Back

ⓘ John Garang. Dkt John Garang de Mabior alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan na kiongozi wa zamani wa waasi wa Sudan Peoples Liberation Army. ..
John Garang
                                     

ⓘ John Garang

Dkt John Garang de Mabior alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan na kiongozi wa zamani wa waasi wa Sudan Peoples Liberation Army.

                                     

1. Miaka ya Awali

Kutoka kabila la Dinka Garang alizaliwa katika familia maskini katika kijiji cha Wanglei huko Bor, Sudan, katika ukanda wa upper Nile ya Sudan kwa sasa Jonglei State. Kwa kuachwa yatima akiwa na umri wa miaka kumi, alilipiwa karo ya shule na mmoja wa jamaa zake, na kwenda shule Wau na kisha Rumbek. Mwaka wa 1962 alijiunga na vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe Sudan lakini kwa sababu alikuwa mchanga sana, viongozi walimshauri yeye na wenzake kutafutilia elimu. Kwa sababu ya mapigano yaliyokuwa yakiendelea, Garang alilazimishwa kuhudhuria elimu yake ya Sekondari nchini Tanzania. Baada ya kushinda udhamini, aliendelea na kuweza kupata shahada ya BA katika uchumi mwaka wa 1969 kutoka Grinnell College, Iowa, USA. Huko alijulikana sana kwa kupenda vitabu kwake. Alipewa udhamini mwingine kufanyaa masomo hitimu katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley, lakini akachagua kurudi Tanzania na kusomea Uchumi wa kilimo katika Afrika Mashariki kama Thomas J. Watson Fellow katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM. Akiwa UDSM, alikuwa mwanachama wa University Students African Revolutionary Front. Hata hivyo, punde Garang aliamua kurejea Sudan na kujiunga na waasi. Kuna ripoti nyingi za makosa zinazodai kwamba Garang alikutana na kufanya urafiki na Yoweri Museveni, rais wa baadaye wa Uganda, wakati huu; ingawaje Garang na Museveni walikuwa wanafunzi wa UDSM katika miaka ya 1960, hawakuhudhuria wakati mmoja.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilimalizika baada ya Mkataba wa Addis Ababa wa 1972 na Garang, kama waasi wengine, aliwekwa katika jeshi la Sudan. Kwa miaka kumi na moja, alifanya kazi kama askari na kupanda kutoka safu ya Kapteni hadi Kanali baada ya kufanya Infantry Officers Advanced Course katika Fort Benning, Georgia. Katika kipindi hiki alichukua ruhusa ya kimasomo ya miaka minne na akapata Shahada ya Masters katika Uchumi wa Kilimo na Ph.D. katika uchumi kutoka Iowa State University, baada ya kuandika Thesis juu ya maendeleo ya kilimo ya Sudan Kusini. Kufikia 1983, Knl Garang alikuwa akitumika kama mwalimu mwandamizi katika Shule ya jeshi iliyokuwa Wadi Sayedna kilomita 21 kutoka kitovu cha Omdurman ambapo aliwaelekeza makadeti kwa zaidi ya miaka 4 na baadaye yeye akateuliwa kutumika katika idara ya kijeshi katika idara ya utafiti wa kijeshi katika Makao Makuu ya Jeshi mjini Khartoum.

                                     

2. Kiongozi wa waasi

Mwaka wa 1983, Garang alikwenda Bor, kwa minajili ya kupatanisha askari wa serikali ya kusini wapatao 500 katika Battalion 105 ambao walikuwa wakipinga kuwekwa doria katika vituo vya kaskazini. Hata hivyo, Garang tayari alikuwa mmoja wa baadhi ya maafisa waliokuwa na njama katika amri ya Kusini kwa ajili ya kupanga kuhama Battalion 105 na kuunga mkono waasi waliopinga serikali. Wakati serikali iliposhambulia Bor mwezi wa Mei, Battalion ilijitoa nje, Garang akaenda kwa njia nyingine na kujiunga nao katika ngome ya waasi nchini Ethiopia. Kufikia mwisho wa Julai, Garang alileta askari waasi zaidi ya 3000 chini ya utawala wake kupitia vuguvugu mpya la Sudan Peoples Liberation Army / Movement SPLA / M, ambalo lilikuwa linapinga utawala wa kijeshi na kutwaliwa kwa sehemu kubwa ya nchi na Uislamu, na kuzihimiza ngome nyingine za jeshi kuasi dhidi ya sheria ya Kiislamu juu ya nchi na serikali. Hatua hii ilikuwa ndio mwanzo unaokubaliana wa Vita Kuu vya Pili vya weneyewe kwa wenyewe vya Sudan, ambavyo vilisababisha vifo milioni mmoja na nusu katika kipindi cha miaka ishirini ya migogoro. Ingawa Garang alikuwa Mkristo na eneo kubwa la kusini mwa Sudan sio la Waislamu wengii ni animist, mwanzoni hakuzingatia masuala ya kidini ya vita.

SPLA ilipata msaada wa Libya, Uganda na Ethiopia. Garang na jeshi lake walidhibiti sehemu kubwa ya mikoa ya kusini mwa nchi, iliyoitwa Sudan Mpya. Yeye alidai kuwa ujasiri wa askari wake kutoka kwa "uthibitisho kwamba sisi tunapambana vita vya haki. Hilo ni jambo ambalo Sudan Kaskazini na watu wake hawana. Wakosoaji walipendekeza motisha za fedha kwa uasi wake, wakibainisha kuwa kiasi kikubwa cha mafuta ya Sudan kiko katika kusini mwa nchi.

Garang alikataa kushiriki katika serikali ya mpito mwaka wa 1985 au uchaguzi wa 1986, na kubaki akiwa kiongozi wa waasi. Hata hivyo, SPLA na serikali zilitia saini mkataba wa amani tarehe 9 Januari 2005 mjini Nairobi, Kenya. Tarehe 9 Julai 2005, aliapishwa kama makamu wa rais, cheo cha pili kwa ukuu katika nchi, kufuatia sherehe ambapo yeye na Rais Omar al-Bashir walitia saini katiba ya kugawana madaraka. Yeye pia alikuwa kiongozi wa utawala wa kusini mwa Sudan yenye uhuru mdogo kwa miaka sita kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni ya uwezekano wa Kuganywa. Hakuna Mkristo au mtu kutoka kusini aliwahi kushikilia cheo cha juu kama hicho serikalini. Akizungumza baada ya sherehe, Garang alisema, "Mimi nawapongeza watu wa Sudan, hii si amani yangu au amani ya al-Bashir, ni amani ya watu wa Sudan."

Kama kiongozi, sifa za kidemokrasia za John Garang zilitiliwa mashaka mara nyingi. Kwa mfano, kulingana na Gill Lusk "John Garang hakuvumilia upinzani na mtu yeyote aliyehitilafiana naye aidha alifungwa jela au kuuawa". Chini ya uongozi wake, SPLA ilishutumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

Itikadi za SPLA zilikuwa za uvuli kama Bw Garang mwenyewe. Aligeuka kutoka kwa mrengo wa Marxism hadi kupata msaada kutoka kwa Wakristo wenye siasa kali kutoka Marekani.

Idara ya Taifa ya Marekani ilisema kuwa kuwepo kwa Garang katika serikali kungesaidia kutatua Mgogoro wa Darfur magharibi mwa Sudan, lakini wengine waliona madai haya kuwa "matumaini kupita kiasi".

                                     

3. Kifo

Mwishoni mwa Julai 2005, Garang alikufa baada ya ndege ya rais wa Uganda aina ya helikopta Mi-172 aliyokuwa akisafiria kuanguka. Alikuwa anarudi kutoka mkutano wa Rwakitura na mshirika wake wa muda mrefu Rais Yoweri Museveni wa Uganda. Hakuiambia serikali ya Sudan kwamba alikuwa anaenda mkutano huu na hivyo basi hakuchukua ndege ya rais. Shirika la televisheni la kitaifa kwanza lilisema kuwa ndege iliyombeba Garang ilikuwa imetua salama, lakini Abdel Basset Sabdarat, Waziri wa Habari wa nchi, alikwenda kwenye televisheni masaa kadhaa baadaye kukataa ripoti hiyo. Kwa kweli, ilikuwa ni Yasir Arman, msemaji wa SPLA / M ndiye aliiambia serikali kuwa ndege iliyombeba Garang iliwasili salama ili kuokoa muda kwa ajili ya mipangilio ya ndani katika SPLA kabla ya kifo chake kujulikana.Ndege ya Garang ilianguka siku ya Ijumaa na hivyo ilibakia kuwa iliyotoweka hadi Jumamosi iliyofuata na wakati huu wote serikali ilidhani bado alikuwa Sudan Kusini. Mapema baadaye, taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa Sudan Omar el-Bashir alithibitisha kuwa helikopta ya rais wa Uganda ilianguka katika "mojawapo ya mlima iliyoko kusini mwa Sudan kwa sababu ya kutoona vizuri na kusababisha kifo cha Dkt John Garang De Mabior, wenzake sita na wafanyikazi saba wa ndege hiyo ya Uganda." Migogoro pia iliripotiwa katika maeneo mengine ya nchi. Viongozi wakuu wa SPLM, pamoja na Halifa wa Garang Salva Kiir Mayardit, walisema kwamba mchakato wa kutafuta amani ungeendelea. Wachambuzi walipendekeza kwamba kifo kingeleta aidha demokrasia mpya ya uwazi katika SPLA, ambayo baadhi ya watu walikosoa kwa kuongozwa sana na Garang, au kuzuka kwa vita vya wazi kati ya makundi mbalimbali ya kusini yaliyokuwa yameletwa pamoja na Garang.                                     

4. Viungo vya nje

 • NPR Weekend Edition: John Garang: A Conversation on Sudan
 • Return of Sudanese survivor Archived Aprili 7, 2011 at the Wayback Machine., makala ya maoni katika The Daily Star, Lebanon 19 Julai 2005 - habari juu ya maisha yake ya awali
 • Sudan ex-rebel joins government, BBC, 9 Julai 2005
 • Obituary, BBC
 • Uganda joins Sudan in Investigating Garangs Death, William Eagle, Sauti ya Amerika, 9 Agosti 2005
 • Deadly riots erupt in Sudan after Garang death Archived Septemba 10, 2005 at the Wayback Machine., Reuters, 1 Agosti 2005
 • Tovuti rasmi ya Sudan Peoples Liberation Army
 • A State Department archive of information before Januari 2001
                                     
 • 1994 - 2000 mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 2008 1945 - John Garang Rais wa kwanza wa Sudan Kusini 1953 - Filbert Bayi, mwanariadha kutoka
 • Baada ya kipindi cha amani, vita vilianza upya mwaka 1983 wakati kanali John Garang alipounda SPLA dhidi ya badiliko la Sudan kutangazwa nchi ya Kiislamu
 • Otto von Bismarck, Chansella wa Dola la Ujerumani 1862 - 1890 2005 - John Garang Rais wa kwanza wa Sudan Kusini 2007 - Ingmar Bergman, mwongozaji wa
 • Simon mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi, mwaka wa 1985 30 Julai - John Garang Rais wa kwanza wa Sudan Kusini 16 Agosti - Frere Roger Roger Schutz
 • utangazaji mjadala wa sababu ya kifo cha makamu wa rais wa Sudan John Garang Garang aliuawa wakati helikopta ya rais wa Uganda ilianguka katika eneo
 • Baada ya kipindi cha amani, vita vilianza upya mwaka 1983 wakati kanali John Garang alipounda SPLA dhidi ya badiliko la Sudan kutangazwa nchi ya Kiislamu
 • Tanzania 22 Juni - Juma Athumani Kapuya, mwanasiasa wa Tanzania 23 Juni - John Garang Rais wa kwanza wa Sudan Kusini 30 Julai - Patrick Modiano, mwandishi
 • katika serikali mpya. Baada ya kifo cha kiongozi wa Sudan ya Kusini John Garang katika ajali ya ndege palitokea ghasia kali mwanzo wa Agosti 2005. Tangu
 • Uganda Laurent Kabila, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo John Garang Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Joseph Obgeb Jimmy, mwanadiplomasia
 • Aliyekuwa makamu wa Rais John Garang ambaye awali aliongoza wanamgambo wa Sudan Kusini kupigania uhuru wa majimbo ya kusini.

Users also searched:

...
...
...