Back

ⓘ Invincible, albamu ya Michael Jackson. Invincible ni jina la kutaja albamu ya kumi ya mwimbaji, mwanamuziki, mtayarishaji wa rekodi, mfanyabishara, na mhisani w ..
Invincible (albamu ya Michael Jackson)
                                     

ⓘ Invincible (albamu ya Michael Jackson)

Invincible ni jina la kutaja albamu ya kumi ya mwimbaji, mwanamuziki, mtayarishaji wa rekodi, mfanyabishara, na mhisani wa Kimarekani, Michael Jackson. Albamu ilitolewa na studio ya Epic Records mnamo tar. 30 Oktoba 2001, miaka sita tangu kutolewa kwa albamu yake ya 1995 yenye matoleo mawili kwa pamoja, HIStory. Albamu hii imeingiza nyimbo mpya tu tangu kutolewa kwa albamu ya Dangerous mnamo mwaka wa 1991. Kasha la aalbamu, lina picha ya sura ya Jackson, inapatika katika rangi tano tofauti - nyekundu, kijani, chungwa, buluu na fedha. Hadi leo, albamu imekadiriwa kuuza kati ya nakala milioni 8 - 12 kwa hesabu ya dunia nzima.

                                     

1. Matayarisho

Albamu imekuwa ya kwanza kutoa nyimbo zoote mpya tangu kutolewa kwa albamu ya Dangerous ya mwaka wa 1991. Katika upande wa utayarishaji ulishikiriwa na wasanii kadhaa kama vile Rodney Jerkins, R. Kelly na mwanachama wa zamani wa kundi la muziki wa R&B la Jodeci, DeVante Swing. Mtayarishaji wa hip hop Dr. Dre naye aliombwa atayarishe albamu, lakini alikataa.

                                     

2. Vyanzo zaidi

  • George, Nelson 2004. Michael Jackson: The Ultimate Collection booklet. Sony BMG.
  • Taraborrelli, J. Randy 2004. The Magic and the Madness. Terra Alta, WV: Headline. ISBN 0-330-42005-4.
                                     
  • Jackson alisema kwamba huu ndiyo wimbo wake kipenzi kutoka katika albamu ya Invincible Wimbo hasa ulitungwa kunako mwaka wa 1997 wakati huo Ambrosius yupo
  • Cry ni wimbo kutoka katika albamu ya Michael Jackson ya mwaka wa 2001, Invincible wimbo umetungwa na mwimbaji wa R&B na mtunzi, R. Kelly, ambaye ndiye
  • Diskografia ya albamu za Michael Jackson Visionary: The Video Singles Billboard magazine. Billboard charts. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008 - 02 - 02.
  • 1995 Invincible 2001 Afya na mwonekano wa Michael Jackson film.com: Michael Jackson A Fashion Retrospective, 29. Novemba 2009 Michael Jackson album
  • kutoka nchini Marekani, Michael Jackson Hii ilikuwa single yake ya kwanza kutoka katika albamu yake ya mwaka wa 2001, Invincible Wimbo umeshika 10 kwenye
  • Michael Jackson Albamu imetengeneza maremixi kadhaa kutoka katika albamu yake iliyopita ya HIStory, na nyimbo zingine tano ambazo ni mpya. Jackson alijikita

Users also searched:

...
...
...