Back

ⓘ Ignas wa Antiokia alizaliwa kati ya miaka 35 na 50 B.K. akafa kati ya 98 na 117. Ni kati ya Mababu wa Kanisa wa kwanza, akiwa askofu wa tatu wa Antiokia na mwan ..
Ignas wa Antiokia
                                     

ⓘ Ignas wa Antiokia

Ignas wa Antiokia alizaliwa kati ya miaka 35 na 50 B.K. akafa kati ya 98 na 117.

Ni kati ya Mababu wa Kanisa wa kwanza, akiwa askofu wa tatu wa Antiokia na mwanafunzi wa Mitume wa Yesu.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa na Waorthodoksi tarehe 20 Desemba, lakini na Wakatoliki, Waanglikana na Waorthodoksi wa Mashariki kwenye 17 Oktoba.

                                     

1. Maandishi yake

Akielekea kifodini chake huko Roma, aliandika barua kadhaa kwa makanisa na kwa Polikarp Mtakatifu ambazo 7 za hakika zimetunzwa kama kielelezo cha teolojia ya awali ya Ukristo. Humo kwa mara ya kwanza tunasoma juu ya Kanisa Katoliki ambalo linaitwa hivi kwa kulitofautisha na makundi ya Wakristo waliotengana nalo.

Kati ya mada muhimu zaidi kuna Kanisa, sakramenti na nafasi ya askofu pekee katika kila jimbo.

Barua zake zimetafsiriwa kwa Kiswahili na kutolewa Italia kama ifuatavyo: MT. IGNASI WA ANTIOKIA, Nyaraka - tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna 1992 – ISBN 88-307-0404-0

                                     

2. Viungo vya nje

 • Catholic Encyclopedia: Spurious Epistles of St. Ignatius of Antioch
 • Opera Omnia by Migne Patrologia Graeca with analytical indexes
 • The Short Syriac Version
 • The Ecclesiology of St. Ignatius of Antioch by Fr. John S. Romanides
 • : On-line texts of St. Ignatius letters archived" non-archived linkArchived Januari 21, 2008 at the Wayback Machine.
 • Catholic Encyclopedia: St. Ignatius of Antioch
 • Holy Letters and Syllables, the function and character of Scripture Authority in the writings of St Ignatius Archived Septemba 22, 2009 at the Wayback Machine.
 • Saint Ignatius
                                     
 • na Patriarki wa mji huo kama Ignas wa Antiokia mwanzoni mwa karne ya 2 lakini, baada ya farakano la mwaka 451 lililofuata Mtaguso wa Kalsedonia, ilitafsiriwa
 • huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Ignas wa Antiokia Nabii Hosea, Rufo na Zosimo, Wafiadini wa Voli, Yohane wa Asyut, Fiorenso wa Orange, Richadi Gwyn, Isidori
 • Kaisari Marko Aurelio Ignas wa Antiokia askofu na mfiadini Yustino mfiadini, mwanafalsafa Polikarpo, askofu na mfiadini Irenei wa Lyon, askofu na mwanateolojia
 • Wakristo wengi wa wakati ule hata mjini Roma. Pamoja na maandiko mengine kama vile Didake, Waraka wa Barnaba na nyaraka saba za Ignas wa Antiokia iko katika
 • Teodora, akitawala kwa niaba ya mtoto Mikaeli III wa Bisanti alilazimisha nafasi yake ishikwe na Ignas I 847 - 858 mmonaki mwenye msimamo mkali, ambaye
 • za watakatifu Apolinari wa Ravenna, Elia, Yosefu Barsaba, Marina wa Antiokia Frumensyo, Aurelius wa Karthago, Vulmari, Paulo wa Cordoba, Magdalena Yi Yong - hui
 • Barua zilizoandikwa na Ignas wa Antiokia kwa Wakristo wenzake wa sehemu mbalimbali mwaka 106 hivi ni ushahidi wa awali wa matumizi ya neno Kanisa Katoliki
 • ufafanuzi wa Pseudo - Dionysius, George Pachymeres karne ya 14 ufafanuzi wa Pseudo - Dionysius PG 5: Ignas wa Antiokia Polikarpo, Melito wa Sardi, Papias wa Hierapoli

Users also searched:

...
...
...