Back

ⓘ Jangwa ni eneo kavu lenye mvua au usimbishaji kidogo tu. Kutokana na ukavu kuna mimea michache tu, pia wanyama wachache. Wanyama walioko hufanya shughuli zao ha ..
Jangwa
                                     

ⓘ Jangwa

Jangwa ni eneo kavu lenye mvua au usimbishaji kidogo tu. Kutokana na ukavu kuna mimea michache tu, pia wanyama wachache. Wanyama walioko hufanya shughuli zao hasa wakati wa usiku. Kipimo cha usimbishaji kinachotambulika kimataifa ni kiwango cha chini ya mm 250 kwa mwaka. Uoto wa mimea hufunika chini ya asilimia 5 za eneo lake.

Wakati mwingine huitwa jangwa hata maeneo ambayo ni makavu kutokana na baridi kali.

                                     

1. Aina za maeneo makavu: jangwa na mibuga

Maeneo makavu yanaweza kutofautishwa kuwa yabisi sana en: extremely arid pasipo usimbishaji kwa muda wa miezi 12 mfululizo maana yake hakuna mvua kila mwaka, yabisi en: arid pasipo usimbishaji zaidi ya mm 250 kwa mwaka, nusu yabisi en:semiarid penye usimbishaji kati ya mm 250 and 500 kwa mwaka. Maeneo yabisi sana na maeneo yabisi ni jangwa. Maeneo nusu yabisi yenye nyasi huitwa mbuga.

Takriban theluthi moja ya uso wa nchi kavu duniani ni yabisi sana, yabisi au nusu yabisi.

                                     

1.1. Aina za maeneo makavu: jangwa na mibuga Athari ya uvukizaji

Kiasi cha usimbishaji peke yake hakitoshi kila mahali kutofautisha maeneo makavu. Mm 200 za mvua katika eneo la joto zitasababisha eneo kuonekana kama jangwa kabisa kwa sababu kiasi kikubwa cha maji yale kidogo yanayoneshewa hupotea kutokana na uvukizaji. Kuna mifano ya kwamba eneo penye kiasi kilekile cha 200 mm halionekani kuwa jangwa tayari kwa sababu kutokana na halijoto na mawingu hata yasiponyesha mvua kiasi kidogo cha maji yanavukiza.

Kama uvukizaji unapita kiasi cha mvua hata eneo penye mvua zaidi ya 250 mm inaonekana kama jangwa.

                                     

1.2. Aina za maeneo makavu: jangwa na mibuga Aina za jangwa

Mara nyingi majangwa hutofautishwa kutokana na uso wake:

 • Jangwa la mchanga - uso lake huonyesha hasa mchanga. Mchanga umetokea kutokana na mmomonyoko wa changarawe na kokoto kama mawe haya ni hasa ya shondo. Punje ndogo za mchanga husukumwa na upepo na kutokea kama matuta makubwa ya mchanga. Jangwa la mchanga ni mahali pagumu mno kwa maisha ya kila aina. Mfano bora ni jangwa la Rub al-Khali katika Uarabuni Saudi. Sahara ina pia sehemu za jangwa la mchanga.
 • Jangwa la mawe - uso lake huonyesha miamba na mawe makubwa. Maana yake hapo udongo wote mwenye rutba na mchanga vimeshapulizwa mbali na mwamba umebaki. Athira za joto na baridi zinaweza kupasua mwamba. Mmomonyoko wa upepo hutokea.
 • Jangwa la chumvi - mara nyingi penye beseni yabisi za mashapo bila njia ambako maji ya mvua au mto yanaweza kutoka. Maji yote huvukiza na kuacha chumvi yake katika udongo. Kiasi cha chumvi kinaendelea kuongezeka polepole katika udongo wa beseni hizi.
 • Jangwa la changarawe - uso lake huonyesha hasa changarawe. Changarawe imetokea kutokana na mmomonyoko wa mawe au miamba - punje ndogo zaidi zimeshapulizwa mbali na upepo. Hii ni sababu ya majangwa mengi kuwa na maeneo ya mchanga na changarawe yanayobadilishana. Changarawe hupatikana pia pale ambako zamani barafuto zilisaga mawe na kuzisukuma mbele ya barafu zao pale zilizobaki. Ni ajabu kutafakari ya kwamba sehemu fulani ilikuwa ya barafuto tukisimama leo mahali penye joto kali lakini mabadiliko ya hali ya hewa yalileta baridi au joto kila sehemu ya dunia yetu katika mamilioni ya miaka iliyopita.


                                     

2.1. Maji Maji ya chini

Mara nyingi kuna maji chini ya ardhi. Pale ambako maji haya si chini mno mimea inaweza kuyafikia kwa mizizi yao. Mahali kadhaa chemchemi hutokea. Sehemu kama hizi zinaonekana kama oasisi penye miti, wakati mwingine hata na bwawa. Mahali pengine wakazi wa jangwa wamechimba kisima kirefu pasipo na mimea kinachosaidia maji ya watu na wanyama hasa wa misafara.

                                     

2.2. Maji Maji ya mvua

Mvua ikionyesha unaweza kutokea kwa wingi. Maji yake hukusanyika katika mabonde na kutokea kama mto wa muda. Kuna mifano mingi ya wasafiri jangwani waliokufa kwa sababu walipiga kambi katika bonde penye kivuli lakini walizama kwa sababu mto mkali ulijitokeza kwa ghafla kutokana na mvua ulionyesha katika umbali mkubwa.

Sehemu nyingine mvua husababisha kutokea kwa mbwawa hata maziwa kwa muda.

                                     

2.3. Maji Mito inayopita jangwa

Mito kadhaa kama Nile ina maji ya kutosha ili ivuke neo la jangwa. Inawezesha maisha ya mimea, wanyama na watu katika mabonde yao.

Mito mingine inakwisha jangwani kwa sababu maji yote hupotea na kuvukiza. Mfano wake ni delta ya mto wa Okavango unaokwisha katika jangwa la Kalahari huko Botswana. Delta hii ni eneo la mimea na wanyama wengi katikati ya jangwa.

Mto wa Ewaso Nyiro katika Kenya ya kaskazini kwa kawaida hukwisha katika nchi yabisi za Usamburu. Lakini kila baada ya miaka makumi kadhaa baada ya mvua kubwa sana inaendelea kuvuka jangwa la Somalia ya kusini na kufikia Bahari Hindi jinsi ilvyotokea wakati wa El-Nino 1998.

                                     
 • kaskazini kwenye bara la Afrika. Kwa kwaida nchi za Afrika kaskazini ya jangwa Sahara huhesabiwa kuwa Afrika ya Kaskazini. Kanda la Afrika ya Kakazini
 • 2006 wanaokalia eneo la 295, 254 km² ambalo sehemu kubwa ni milima na jangwa Mji mkuu na mji mukubwa jimboni ni Phoenix. Imepakana na Utah, New Mexico
 • 900 2008 wanaokalia katika eneo la 135, 765 km² ambalo ni hasa milima na jangwa Orodha ya miji ya Alabama Wikimedia Commons ina media kuhusu: Alabama State
 • unakwisha kwenye delta yake katika jangwa la Kalahari Botswana Delta hii ni eneo lenye mimea na wanyama wengi katikati ya jangwa kubwa. Delta inavuta watalii
 • mvua kinachopatikana. Tabia kuu ya savana ni uhaba wa maji. Tofauti na jangwa maji yapo ingawa kidogo. Kiwango cha kawaida cha mvua ni kati ya milimita
 • Sahara ni eneo lote la bara la Afrika ambalo liko upande wa kusini wa Jangwa la Sahara. Kulingana na Umoja wa Mataifa, eneo hili linajumuisha nchi zote
 • pia feri ya moja kwa moja kati ya Botswana na Zambia kuvukia mto Zambezi. Jangwa la Kalahari linafunika theluthi mbili za eneo la Botswana. Moja ya maeneo
 • 220, 939 2008 wanaokalia eneo la 225, 365 km² ambalo ni hasa milima na jangwa State of Minnesota Official Website Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 • 410, 796 2008 wanaokalia eneo la 135, 382 km² ambalo ni hasa milima na jangwa State of Louisiana Official Website Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Users also searched:

...
...
...