Back

ⓘ Kenya Peoples Union. Mnamo Machi 1966, mzozo ulitokea katika mkutano wa chama tawala KANU uliyofanya mlengo wa kushoto wa chama ukiacha chama hicho na kuanzisha ..
                                     

ⓘ Kenya Peoples Union

Mnamo Machi 1966, mzozo ulitokea katika mkutano wa chama tawala KANU uliyofanya mlengo wa kushoto wa chama ukiacha chama hicho na kuanzisha KPU. KANU ilibadilisha sheria za uchaguzi kulazimisha wabunge waliyejiunga na KPU kutetea viti vyao katika uchaguzi mdogo. KPU iliweza kushinda hasa kwa Waluo Mkoani Nyanza pekee, huku waliyesimama kwingine wakishindwa na wanasiasa kutoka chama cha KANU ambacho wakati huo kilikuwa kikitawalwa na wanasiasa Wakikuyu. Mwisho wa Chama hiki uliwadia wakati wa Ufunguzi wa Hospitali ya New Nyanza mnamo 25 Oktoba 1969. Wakati huo rais Jomo Kenyatta hakupendezwa na ufunguzi wa hospitali hiyo kwa vile ilijengwa na fedha za Soviet na ilionekana kama mradi wa Odinga. Hata hivyo Kenyatta aliongoza sherehe za ufunguzi wake ili kuimarisha umaarufu wake Mkoani Nyanza. Wajaluo walijulikana kuwa wenye hasira mno kwa kawaida, hasa kwa serikali tangu mauaji ya Tom Mboya miezi michache iliyotangulia, huku vidole vingi vikimwelekea Kenyatta. Maandamano yalianzishwa wakati wa sherehe hizo za ufunguzi wakati wafuazi wa KPU waliushanbulia msafara wa rais. Zaidi ya watu kumi waliuawa wakati walinzi wa Kenyatta walifunguaufyatuaji wa risasi dhidi ya waandamanaji hao. Odinga na maafisa wengine wa chama cha KPU walititiwa nguvuni siku mbili baada ya tukio hilo. KPU kilifutiliwa mbali mnamo 30 Oktoba 1969, huku Kenya ikibakia na Chama Kimoja.

                                     

1. Wanasiasa wa KPU

Wafuatao ni wanasiasa waliojiunga na KPU. ’Katika mabano ni jimbo la uchaguzi walilowakilisha’’.:

 • Achieng Oneko Nakuru Town
 • Bildad Kaggia Kandara
 • Ondiek Chilo Nyakach
 • Tom Obok Odongo Kisumu Rural
 • Okudo Bala Nyando
 • George Fredrick Oduya Elgon West
 • John Odero-Sar Ugenya
 • Luke Rarieya Obok Alego
 • Joseph Mwasia Nthula Iveti South
 • Wasonga Sijeyo Gem
 • Oginga Odinga Bondo
                                     
 • za Binadamu na za Mataifa kwa Kiingereza: African Court on Human and Peoples Rights ni mahakama ya kibara iliyoanzishwa na nchi za Afrika ili kulinda
 • PNU au Chama cha Umoja wa Kitaifa ni muungano wa vyama vya kisiasa nchini Kenya ulioanzishwa tarehe 16 Septemba 2007 kabla ya uchaguzi mkuu wa rais na bunge
 • Movement ni chama cha kisiasa nchini Kenya Chama hicho kilianzishwa mwaka 2006 katika maandalizi ya uchaguzi wa bunge la Kenya wa mwaka 2007 ikijulikana kama
 • Kwame Nkrumah na chama chake. 1958 alichaguliwa katibu mkuu wa All - African Peoples Conference na wawakilishi wa nchi 28 za Afrika. Kutokana na hali ya afya
 • Movement Party of Kenya ni chama cha kisiasa nchini Kenya Kilianzishwa mwaka 2006 katika maandalizi ya uchaguzi wa bunge la Kenya wa mwaka 2007, lakini

Users also searched:

national bureau of statistics; tanzania 2019 pdf, national bureau of statistics; tanzania 2020 pdf,

...
...
...