Back

ⓘ Kamusi za Kiswahili ni zile zinazofafanua maana ya maneno ya lugha hiyo ya Afrika Mashariki ambayo inazidi kuenea hasa barani Afrika. Kamusi hizo ni vyombo muhi ..
                                     

ⓘ Kamusi za Kiswahili

Kamusi za Kiswahili ni zile zinazofafanua maana ya maneno ya lugha hiyo ya Afrika Mashariki ambayo inazidi kuenea hasa barani Afrika.

Kamusi hizo ni vyombo muhimu kwa kukuza na kuimarisha Kiswahili, ambacho kwa sasa ni lugha rasmi ya Jumuia ya Afrika Mashariki na mojawapo kati ya lugha za mawasiliano za Umoja wa Afrika.

                                     

1. Historia ya awali

Kamusi za lugha hiyo zilianza kupatikana katika karne ya 19 BK, kabla na wakati wa ukoloni wa Kizungu katika nchi za Afrika Mashariki. Hivyo watungaji wa kamusi za kwanza walikuwa Wazungu waliofahamu vizuri lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, n.k.

Waswahili wenyewe, watu wa pwani ya Afrika Mashariki na visiwa vya jirani kama Unguja na Pemba, hawajulikani kuwa wametunga kamusi kabla ya wakati huo. Wasomi wao walijua kwa viwango tofauti Kiarabu, ambacho kilikuwa lugha kuu ya elimu kwenye mwambao wa Bahari Hindi mashariki mwa Afrika na pia lugha ya kidini katika Uislamu.

Vilevile hatuna habari kwamba Wareno waliofika Afrika ya Mashariki tangu mwaka 1500 hivi walitunga kamusi.

Utungaji wa Kamusi za Kiswahili ulianza kwa kukusanya orodha za maneno/msamiati wa Kiingereza-Kiswahili na Kifaransa-Kiswahili. Msamiati wa Kiswahili ulikusanywa ili kuwasaidia wageni hawa kuifahamu lugha ya Kiswahili na waweze kuwasiliana na wenyeji wao ambao ni Waswahili. Nakala za msamiati huo zilipelekwa Uingereza ili wageni wengine waliotaka kufika Afrika Mashariki wajifunze kabla hawajafika katika nchi hizo.

Mfano wa kwanza ni mkusanyo wa maneno uliyofanywa na nahodha Mwingereza T. Smee alipotembelea pwani kuanzia Somalia hadi Zanzibar kwenye mwaka 1811-1812; alikusanya istilahi 250 hivi za Kiingereza na maana yake kwa Kiswahili alichoita "Souallie", Kisomali na lugha ya Wagalla. Orodha hiyo ilichapishwa kwenye mwaka 1844. Wengine wanaotajwa ni Henry Salt 1811-1813 na Browse Ross 1843. Msamiati uliokusanywa na watu hao unafikiriwa kuwa ni wa Kiswahili cha kaskazini mwa Mombasa na ulikuwa na maneno machache sana. Wakati huo mchungaji Krapf alikuwa ameshaanza kazi ya kutunga kamusi yake.

                                     

2. Ludwig Krapf

Kamusi ya kwanza inayojulikana ilitungwa mnamo 1848 na Ludwig Krapf huko Rabai Mpya / Mombasa Kenya; ilikamilishwa na kutolewa kama "A Dictionary of the Suahili language, London 1882". Kamusi inapatikana pia mtandaoni.

Tahajia ya maneno mara nyingi ni tofauti na kawaida ya leo kwa sababu usanifishaji wa lugha ulitokea tu miaka 40-50 baada ya kutokea kwa kamusi yake; pia alikusanya maneno mengi huko Rabai / Mombasa kwa hiyo athira ya Kimvita ni kubwa. Pia si rahisi kutumia kamusi yake kwa sababu ilhali alitoa maana ya maneno ya Kiswahili kwa Kiingereza aliongeza maelezo juu ya matumizi na etimolojia kwa lugha ya Kilatini.

Alipoanza kazi aliamua kutotumia mwandiko wa Kiarabu uliokuwa njia ya kawaida ya kuandika Kiswahili akiona haulingani sana na lugha yenyewe, maana Kiarabu kina herufi kadhaa kwa sauti ambazo hazipatikani katika Kiswahili. Alitafakari angetumia herufi za Kiamhari alichojua vizuri lakini aliamua kuendelea kwa alfabeti ya Kilatini kwa sababu hakutaka kuwapa wanafunzi wa lugha tatizo la kupambana na alfabeti ya ziada.

                                     

3. Kamusi nyingine za kwanza

Wengine walioendelea kukusanya maneno na kutoa kamusi ni

 • A. C. Madan English-Swahili Dictionary, Oxford 1901 online hapa
 • A. C. Madan Swahili-English Dictionary Oxford 1903 online hapa.
 • Askofu Mwanglikana Edward Steere A handbook of the Swahili language: as spoken at Zanzibar. London: Bell & Daldy, 1870 online hapa

Kamusi ya Kiswahili - Kijerumani ya kwanza ilitungwa mwaka 1890, wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, na Carl Gotthilf Büttner Wörterbuch der Suaheli-Sprache, Berlin 1891 aliyetoa pia matini za Kiswahili kwa mwandiko wa Kiarabu. Kamusi pana zaidi ilitolewa mwaka 1911 na Carl Velten Suaheli Wörterbuch, Berlin 1910.

Kamusi ya Kiswahili - Kifaransa ilitolewa na Charles Sacleux Sacleux, Charles. 1939. Dictionnaire Swahili - Français. Travaux et Mémoires de lInstitut dEthnologie, Vols. 36/37. Paris: Institut dEthnologie, Université de Paris. Reprint 1959). Kamusi hii imesifiwa kuwa ya pekee iliyokusanya pia maneno ya lahaja za Kiswahili nje ya Kiunguja Zanzibar na Kimvita Mombasa. Inasifiwa pia kwa upana wa maelezo yake kuhusu historia ya maneno.                                     

4. Kiswahili sanifu

Hadi mwanzo wa karne ya 20 Kiswahili kilipatikana katika lahaja zake tu. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza kamati iliundwa na serikali ya kikoloni kwa kusudi la kuunda Kiswahili sanifu kitakachotumiwa kote Afrika ya Mashariki. Kamusi mbili za "Inter-territorial Language Swahili committee to the East African Dependencies" zilitolewa mwaka 1939 na zimechapishwa upya mara nyingi. Mhariri mkuu wa kamati alikuwa katibu wake Frederick Johnson. Msingi wa kamusi hizi ulikuwa kazi ya Madan taz. juu. Hivyo kamusi hizi hutajwa kama Madan-Johnson ".

                                     

5. Kiswahili tangu uhuru

Tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi za Afrika ya Mashariki Kiswahili kiliendelea sana. Azimio la serikali ya Tanzania la kufanya Kiswahili kuwa lugha ya elimu katika shule za msingi lilianzisha masharti ya kutunga vitabu vya shule na kupanua msamiati wa Kiswahili. Orodha za maneno zilitungwa kwa ajili ya masomo mbalimbali.

Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili leo: TATAKI katika Dar es Salaam ilianza kuandaa kamusi mbalimbali, hasa "Kamusi ya Kiswahili Sanifu" inayoeleza maana ya maneno kwa kutumia lugha yenyewe. Kamusi mbalimbali zilifuata.

                                     

6. Kamusi za maana zinazopatikana madukani

Vifupisho katika mabano si vya kawaida lakini vimeingizwa hapa kwa kusudi la kurahisisha marejeo katika makala za Wikipedia.

Kiitalia - Kiswahili - Kiitalia

 • Pick, M. Vocabolario Kiswahili-Italiano Italiano-Kiswahili Kamusi ya Kiswahili - Kiitalia - Kiswahili
                                     

6.1. Kamusi za maana zinazopatikana madukani Kiswahili - Kiswahili

 • Wamitila, K.W., Kamusi ya Fasihi. Istilahi na Nadharia, Focus Books, Nairobi 2003, ISBN 9966 882 79 6
 • Kamusi ya Kiswahili Sanifu KKS. Dar es Salaam, Tanzania: Oxford University Press. 1981, 2004, 2013. imetungwa na TATAKI, awali TUKI
 • Wamitila, K.W., Kamusi ya Tashbihi, Vitendawili, Milio na Milingano, Longhorn 2003, ISBN 9966 49 768 4
 • Massamba, D.P.B., Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha, TUKI, Dar es Salaam, 2004, ISBN 9976 911 73 4
 • Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia / English-Swahili Dictionary of Biology, Physics and Chemistry - TUKI/UNESCO/SIDA, Dar es Salaam, 1990
 • Kamusi ya Karne ya 21 KK21. Nairobi, Kenya: Longhorn. 2011 - ISBN 978 9966 36 120 0.
 • Kamusi la Kiswahili Fasaha KKF, imetungwa na BAKIZA, Oxford 2010 - ISBN 978 019 5736182.
 • Bakhressa, Salim K., Kamusi ya Manaa na Matumizi KMM. Nairobi, Kenya: Oxford University Press, 1992
 • Arege, T. - Nyanje, M., Kamusi Fafanuzi ya Methali, Target Publications Ltd, Nairobi 2011, ISBN 9966 002 41 3
 • Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha - TUKI/UNESCO/SIDA, Dar es Salaam, 1990, ISBN 9976 911 10 6
 • Kamusi Kuu ya Kiswahili KKK. Nairobi, Kenya; Kampala, Uganda; Dar es Salaam, Tanzania: Longhorn, 2015. imetungwa na BAKITA
 • Mwansoko H.T.Z. - Tumbo-Masabo Z.N. - Sewangi S.S., Kamusi ya Historia - TUKI, Dar es Salaam, 2004 - ISBN 9976 911 75 0
 • Kamusi ya Tiba KyT, TUKI, dar es Salaam 2003, ISBN 9976-911-65-3
 • Mlingwa, C.O.F. - Kiango, J.G., Kamusi ya Ndege kwa Picha, TUKI 2006ù
 • Mdee T.S. - Kiango J.K., Kamusi ya Wanyama - TUKI 2008, ISBN 978 9987 442 263
 • Mkota, A., Kamusi ya Methali, Vide-Ruwa, Nairobi 2009
 • Tumbo-Masabo, Z.N. - Chuwa A.R., Kamusi ya Biashara na Uchumi, TUKI, Dar es Salaam, 1995, ISBN 9976 911 37 8
 • Mwita, A.M.A. - Mwansoko, H.J.M., Kamusi ya Tiba TUKI 2003
 • Kamusi Teule ya Kiswahili KTK. Nairobi, Kenya: East Africa Educational Publishers, 2014.
 • Kingei, K. - Ndalu, A., Kamusi ya Semi, EAEP Ltd, Nairobi, Kampala, Dar es Salaam, 1988-2007, ISBN 9966 46 898 6
 • Kiputiputi, Omari M. Kamusi Sanifu ya Kompyuta KSK, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, toleo la kwanza 2011, ISBN 978 9987 531 12 7
 • Mkota, A. - Sakara, F., Kamusi ya Semi, Vide-Ruwa, Nairobi 2011
 • Mohamed, H.A. - Mohamed, S.A., Kamusi ya Visawe, Swahili Dictionary of Synonims, EAEP, Nairobi, Kampala, Dar es Salaam, 1998
 • Nyenyembe, J. - Kamusi ya Ukristo, Mkuki na Nyoka, Dar es Salaam, 2016, ISBN 978-9987-753-17-8


                                     

6.2. Kamusi za maana zinazopatikana madukani Kiswahili - Kiingereza

 • Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinolojia KAST. Dar es Salaam, Tanzania: Ben & Co. Ltd., 1995.imetungwa na TUKI
 • Madan-Johnson, A Standard Swahili-English Dictionary M-J SSE
 • Kamusi ya Kiswahili - Kiingereza Swahili-English Dictionary KKK/SED
                                     

6.3. Kamusi za maana zinazopatikana madukani Kiingereza - Kiswahili

 • Familia za Maamkio, English-Kiswahili Catholic Dictionary a first English-Swahili dictionary of terms in use in the Catholic Church - with glosses in Latin and Italian - Ndanda Mission Press, 2001, ISBN 9977 663 625 3
 • Mlacha, S.A.K., Kamusi ya Sheria Kiingereza-Kiswahili, TUKI 1999
 • Kirkeby, Willy A. English Swahili Dictionary Kamusi ya Kiingereza-Kiswahili
 • English-Swahili Dictionary Kamusi ya Kiingereza-Kiswahili KKK/ESD
 • Kamusi sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia English-Swahili dictionary of Biology, Physics and Chemistry, David P.B. Massamba & alii, kutolewa na TUKI/UNESCO/SIDA,TUKI 1990, chapa ya tatu 2012, ISBN 9976 911 09 2
 • Snoxall R.A. - Mshindo H.B., Concise English-Swahili Dictionary / Kamusi ya Kiingereza-Kiswahili
 • Madan-Johnson, A. Standard English-Swahili Dictionary M-J SES
                                     

6.4. Kamusi za maana zinazopatikana madukani Kiitalia - Kiswahili - Kiitalia

 • Pick, M. Vocabolario Kiswahili-Italiano Italiano-Kiswahili Kamusi ya Kiswahili - Kiitalia - Kiswahili
                                     

6.5. Kamusi za maana zinazopatikana madukani Kiswahili - Kijerumani

 • Handwörterbuch Swahili-Deutsch, von Hildegard Höftmann, Irmtraud Herms Langenscheidts Handwörterbuch München 2000, ISBN 3468043902
 • Handwörterbuch Deutsch-Swahili von Karsten Legere Langenscheidts Handwörterbuch München 2000, ISBN 3468043910
 • Swahili: Wörterbuch des internationalen Swahili, von Cosmo Ambokile Lazaro, 2010 Verlag AM-CO Publishers, Cologne, ISBN 978-3-9806714-5-3
                                     

7. Kamusi zinazopatikana kwa njia ya intaneti

 • Elimuyetu.co.tz English-Swahili dictionary
 • Vocabolario Italiano-Swahili Kamusi ya Kiitalia-Kiswahili
 • A dictionary of the Suahili language, by L Krapf, 1882
 • Kamusi ya Sacleur kwenye tovuti ya Chuo Kikuu cha Leipzig
 • Swahili - English dictionary, by A C Madan, London 1903
 • Elimuyetu.co.tz Swahili-English dictionary
 • Madan-Johnson, A Standard English-Swahili Dictionary - Online edition via google-books
 • The Kamusi Project ilikuwa kamusi ya Kiswahili lakini tangu miaka haiionyeshi tena maudhui upande wa kiswahili, Multilingual, zamani: INTERNET LIVING SWAHILI DICTIONARY ILSD
                                     

8. Viungo vya nje

 • Gudrun Miehe & Henrike Fiersching, Exploring Krapfs Dictionary Archived Machi 9, 2016 at the Wayback Machine., utathmini wa kamusi ya Krapf, pamoja na orodha ya maneno, katika Swahili Forum 16, Special Edition 2009; ilitazamiwa Juni 2015
 • Arvi Kurskainen, Tathmini ya Kamusi Tano za Kiswahili, Nordic Journal of African Studies 112: 283-301 2002
                                     
 • Afrika ya Mashariki. Kamati hiyo iliandaa kamusi mbili za Kiingereza - Kiswahili M - J SES na pia Kiswahili - Kiingereza. Mhariri Mkuu wa kamati alikuwa
 • Wikipedia ya Kiswahili au Wikipedia kwa Kiswahili ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kiswahili Wikipedia ya Kiswahili ilianzishwa tarehe
 • Sheng: Kiswahili cha mtaani Nairobi Kenya chenye maneno mengi ya asili ya Kiingereza, Gikuyu na lugha zingine za Kenya. TUKI 1990, Kamusi Sanifu ya
 • mizuri ya riwaya kwa lugha ya Kiswahili ni Nagona au Mzingile, zilizoandikwa na mwandishi Euphrase Kezilahabi. Kamusi ya Fasihi iliyotolewa na K. W.
 • Uingereza katika Afrika ya Mashariki. Kamati iliandaa kamusi mbili za Kiingereza - Kiswahili na pia Kiswahili - Kiingereza M - J SSE Mhariri Mkuu wa kamati alikuwa
 • KKK ESD ni kifupi cha Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili English - Swahili Dictionary iliyoandaliwa na wataalamu wa TUKI kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
 • kufanya utafiti wa lugha na kutunga kamusi na sarufi za kwanza pamoja na kuunda mfumo wa kuandika Kiswahili kwa herufi za Kilatini. Utawala wa kikoloni ulirahisisha
 • Extended Glossary May 2009 Kiputuputi, Omari 2011 Kamusi Sanifu ya Kompyuta, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Toleo la Kwanza
 • Mwanglikana anayejulikana hasa kwa utafiti wake wa lugha za Kiafrika na hasa kamusi za Kiswahili Alizaliwa 8 Machi 1846 kwenye kijiji cha Cam, Gloucestershire

Users also searched:

...
...
...