Back

ⓘ Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo au Kongo-Kinshasa ni nchi iliyoko Afrika ya Kati; kwa ukubwa wa eneo ni ya pili barani Afrika. Ni tofauti na nchi jirani ya Jam ..
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
                                     

ⓘ Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo au Kongo-Kinshasa ni nchi iliyoko Afrika ya Kati; kwa ukubwa wa eneo ni ya pili barani Afrika. Ni tofauti na nchi jirani ya Jamhuri ya Kongo.

                                     

1. Jiografia

Nchi imepakana na Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi, Tanzania, Zambia na Angola.

Ina sehemu ndogo ya pwani kwenye Bahari ya Atlantiki. Sehemu hiyo inatenganisha eneo la Cabinda kutoka maeneo mengine ya Jamhuri ya Angola.

Eneo lote ni la kilometa mraba 2.345.409 na linafanya Kongo iwe nchi ya 11 duniani kwa ukubwa wa eneo.

                                     

2.1. Historia Historia ya kale

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani na ya Wabilikimo.

Katika karne za BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Jina la Kongo lahusiana na mto Kongo unaopitia nchi yote.

Mnamo karne ya 15, wakati wapelelezi wa kwanza Wareno walipofika kwenye pwani za Afrika, milki kubwa katika nchi ya Kongo ya magharibi pamoja na Angola ya kaskazini ilikuwa Ufalme wa Kongo. Wakati wa uenezaji mkuu ufalme huu ulianza kwenye mwambao wa Atlantiki na kuendelea hadi mto Kwango kwenye mashariki, halafu maeneo kutoka Pointe-Noire leo: Jamhuri ya Kongo, upande wa kaskazini ya Cabinda upande wa kaskazini hadi mto Loje leo: mji wa Ambriz katika kusini.

Mtawala alikuwa na cheo cha Manikongo na ufalme uligawiwa kwa majimbo sita. Baada ya kufika kwa Wareno wafalme na matabaka ya juu walikuwa Wakristo. Ufalme uliporomoka kutokana na vita vilivyosababishwa na biashara ya watumwa na kuingilia kwa wafanyabiashara ya watumwa katika siasa ya ndani. Hata hivyo, nasaba za watawala waliotumia cheo cha "Awenekongo" waliendelea kukaa katika mji mkuu wa kale Mbanza-Kongo iliyobadilishwa jina kuitwa San Salvador hadi mwaka 1914 ambako Wareno walifuta mabaki ya uhuru na kufanya eneo lililobaki sehemu kamili ya koloni lao la Angola.

Upande wa kusini, kuanzia karne ya 17, kulikuwa na ufalme ulioitwa Dola la Kazembe.

                                     

2.2. Historia Koloni binafsi la mfalme kuwa koloni la Ubelgiji

Nchi jinsi ilivyo ilianzishwa kama Dola huru la Kongo likiwa mali binafsi ya mfalme Leopold II wa Ubelgiji. Historia yake ni ya aibu na ya ukatili kupindukia.

Utawala wa mfalme ulionekana kuwa wa kinyama na upinzani dhidi yake ulikua katika nchi nyingi za dunia.

Hatimaye alipaswa kukabidhi koloni lake binafsi mikononi mwa serikali ya Ubelgiji iliyomlipa fidia kwa mali aliyoacha.

Kati ya mwaka 1908 hadi 1960 ilikuwa koloni la Ubelgiji kwa jina la Kongo ya Kibelgiji baada ya kuhamishiwa mikononi mwa serikali ya Ubelgiji.

Katika miaka 1925 hadi 1946 maeneo ya Rwanda na Burundi yalitawaliwa kama sehemu za Kongo ya Kibelgiji.

                                     

2.3. Historia Siasa ya wakoloni

Wabelgiji walijitahidi kuboresha hali ya maisha ya wenyeji baada ya miaka mibaya ya Leopold II. Nia ilichelewa kuonekana hali halisi kwa sababu utaratibu wa kulazimisha Waafrika kufanyia kazi kampuni na shirika kubwa iliendelea hata bila idhini ya serikali mpya ukadai vifo vingi.

Kwenye uwanja wa elimu, matibabu na mawasiliano jitihada za siasa mpya zilionekana zaidi. Kongo ilikuwa kati ya nchi chache ambako lugha za kienyeji zilifundishwa shuleni kwa sababu shule nyingi ziliendshwa na wamisionari.

Kwa upande mwingine ubaguzi wa rangi uliwaruhusu Waafrika wachache sana kufikia ngazi za juu za elimu.

Makampuni makubwa ya migodi kama vile "Société Générale" na "Union Minière du Haut Katanga" yalichimba madini hasa katika jimbo la Katanga. Makampuni haya yalikuwa na athira kubwa.

Katanga ilikuwa maarufu kwa shaba iliyochimbwa huko. halafu pia kwa uranium iliyotumiwa kwa mabomu ya kwanza ya kinyuklia ya Marekani mwaka 1945.                                     

2.4. Historia Upinzani

Baada ya unyama wa miaka ya Leopold II upinzani dhidi ya utawala wa kikoloni ulikuwa hafifu. Kuanzia miaka ya 1920 Wakongo wengi walionyesha upinzani huo katika mahudhurio katika madhehebu mapya ya wafuasi wa Simon Kimbangu yaliyopigwa marufuku na Wabelgiji kuanzia mwaka 1926.

Tangu mwaka 1950 upinzani uliongezeka na kuonyesha pia uso wa kisiasa.

Wabelgiji ambao hawakujiandaa kwa madai hayo yalipaswa kukubali uchaguzi wa halmashauri za vijiji na miji mwaka 1957.

Mwaka 1958 vyama vya kisiasa vilikubaliwa. Harakati mbili muhimu kati ya hivi zilikuwa Abako Alliance de Bakongo chini ya Joseph Kasavubu na MNC Mouvement National Congolais chini ya Patrice Lumumba.

Mwaka 1959 mkutano wa wanasiasa Wakongo ulidai uhuru wa nchi.

                                     

2.5. Historia Mwisho wa koloni na uhuru

Wabelgiji walijaribu kuchelewesha harakati hizo lakini baada ya kutambua matatizo serikali ya Ubelgiji ilitangaza mnamo Januari 1960 kuwa uchaguzi utaendeshwa haraka na baada ya miezi sita Wabelgiji watakabidhi nchi kwa wenyeji.

Chama cha Patrice Lumumba kilishinda kwa kura nyingi naye akawa kiongozi wa kwanza wa nchi huru kama waziri mkuu.

Koloni la Kongo ya Kibelgiji lilipata uhuru tarehe 30 Juni 1960.

Kati ya 27 Oktoba 1971 na 17 Mei 1997, chini ya utawala wa dikteta Mobutu, nchi ilijulikana kwa jina la "Zaire".

Leo hii ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

                                     

3. Watu

Mwaka 2017 wakazi walikuwa 81.339.988: idadi hiyo ni ya 4 kati ya nchi zote za Afrika, baada ya Nigeria, Ethiopia na Misri.

Wakazi asilia ni Wabilikimo, ambao kwa sasa ni 600.000. Kumbe walio wengi ni Wabantu.

                                     

3.1. Watu Lugha

Kifaransa ni lugha rasmi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ilikuwa lugha ya utawala ya koloni ikaendelea kutumiwa kama lugha isiyoelekea upande wowote kati ya makabila, lugha na tamaduni za nchi hii.

Lugha ya Kiholanzi iliyotumiwa na Wabelgiji pamoja na Kifaransa katika utawala haitumiki tena.

Kwa jumla kuna takriban lugha 242, hasa lugha za Kibantu, zinazozungumzwa nchini angalia orodha ya lugha. Kati yake, lugha 4 zinatambuliwa kama lugha za kitaifa, nazo ni: Kikongo Kituba, Kingala Kongo, Kiluba Tshiluba na Kiswahili. Wakati wa ukoloni lugha hizo nne za kitaifa ziliwahi kutumiwa kieneo katika shule za msingi.

Kingala kilikuwa lugha rasmi ya jeshi la kikoloni liloitwa "Force Publique" chini ya utawala wa Ubelgiji likaendelea kuwa lugha ya jeshi la jamhuri baada ya uhuru.

Tangu mapinduzi ya 1997 sehemu za jeshi, hasa mashariki, hutumia pia Kiswahili.

Takriban 47% wanatumia Kifaransa kama lugha ya kwanza au lugha ya pili.                                     

3.2. Watu Dini

Wananchi wengi zaidi ya 90% wanajihesabu Wakristo wa madhehebu mbalimbali; kati yao asilimia 29.7 ni Wakatoliki. Waislamu ni asilimia 10-12. Wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 3%.

                                     

4. Tazama pia

 • Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
 • Demografia ya Afrika
 • Orodha ya miji ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
                                     

5. Marejeo

 • Osman, Mohamed Omer GuudleNovember,2011 Africa: A rich Continent where poorest people live, The Case of DR Congo and the exploitation of the World Market
                                     

6. Viungo vya nje

 • Karen Fung:Democratic Republic of the Congo. Africa South of the Sahara: Selected Internet Resources. Stanford University.
 • The Democratic Republic of Congo from Global Issues
 • Democratic Republic of the Congo Archived Julai 27, 2008 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
 • Uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia baada ya miongo minne
 • Chief of State and Cabinet Members
 • Democratic Republic of the Congo entry at The World Factbook
 • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika Open Directory Project
 • Wikimedia Atlas of Democratic Republic of the Congo
 • Country Profile from the BBC News
                                     
 • Kikele ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Wakele. Mwaka wa 1980 idadi ya wasemaji wa Kikele imehesabiwa kuwa
 • lugha za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kialur Kiamba Kiasoa Kiaushi Kiavokaya Kibabango Kibaka Kibali Kibaloi Kibamwe Kibanda ya Kati Kibanda ya Kusini
 • Kongo Kinshasa ni kifupi cha kutaja nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yenye mji mkuu wa Kinshasa. Jina limeundwa kwa nia ya kuwa na jina fupi
 • wilaya ya Bundibugyo ukitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Unaanza katika ziwa Edward na kuishia katika ziwa Albert. Orodha ya mito ya Uganda Orodha
 • Brazzaville. Jina limeundwa kwa nia ya kuwa na jina fupi tena la kutofautisha na Kongo nyingine yaani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo au Kongo Kinshasa
 • Mkoa wa Katanga ya Juu ni mmojawapo kati ya mikoa 26 ya kujitawala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Idadi ya wakazi wake ni takriban 3, 960, 945. Mji
 • Akanyaru Mto Kongo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mto Lualaba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mto Lukuga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Ziwa Tanganyika
 • Kibanda ya Kati ni lugha ya Kiniger - Kongo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini inayozungumzwa na Wabanda
 • Tanganyika ni moja ya mikoa 26 ya kujitawala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Liko upande wa Mashariki wa nchi likipakana na nchi ya Tanzania na Ziwa
 • Costermansville, Costermansstad ni mji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliopo upande wa kusini magharibi mwa pwani ya Ziwa Kivu na mji mkuu wa mkoa wa Kivu

Users also searched:

...
...
...