Kuosha pamoja na kufunika jipu na krimu ya antibiotiki au mafuta ya antiseptiki kwa jina maarufu tea tree oil na kufunga bendeji kunasababisha kupona kwa haraka. Majipu hayastahili kufinywa au kutobolewa bila idhini ya daktari au muuguzi yeyote, kwani kunaweza kusababisha maambukizi mengine.

Katika hatari ya kutosababisha matatizo makubwa ni lazima majipu yakatwe au yafyonzwe na daktari. Hii ni pamoja na majipu makubwa yanayokaa zaidi ya wiki mbili, ama yale yanayopatikana katikati ya uso au kwenye uti wa mgongo.

Tiba ya antibiotiki linahimizwa haswa kwa kupigana na majipu makubwa yanayopatikana kwenye sehemu nyeti kama vile pua na ndani ya masikio.

                                     
  • vijidudu vitaenea hadi kwenye utando wa ule mfupa na hatimaye kusababisha jipu na madhara mengine kinywani. Zaidi ya kuoza kwa meno kuna ugonjwa wa mishipa
  • pafu zitatengeneza kibonge cha kiowevu chenye maambukizi kiitwacho jipu la pafu. Jipu kwenye pafu huonekana kwa eksirei ya kifua lakini mara kwa mara huitaji
  • Taifa ya Kenyatta Huduma ya kwanza Jenetikia Jeraha la moto Jinekomastia Jipu Jiua Jongo Kafeini Kamusi ya Tiba Kandidiasisi Kaswende Kichaa Kichapuzi
  • kutambua uwezekano wa tyuma, ya rektamu polipsisi, prosteti iliyo kubwa, au jipu Uchunguzi huu unaweza kutofaulu bila utulizaji unaofaa kwa sababu ya maumivu
  • epiglotitisi, njia ya hewa kifaa kigeni, stenosisi ya subglottic, anjioedema, jipu lililo nyuma ya farinksi, na trakeitisi ya bacteria. Eksirei ya upande wa

Users also searched:

...
...
...