Back

ⓘ Kanisa la Wamaroni ni moja ya Makanisa Katoliki ya Mashariki, yaani ni Kanisa linalojitegemea kisheria ndani ya umoja wa Kanisa Katoliki. ..
Kanisa la Wamaroni
                                     

ⓘ Kanisa la Wamaroni

Kanisa la Wamaroni ni moja ya Makanisa Katoliki ya Mashariki, yaani ni Kanisa linalojitegemea kisheria ndani ya umoja wa Kanisa Katoliki.

                                     

1. Historia

Mzizi wake ni katika Kanisa la Kisirya la Kiorthodoksi kwenye nchi za Syria na Lebanoni za leo, kwa hiyo katika utamaduni wa Wakristo waliotumia lugha ya Kiaramu cha magharibi.

Kanisa hilo lilianza katika mvutano juu ya maamuzi ya Mtaguso wa Kalsedonia wa mwaka 451 yaliyokataliwa na Wasirya wengi. Wafuasi wa mmonaki Maroni, mwanzilishi wa monasteri maarufu katika karne ya 4, walisimama upande wa maazimio ya huo mtaguso mkuu ingawa walikuwa Wasirya. Kwa hiyo Wamaroni waliteswa na wenzao wakawa kundi la Wasirya waliosimama upande wa Kanisa la Kigiriki la Kiorthodoksi.

Katika mabishano yaliyofuata ndani ya Kanisa la Kigiriki Wamaroni waliamua kukaa kando, wakawa jumuiya ya pekee na kutafuta hifadhi yao kwenye milima ya Lebanoni.

Wakati wa vita vya msalaba Wamaroni walielewana vizuri na Wakatoliki kutoka Ulaya wakatafuta ushirikiano nao. Hapo walikubali uongozi wa Papa wa Roma na kuwa hadi leo Kanisa pekee la Ukristo wa Mashariki lililopo lote chini ya Papa.

                                     

2. Hali ya leo

Wamaroni wanatunza liturujia, teolojia na maisha ya kiroho ya mazingira hayo kulingana na tapo lililoanzishwa na Maroni. Hadi leo sehemu za liturujia ziko kwenye lugha ya Kisirya au Kiaramu cha magharibi lakini kwa jumla Kanisa na pia jumuiya ya Wakristo wake hutumia Kiarabu.

Patriarki wake anachaguliwa na Sinodi ya maaskofu wa Kanisa hilo, halafu anamuomba Papa wa Roma ushirika kamili. Anaishi Bkerke Lebanoni, ambapo ana jimbo lake, ingawa anatumia bado jina rasmi la Patriarki wa Antiokia.

Kanisa hilo linakubali kuwapa upadri waamini waliokwishaoa.

                                     

3. Uenezi

Huko Lebanoni, ni kundi kubwa, ingawa wanazidi kupungua kwa sababu ya matatizo yanayowafanya wengi kuhamia nchi nyingine.

Wanakaribia kuwa 3.500.000 duniani kote, wakiishi katika majimbo 28 kama yafuatavyo.

Huko Lebanoni: Zahleh, Tiro, Tripoli, Sidoni, Joubbeh - Sarba - Jounieh jimbo la Patriarki, Jbeil - Byblos, Beirut, Batrun, Baalbeck - Deir el Ahmar na Antelias

Huko Syria: Latakia, Damascus na Aleppo.

Huko Israel: Haifa - Nchi Takatifu.

Katika nchi nyingine: Afrika Magharibi na ya Kati Ibadan, Nigeria, Brooklyn Marekani, Buenos Aires Argentina, Cairo Misri, Cyprus, Kolombia, Los Angeles Marekani, Mexico, Montreal Canada, Paris Ufaransa, Sao Paulo Brazil, Sudan na Sydney Australia.

                                     

4. Marejeo

 • Maronite Church. New Catholic Encyclopedia, Second Edition, 2003.
 • Moosa, Matti, The Maronites in History, Gorgias Press, Piscataway, NJ, 2005, ISBN 978-1-59333-182-5
 • R. J. Mouawad, Les Maronites. Chrétiens du Liban, Brepols Publishers, Turnhout, 2009, ISBN 978-2-503-53041-3
 • Kamal Salibi - A House of Many Mansions - The History of Lebanon Reconsidered University of California Press, 1990.
 • Riley-Smith, Johnathan - The Oxford Illustrated History of the Crusades
                                     

5. Viungo vya nje

 • Hati Orientalium Ecclesiarum ya Mtaguso wa pili wa Vatikano
 • Ujuzi wa msingi kuhusu Makanisa hayo
 • The Maronite Monks of Adoration, Most Holy Trinity Monastery Archived Novemba 7, 2008 at the Wayback Machine. - monastery in Massachusetts
 • Maronite Rite diocese based in Sydney, Australia
 • Catholic Culture: News - Maronite population discussed
 • Orientale Lumen - Hati ya Papa Yohane Paulo II kuhusu Makanisa ya Mashariki
 • CNEWA Idara ya Papa inayosaidia Makanisa hayo
 • Instruction for Applying the Liturgical Prescriptions of the Code of Canons of the Eastern Churches Archived Aprili 25, 2009 at the Wayback Machine. - Hati ya Idara ya Papa kwa Makanisa ya Mashariki kuhusu liturujia
 • Maronite History Project - a Maronite encyclopedia wiki
 • The Druzes and the Maronites under the Turkish Rule from 1840 to 1860 Cornell University Library Historical Monographs Collection.
 • Orodha ya majimbo ya Kanisa la Wamaroni
 • Hati Orientales omnes Ecclesias ya Papa Pius XII
 • Eparchy of Saint Maron of Brooklyn
 • Eparchy of Our Lady of Lebanon
 • Takwimu za Makanisa Katoliki ya Mashariki
 • Codex Canonum Ecclesiarum Orientalium - Mkusanyo wa Sheria za Makanisa ya Mashariki katika Kilatini pamoja na sehemu sambamba
 • Sura ya Idara ya Papa kwa Makanisa hayo
 • Congregation of the Lebanese Maronites Missionnaries
 • Tovuti rasmi ya Kanisa la Wamaroni


                                     
 • historia yao, ni imani ya Kikristo katika Kanisa la Wamaroni ambalo lina ushirika kamili na Papa wa Roma na Kanisa Katoliki lote duniani, ingawa linafuata
 • Sirmaniyah au Sarmin nchini Syria, 628 Kfarhy, Lebanon, 707 aliongoza Kanisa la Wamaroni kama Patriarki wake wa kwanza. Baada ya kuwa mmonaki wa monasteri
 • Chanzo cha Wakatoliki wa Mashariki ni tofauti: baadhi hasa wale wa Kanisa la Wamaroni wanadai kuwa wamedumu tangu mwanzo katika ushirika kamili na Papa
 • wa tapo la kiroho lenye jina lake ambalo lilizaa nchini Lebanon Kanisa la Wamaroni lililomo katika ushirika kamili na Kanisa la Roma na Kanisa Katoliki
 • Bekaa Kafra katika nchi ya Lebanon kaskazini mpaka akawa mmonaki wa Kanisa la Wamaroni halafu pia padri. Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 5
 • Jrebta, 23 Machi 1914 alikuwa mwanamke mmonaki wa Kanisa la Wamaroni nchini Lebanon. Baada ya kujiunga la masista walimu alichukua nafasi ya kujifungia monasterini
 • yakiwa pamoja na Kanisa Katoliki la Kisiria na Kanisa Katoliki la Kimalankara. Kwa kiasi kikubwa liturujia hiyo ni pia ya Kanisa la Wamaroni Liturujia hiyo

Users also searched:

...
...
...