Back

ⓘ Khalid bin Barghash wa Zanzibar. Sayyid Khalid bin Barghash Al-Busaid alikuwa mtawala wa 6 wa Usultani wa Zanzibar. Alikuwa sultani kwa siku tatu pekee kuanzia ..
Khalid bin Barghash wa Zanzibar
                                     

ⓘ Khalid bin Barghash wa Zanzibar

Sayyid Khalid bin Barghash Al-Busaid alikuwa mtawala wa 6 wa Usultani wa Zanzibar.

Alikuwa sultani kwa siku tatu pekee kuanzia tarehe 25 Agosti hadi 27 Agosti 1896 akaondolewa madarakani na Waingereza kwa nguvu ya jeshi.

Khalid bin Bargash alikuwa mwana wa kwanza wa Sayyid Barghash bin Said Al-Busaid. Baada ya kifo cha mjomba wake, sultani Hamad bin Thuwaini wa Zanzibar, alitangazwa na sehemu ya viongozi kuwa sultani mpya, lakini wengine walimpinga. Kulikuwa na uvumi wa kwamba alisababisha kifo cha mjomba wake kwa kumsumisha.

Mwakilishi wa Uingereza aliwahi kumkubali mgombea mwingine kutoka familia ya sultani, Hamud bin Mohammed, hakuwa tayari kumwona Khalid kwenye kiti cha mtawala akirejea mkataba kati ya Uingereza na Zanzibar ya mwaka 1890 iliyowapa Waingereza nafasi ya kumkubali sultani mpya.

Khalid alipewa muda wa kuondoka katika jumba la Sultani akakataa, akakusanya zaidi ya askari 2000 tayari kwa utetezi.

Asubuhi ya 27 Agosti 1896 Waingereza walikuwa na manowari 5 tayari kwenye bandari ya Zanzibar zilizolengesha bunduki zake kwa jumba la sultani. Saa 9.02 zilianza kulipiga jumba la sultani na kikosi cha wanajeshi kilishambulia jumba. Saa 9.40 jeshi la Sultani likajisalimisha baada ya kifo cha Wazanzibari 500. Sultani mwenyewe alikimbilia ubalozi wa Ujerumani kisiwani.

Baadaye Wajerumani walimpeleka kwa siri Dar es Salaam, alipopewa hifadhi katika koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, na Hamud bin Mohammed alipanda kiti cha sultani.

Sultani aliyefukuzwa aliishi Dar es Salaam hadi mwaka 1916. Mwaka ule Waingereza walitwaa mji wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia wakamkuta huyo aliyewahi kuwa sultani wa siku 3 wakampeleka kifungoni huko visiwa vya Shelisheli na baadaye Morisi.

Baada ya vita kwisha aliruhusiwa kurudi Afrika ya Mashariki.

Aliaga dunia mjini Mombasa mwaka 1926.

                                     
  • 1888 1890 Ali bin Said 1890 1893 Hamad bin Thuwaini 1893 1896 Khalid bin Barghash 1896 Hamud bin Muhammed 1896 1902 Ali bin Hamud 1902 1911
  • mtoto wa Turki bin Said, aliyekuwa sultani wa Maskati. Hamad alifariki ghafla ikisemekana alipewa sumu na binamu yake Khalid bin Barghash ambaye alijitangaza
  • kijana Seyyyid Khalid bin Barghash alifika kwenye Jumba la Sultani akajitangaza kuwa sultani mpya. Alitambuliwa na kikosi cha askari wa ulinzi na sehemu

Users also searched:

...
...
...