Back

ⓘ John Michael Talbot ni mfuasi wa Yesu Kristo, mwimbaji na mpigaji gitaa wa Kimarekani. Ni mwanzilishi wa The Brothers and Sisters of Charity huko Eureka Springs ..
John Michael Talbot
                                     

ⓘ John Michael Talbot

John Michael Talbot ni mfuasi wa Yesu Kristo, mwimbaji na mpigaji gitaa wa Kimarekani. Ni mwanzilishi wa The Brothers and Sisters of Charity huko Eureka Springs, Arkansas.

                                     

1.1. Wasifu Maisha y awali

Alizaliwa katika familia ya Wamethodist wenye historia ya muziki huko mjini Oklahoma City, Oklahoma. Aliamza kujifunza kupiga gitaa akiwa na umri wa miaka 10. Akiwa na umri wa miaka kumi na tano aliacha shule na akawa akifanyakazi kama mpiga gitaa wa Mason Proffit, bendi ya muziki wa rock/asili ilioanzishwa na kaka yake mkubwa, Terry. Bendi ilitoa albamu tano na ilikuwa moja kati ya bendi za muziki wa rock zilizopiga hatua na kupata mafanikio makubwa kama ilivyikubwa bendi ya Eagles

Baada ya kuvutwa karibu na kupata mafanikio, Talbot akajiingiza katika safari ya kiroho ambayo ilimwongoza mpaka katika dini za jadi za Kiamerika, Ubudha hadi Ukristo. Kwa maana hii yeye na ndugu yake wakajiunga katika Jesus Movement, wakarekodi albamu moja ilioitwa Reborn ambayo pia ilitoliewa tena na studio ya Sparrow Recordsalbamu asilia ilitolewa na jina la "The Talbot Bros." katika studio za Warner Brothers.

Baadaye albamu mbili za Talbot zilifuata: John Michael Talbot 1976 na The New Earth 1977. Albamu zote mbili zilitayarishwa na Billy Ray Hearn. Talbot alishawahi kuoa, kisha akaacha, na mkewe ndiye anayemlea binti yake. Baadaye akaamua kijtoa machoni mwa umma. Na kuanza kusoma maisha ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, alikuwa na shauku ya kuanza kusomea masula yake katika chuo cha Franciscan cha mjini Indianapolis.

Akawa Mromani Katoliki, na kujiunga na Secular Franciscan Order mnamo 1978. Baadaye akaanzisha nyumba ya ibada, The Little Portion, na akapanga kuishi maisha ya kujitenga upweke. Baadaye ikatokea kuwa na maombi mengi yaliyokuwa yakiendele ya kiumuziki, Talbot akaendelea kutayarisha muziki wa sauti na gitaa katika staili ya Kiroma.

Alihamia kwenye Nyumba ya Ibada ya mjini Eureka Springs, Arkansas ambayo aliinunua wakati wa siku za Mason Proffit. Alianzisha jumuia yake mwenyewe ilioitwa Brothers and Sisters of Charity katika Little Portion Hermitage. Ni jumuia ambayo imejengwa kwa ajili ya watu aina mbalimbali, ikiwa na madada na makaka ambao hawajaolewa, vilevile na familia kadhaa.

Mnamo mwaka wa 1989, Talbot amemwoa kwa ruhusa ya Kanisa la Katoliki mwanamke mmoja aliyeitwa Viola Pratka, ambaye zamani alikuwa mwa wamoja wa "Incarnate Word Sister" sista:mtawa; Incarnate Word Sister enye oda ya Kikatoliki ambaye alijiunga na jumuia hiyo mnam mwaka wa 1986. Kwa miaka mingi Talbot amesaidia sana shirika la Mercy Corp, shirika ambalo lanasaidia watu pale unapotokea msiba.

Mnamo mwaka wa 2008, Hermatige Kiswahili: Kificho, ni jina la jumuia ilisumbuliwa na tatizo la moto na kupelekea kuharibu maktaba zake na baadhi ya majengo mengine. Jumuia hiyo inaomba msaada kwa Mungu ili waweze kurejesha vile vitu vyote vilivyopotea kwenye ajali hiyo. Talbot ametumia muda wake mwingi sana kwa kwenda kudhuru eneo lile akiwa kama mtoa msaada-mwimbaji kwa ajili ya jumuia hiyo.

                                     

2. Albamu alizotoa

 • Living Water 50th 2007.
 • Come Worship the Lord Vol. 1 1990.
 • No Longer Strangers 1983.
 • Songs For Worship Vol. 1 1982.
 • Quiet Reflections 1987.
 • Cave of the Heart 1999.
 • Table of Plenty 1997.
 • The Lords Supper 1979.
 • The Master Musician 1992.
 • The John Michael Talbot Collection 1995.
 • Spirit Pathways 1998.
 • Reborn 1972.
 • For the Bride 1981.
 • Chant from the Hermitage 1995.
 • Troubadour Years 2008.
 • Wisdom 2001.
 • The New Earth 1977.
 • Songs For Worship Vol. 2 1985.
 • The Birth of Jesus 1990.
 • John Michael Talbot 1976.
 • Hiding Place 1990.
 • Pathways to Wisdom 1998.
 • The God of Life 1984.
 • Our Blessing Cup 1996.
 • The Beautiful City 2006.
 • The Regathering 1988.
 • Meditations in the Spirit 1993.
 • Pathways of the Shepherd 1998.
 • Master Collection 1988.
 • Monk Rock 2005.
 • Quiet Pathways 1998.
 • The Quiet 1985.
 • Come to the Quiet 1980.
 • Brother to Brother 1996.
 • Come Worship the Lord Vol. 2 1990.
 • City of God 2005.
 • The Lover and the Beloved 1989.
 • Meditations from Solitude 1994.
 • Empty Canvas 1986.
 • Pathways to Solitude 1998.
 • Be Exalted 1986.
 • Troubadour for the Lord 1996.
 • Signatures 2003.
 • Beginnings / The Early Years 1980.
 • Troubadour of the Great King 1981.
 • The Talbot Brothers Collection 1995.
 • Light Eternal 1982.
 • The Heart of the Shepherd 1987.
 • The Painter 1980.
 • Simple Heart 2000.
 • Hidden Pathways 1998.
                                     
 • mwandishi wa kike kutoka Uholanzi 18 Machi - John Damiano Komba, mwanasiasa kutoka Tanzania 8 Mei - John Michael Talbot mwimbaji Mkristo kutoka Marekani 22 Mei
 • Robert Horvitz, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 2002 1954 - John Michael Talbot mwimbaji Mkristo kutoka Marekani 1975 - Enrique Iglesias, mwimbaji
 • Nye, Ken Smith, Jean Symons, Ted Walker 1965: John Fuller, Derek Mahon, Michael Longley, Norman Talbot 1966: Robin Fulton, Seamus Heaney, Hugo Williams

Users also searched:

...
...
...