Back

ⓘ Kilwa Kisiwani. Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Kilwa Kilwa Kisiwani ni jina la kijiji kikubwa kwenye Kisiwa cha Kilwa karibu na mji wa Kilwa Masoko ka ..
Kilwa Kisiwani
                                     

ⓘ Kilwa Kisiwani

Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Kilwa

Kilwa Kisiwani ni jina la kijiji kikubwa kwenye Kisiwa cha Kilwa karibu na mji wa Kilwa Masoko katika Mkoa wa Lindi, Tanzania.

Ndipo mahali pa mji wa Kilwa ya kihistoria iliyokuwa mji mkubwa kabisa kati ya miji ya Waswahili katika pwani ya Afrika ya Mashariki wakati wa karne ya 14 hadi karne ya 16 BK.

                                     

1. Mji muhimu zaidi wa Uswahilini

Kuanzia karne ya 11 Kilwa ilikuwa kituo muhimu cha biashara. Kuanzia karne ya 13 na 14 Kilwa ikawa muhimu kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka Dola la Mwene Mtapa Zimbabwe, pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka Bara Hindi na Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.

Katika karne ya 14 - kati ya 1330 na 1340 BK - mji ulitembelewa na msafiri Mwarabu Ibn Battuta aliyeacha taarifa ya kwanza ya kimaandishi kuhusu mji huo.

Majengo makubwa yalijengwa yakiwa magofu yao yamesimama hadi leo kama vile msikiti mkuu, Jumba ya kifalme ya Husuni Kubwa, Boma la Kireno Kilwa na mengine mengi.

                                     

2. Kuja kwa Wareno

Kuja kwa Wareno katika karne ya 16 ilivuruga biashara ya Waswahili. Kilwa ikarudi nyuma. Katika karne ya 18 na ya 19 ikapata upya nguvu ya kiuchumi kutokana na biashara ya watumwa. Mwisho wa biashara hiyo ulimaliza utajiri wa Kilwa.

                                     

3. Kilwa leo

Leo hii Kilwa Kisiwani ipo katika eneo la Tanzania lisilotembelewa kwa urahisi.

Hata hivyo kisiwa ni kati ya Hifadhi za Kiutamaduni muhimu sana za Tanzania, hata imeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" World Heritage.

Katika wilaya hiyo kuna mahali pengine pa urithi wa dunia, Selous.

                                     

4. Marejeo

 • Dunn, Ross E. 2005, The Adventures of Ibn Battuta, University of California Press, ISBN 0-520-24385-4. First published in 1986, ISBN 0-520-05771-6.
 • Chittick, H. Neville 1974, Kilwa: an Islamic trading city on the East African coast 2 Vols, Nairobi: British Institute in Eastern Africa. Volume 1: History and archaeology; Volume 2: The finds.
                                     

5. Viungo vya nje

 • Geonames.org
 • Free resource for tourists on Kilwa
 • World Monuments Fund Project Page for Kilwa
 • Kilwa katika Historia ya Waswahili BBC
 • Kilwa Kisiwani
 • Kilwa Kisiwani Site Page from the Aluka Digital Library
                                     
 • Fyord ya Oslo Norway Vancouver Kanada Kidaka cha Tokyo Japani Kilwa Kisiwani ni mfano wa bandari asilia nzuri ambayo haitumiki tena kwa sababu kina
 • makala ya Pande ya Wilaya ya Muheza, Tanga. Kwa makala ya Pande ya Wilaya ya Kilwa tafadhali fungua Pande Mikoma. Pande ni jina la kata ya Wilaya ya Muheza
 • Bahrain, Cargados Carajos, Visiwa vya Cocos Keeling Diego Garcia, Kilwa Kisiwani Kirimba visiwa Kisiwa cha Mafia, Komori, Kisiwa cha Krismasi, Lamu
 • ya Taifa Ngorongoro. 1981 Hifadhi ya Serengeti. 1981 Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara. 1982 Hifadhi ya Taifa Selous. 1987 Hifadhi ya Taifa
 • kutengeneza meli za kuabiria kusini hadi miji mingine yenye bandari kama Kilwa na Shanga iliyo katika pwani ya Afrika Mashariki. Wafanyabiashara Waarabu
 • Ngorongoro 1987 - Asili - Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro 1981 - Utamaduni - Kilwa Kisiwani 2006 - Utamaduni - Michoro ya Kondoa 1982 - Asili - Selous Game Reserve
 • kutengeneza meli za kuabiria kusini hadi miji mingine yenye bandari kama Kilwa na Shanga iliyo katika pwani ya Afrika Mashariki. Mombasa ulikuwa mji wenye
 • Kilwa Kisiwani mwaka 1572
 • vyanzo vinataja kutekwa kwa wanawake na watoto kando ya visiwa vya Kilwa Kisiwani Madagaska, na Pemba. Imekadiriwa kwamba wafanyabiashara Waarabu walibeba
 • akatembelea bandari za Uswahilini na kufika Bara Hindi. Katika bandari za Kilwa Zanzibar na Mombasa Wareno wakashangaa kukutana tena na Waarabu Waislamu

Users also searched:

...
...
...