Back

ⓘ Jakaya Kikwete. Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, jimbo la uchaguzi la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwa ..
Jakaya Kikwete
                                     

ⓘ Jakaya Kikwete

Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, jimbo la uchaguzi la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.

Lugha ya mama ilikuwa Kikwere.

Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga.

Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.

                                     

1. Masomo

Miaka 1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Kati Middle School Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga.

Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza kwa kupata digrii yake mwaka 1978.

Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.

Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Katika Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. Katika UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.

                                     

2. Kupanda ngazi katika siasa

1mwaka huu alikuwa mkulima wa Msoga. Mwaka 1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mwaka 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.

Mwaka 1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwalimu Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia nafasi Benjamin Mkapa aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.

Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.

                                     

3. Miaka kumi ya urais

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alitangazwa tena mshindi ingawa kwa asilimia ndogo zaidi na kwa wasiwasi kuhusu uwezekano wa matokeo kuchakachuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyoiteua mwenyewe. Katiba ya nchi hairuhusu kukata rufaa dhidi ya tangazo la tume hiyo.

Katika miaka mitano iliyofuata, rais aliendelea kusafiri sana nje ya nchi, kiasi kwamba alikaa ughaibuni siku nyingi kuliko zile alizokaa nchini Tanzania.

Hali ya mwisho ya nchi ilifananishwa na mwandamizi wake John Magufuli kuwa kama "shamba la bibi", ambamo kila mtu anaweza kuchuma anavyotaka. Pia rais mpya alilalamika kwa kukuta hazina haina fedha, mbali na madeni ya kimataifa kufikia kiasi cha karibu Shilingi za Tanzania milioni 1 kwa kila mwananchi.

                                     

4. Marejeo

 • Nyangoro, Julius E. 2011. JK: A Political Biography of Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania. Trenton, NJ: Africa World Press, Inc. ISBN 1592217753.
                                     

5. Viungo vya nje

 • Government of Tanzania
 • Ippmedia Interview with Col Kikwete Archived Septemba 28, 2007 at the Wayback Machine.
 • Jakaya Kikwete Swearing-In Ceremony
 • Jakaya Kikwete Fans Website Archived Januari 30, 2008 at the Wayback Machine.
 • BBC Profile
                                     
 • Familia ya Jakaya Kikwete ni jina la kutaja familia ya Rais wa awamu ya 4 wa Tanzania Huhesabiwa kama Familia ya Kwanza ya Tanzania. Kikwete alimwoa Bi
 • Ridhiwani Jakaya Kikwete amezaliwa 16 Aprili 1979 ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi CCM Amechaguliwa
 • la Kikwete ni daraja la kuvuka Mto Malagarasi karibu na Uvinza kwenye Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania lililofunguliwa rasmi na rais Jakaya Kikwete tarehe
 • Kikwete alizaliwa tarehe 30 Novemba 1963 ni mwalimu, mwanaharakati na mwanasiasa ambaye ni mke wa aliyekuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya nne Jakaya
 • katika Bunge la Tanzania tangu mwaka wa 2000. Katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete Chiligati ni Waziri wa Ardhi. Mwaka wa 1986 alipata shahada ya pili
 • la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Alichaguliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete mwezi Septemba 2007. Kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa Mkurugenzi Mkuu
 • Tanzania tangu mwaka wa 2005, 2010 na 2015. Katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete Ghasia alikuwa Waziri wa Huduma za Umma. Mwaka wa 2003 alipata shahada
 • 2005 hadi 2010. Anatokea katika chama cha CCM. Katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete Chikawe alikuwa Waziri wa Sheria. Mwaka wa 1982 alipata shahada ya
 • kutumia dawa za kulevya. Mwaka wa 2012, Rais wa Tanzania wakati huo, Jakaya Kikwete alitoa msaada mkubwa wa fedha kwa ajili ya matibabu ya Ray C na baada

Users also searched:

historia ya jakaya mrisho kikwete, jakaya kikwete ni kabila gani,

...
...
...