Back

ⓘ Justino de Jacobis alikuwa mtawa wa Shirika la Misheni, halafu askofu na mmisionari nchini Ethiopia na Eritrea. Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu t ..
                                     

ⓘ Justino de Jacobis

Justino de Jacobis alikuwa mtawa wa Shirika la Misheni, halafu askofu na mmisionari nchini Ethiopia na Eritrea.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu tarehe 26 Oktoba 1975. Hata Wakristo wengine na Waislamu wanatembelea kaburi lake kwa heshima.

Sikukuu yake ni tarehe 31 Julai.

                                     

1. Maisha

Akiwa mtoto wa saba wa Giovanni Battista de Jacobis na wa Maria Giuseppina Muccia, tarehe 17 Oktoba 1818 alijiunga na utawa huko Napoli akaweka nadhiri miaka miwili kamili baadaye.

Ingawa alitaka kukataa kwa unyenyekevu wake mkubwa, alipata upadrisho huko Brindisi tarehe 12 Juni 1824.

Kisha kufanya uchungaji huko Oria na Monopoli, alifanywa mkuu wa kanda katika shirika lake kwanza Lecce halafu Napoli. Huko alijitosa kuhudumia waliopatwa na kipindupindu mwaka 1836.

Akiwa huko alielezwa na Kardinali Franzoni juu ya haja ya umisionari nchini Ethiopia.

Mwaka 1839 alichaguliwa kuwa mkuu wa kitume nchini huko ili aanzishe misheni katoliki.

Justino alijitahidi kujifunza vizuri lugha za nchi, kuishi pamoja na wenyeji, akifuata utamaduni wao na mifano ya wamonaki wao.

Vilevile katika uinjilishaji alitumia mapokeo na liturujia ya Ethiopia, akiweka msingi wa Kanisa Katoliki la Ethiopia.

Baada ya kufanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa miaka minane, mwaka 1847 aliteuliwa kuwa askofu wa Nilopolis na makamu wa Papa kwa Uhabeshi, ila alikataa uaskofu hadi alipolazimika mwaka 1849.

Ingawa alipata mapingamizi mengi hasa kutoka kwa Abuna Salama II, askofu mkuu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia kufungwa, kufukuzwa n.k., aliweza kuanzisha misheni na shule nyingi hasa kwa lengo la kuandaa mapadri wenyeji.

Hatimaye askofu mkuu huyo alikiri kwamba hakuna mtu aliyewahi kushika vizuri maagizo na mashauri ya Injili kuliko Justino.

Kati ya watu 12.000 hivi aliowaongoa, mmojawapo ni mwenyeheri Ghebre Mikaeli.

                                     

2. Heshima baada ya kifo

Kesi ya kumtangaza mwenye heri ilianza tarehe 13 Julai 1904, ikamalizika tarehe 25 Julai 1939 chini ya Papa Pius XII.

Alitangazwa na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu tarehe 26 Oktoba 1975, akiwa wa kwanza kati ya wamisionari wa Afrika kusini kwa Sahara.

                                     

3. Mlolongo wa kitume

 • Papa Benedikto XIII, O.P.
 • Kardinali Ulderico Carpegna
 • Kardinali Girolamo Bernerio, O.P.
 • Papa Klementi XIII
 • Kardinali Bernardino Giraud
 • Kardinali Scipione Rebiba
 • Kardinali Giacomo Filippo Fransoni
 • Kardinali Paluzzo Paluzzi Altieri degli Albertoni
 • Kardinali Guglielmo Massaia, O.F.M. Cap.
 • Askofu Giustino de Jacobis, C.M.
 • Kardinali Alessandro Mattei
 • Kardinali Ludovico Ludovisi
 • Askofu mkuu Galeazzo Sanvitale
 • Kardinali Pietro Francesco Galleffi
 • Kardinali Giulio Antonio Santorio
 • Papa Benedikto XIV
 • Kardinali Luigi Caetani
                                     

4. Marejeo

 • Devin, A., Traduzione inglese di Lady Elizabeth Herbert of Lea, Abyssinia and its Apostle, Burns and Oates, London, 1867
 • Antonio Furioli, Il frutto più prezioso dellapostolato di San Giustino de Jacobis. Il Beato Gabra Mikā’ēl 1791-1855, martire per la fede in Abissinia in Rivista di ascetica e mistica, 75 luglio-settembre 2006 3, 385-403.
 • Antonio Furioli, Leucaristia, epifania di dialogo e di comunione. Sua esemplarità in San Giustino de Jacobis in Rivista di ascetica e mistica, 75 aprile-giugno 2006 2, 213-228.
 • Mkusanyo wa maandishi yake - Giuseppe Guerra - Ed. Vincenziani kwa Kiitalia.
 • Antonio Furioli, Vangelo e testimonianza. Lesperienza di San Giustino de Jacobis in Abissinia 1839-1860, Milano, San Paolo, 2008.
                                     

5. Viungo vya nje

 • Saints of July 31: Giustino de Jacobis Archived Juni 22, 2008 at the Wayback Machine.
 • Hotuba ya Papa Paulo VI katika kumtangaza mtakatifu
 • edition of A. Devin Maisha yake
 • Justin de Jacobis Justino katika Catholic Encyclopaedia
                                     
 • Bernhard Heine, mgunduzi wa osteotomi kutoka Ujerumani 1860 - Mtakatifu Justino de Jacobis C.M., askofu Mkatoliki kutoka Italia mmisionari nchini Ethiopia 1875
 • Septemba - George Bentham 2 Oktoba - Nat Turner 9 Oktoba - Mtakatifu Justino de Jacobis askofu Katoliki nchini Ethiopia 25 Oktoba - Jacques Paul Migne, padre
 • Mtakatifu Yosefu Cafasso, padri nchini Italia 31 Julai - Mtakatifu Justino de Jacobis askofu Mkatoliki kutoka Italia mmisionari nchini Ethiopia 21 Septemba
 • Gaspare Bertoni, padri mwanzilishi kutoka Italia 1800 - Mtakatifu Justino de Jacobis C.M., askofu Mkatoliki kutoka Italia, mmisionari nchini Ethiopia
 • wa Aleksandria, patriarki wa Kanisa la Kikopti 1831 - 1927, Misri Justino de Jacobis askofu wa Wavinsenti 1838 - 1860, Ethiopia na Eritrea Antoni Maria
 • Justini wa Chieti Ndiyo Ndiyo Ndiyo Ndiyo Justiniani I Ndiyo Justino de Jacobis Ndiyo Justus wa Canterbury Ndiyo Ndiyo Ndiyo Juventino na

Users also searched:

...