Back

ⓘ Jua ni kitovu cha mfumo wa Jua wenye sayari nane, sayari vibete na magimba mengi madogo. Dunia ni sayari ya tatu katika mfumo huu. Jua ni nyota iliyo karibu na ..
Jua
                                     

ⓘ Jua

Jua ni kitovu cha mfumo wa Jua wenye sayari nane, sayari vibete na magimba mengi madogo. Dunia ni sayari ya tatu katika mfumo huu. Jua ni nyota iliyo karibu na Dunia yetu kuliko nyota nyingine zote.

                                     

1. Umbo la Jua

Umbo la Jua linakaribia kuwa tufe kamili. Maada yake ni utegili yaani gesi ya joto sana inayoshikamanishwa na nguvu ya graviti.

Kipenyo cha Jua ni takriban kilomita 1.392.684 ambayo ni mara 109 kipenyo cha Dunia yetu. Masi yake ni mara 330.000 ya masi ya Dunia. Kwa ujazo Jua ni kubwa mara milioni moja kuliko Dunia.

Kikemia masi ya Jua ni hasa hidrojeni 73% na heli 25%. Kiasi kinachobaki ni elementi nzito zaidi, kama vile oksijeni, kaboni, chuma na nyingine. Ingawa elementi nzito ni asilimia ndogo tu za masi ya Jua, kutokana na ukubwa wa Jua, elementi nzito zinalingana mara 5.000 na masi ya Dunia

                                     

2. Muundo wa Jua

Muundo wa Jua hufanywa na kanda tatu:

 • Ukanda wa myuko convection zone ambako joto la kiini linaendesha mizunguko ya utegili inayopeleka nishati kutokana kiini kwenda angahewa ya Jua
 • Ukanda wa angahewa ya Jua. Sehemu yake kubwa inaitwa tabakanuru photosphere. Tabakanuru ni asili ya nuru na joto tunazopokea duniani. Sehemu ya nje ya angahewa ni "korona" inayoonekana tu wakati wa kupatwa kwa Jua.
 • Kiini ambako atomi za hidrojeni zinayeyungana kutengeneza heli kutokana na hali ya shinikizo na joto kubwa mno;
                                     

3. Historia ya Jua

Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa Jua lilitokea takriban miaka bilioni 4.57 iliyopita katika wingu kubwa la molekuli za hidrojeni.

Kama nyota zote Jua linapitia ngazi mbalimbali katika maisha yake. Wataalamu wengi hukadiria kwamba baada ya miaka bilioni 5 ijayo akiba ya hidrojeni katika kitovu cha Jua itapungua. Halafu Jua litapanuka sana na kuwa jitu jekundu. Katika hali hii inaweza kuenea hadi njia ya obiti ya Zuhura na hakuna nafasi tena kwa uhai kwenye Dunia kutokana na joto kali.

Wataalamu wanatofautiana katika makadirio yao kama upanuzi huu utasababisha pia kupotea kabisa kwa sayari za Utaridi, Mirihi na Dunia zikimezwa na kuingia ndani ya Jua.

Baada ya miaka bilioni kadhaa ya kuwaka kama jitu jekundu, masi yake itakuwa imepungua itajikaza na kuendelea kwa muda usio mrefu kama nyota ndogo na hafifu. Kuna uwezekano mkubwa wa kwamba Jua litaendelea baadaye kama nyota kibete nyeupe White Dwarf itakayoendelea kuzimika polepole.                                     

4. Mnururisho na upepo wa Jua

Jua linatoa mwanga, joto na mnururisho mwingine wa aina mbalimbali. Sehemu ya mnururisho huu unatoka kwa umbo la chembe kama protoni na elektroni ambazo kwa jumla hujulikana pia kama upepo wa Jua. Masi ya upepo wa Jua ni takriban tani moja kwa kila sekunde. Asili ya nishati hii ni mchakato wa myeyungano wa kinyuklia ndani yake. Katika myeyungano huo hidrojeni inabadilishwa kuwa heliamu. Elementi nyingine zinatokea pia kwa kiasi kidogo. Badiliko kutoka hidrojeni kwenda heliamu inaachisha nishati inayotoka kwenye Jua kwa njia ya mnururisho.

Nishati ya mnururisho huu ni msingi wa maisha ya mimea na viumbe hai katika dunia. Nuru ya Jua inabadilishwa na mimea kwa njia ya usanisinuru kuwa nishati ya kikemia inayojenga miili yao itakayokuwa lishe tena ya mimea na wanyama.

                                     

5. Jua la utosi

Dunia yetu ina mistari ya kubuni inayowezesha kutambua maeneo mbalimbali kwa urahisi,mistari hiyo ni pamoja na mstari wa Ikweta,tropiki ya kansa na tropiki ya Kaprikoni Mstari wa Ikweta unaigawa dunia katika sehemu nbili za kaskazini na kusini,mstari huu una nyuzi 0 na unapita eneo la Afrika mashariki katika nchi za Kenya na Uganda.Mstari wa Tropiki ya kansa upo upande wa kaskazini mwa Ikweta. Mstari wa tropiki ya Kaprikoni Upo Kusini mwa Ikweta. Kipindi ambacho jua la Utosi lipo Tropiki ya kansa,eneo La Kizio cha Kaskazini Huwa na joto,kwa kuwa hewa ikipata joto hutanuka hivyo huwa na mgandamizo mdogo wa hewa.Pepo huvuma kuelekea huko.

                                     

6. Upepo

Pepo hizi huvuma kutoka kusini-mashariki kuanzia mwezi desemba wakati jua la utosi linapokuwa tropiki ya kaprikoni kipindi hiki kizio cha kusini huwa na joto na Pepo huvuma kutoka kusini-mashariki.Pia hali hiyo husababisha mabadiliko ya upatikanaji wa mvua na hali ya joto katika eneo la Afrika Mashariki. Maeneo ya Ikweta yana tabia ya Kiikweta ya kuwa na mvua nyingi na joto jingi.Kusini na Kaskazini mwa eneo lenye tabia ya Kiikweta kuna tabia ya kitropiki yenye majira mawili makuu ya mwaka.Majira hayo ya mwaka ni masika na kiangazi.Lakini katika maeneo ya pwani majira ya mwaka hugawanyika katika sehemu nne ambazo ni vuli,kipupwe,masika na kiangazi.

                                     

7. Mwinuko

Afrika Mashariki ina mwinuko wa meta 0 kutoka usawa wa bahari hadi kufika meta 4600.Maeneo ya pwani mwinuko wake ni kuanzia meta 0 hadi meta 500 kutoka usawa wa bahari. Wastani wa jotoridi ni nyuzi za sentigredi 26.Joto hupungua kadiri unavyoelekea bara.Meta 1500 Kutoka usawa wa bahari ni nyuzi za sentigredi 22 ambapo ni wastani wa joto linalopatikana katika maeneo ya Tabora.Maeneo ya mlima mrefu kama kilimanjaro wenye urefu wa meta 5895 huwa na jotoridi la chini ya nyuzi za sentigredi 0

                                     

8. Maziwa na bahari

Maeneo yaliyo kandokando ya maziwa na bahari huwa na unyevunyevu na mvua nyingi.Mara nyingi maeneo yanayozunguka bahari na maziwa mfano Ziwa Viktoria na Bahari ya Hindi yana tabia ya nchi ya aina moja.Maeneo hayo kwa kawaida hupata mvua nyingi.

                                     

9. Uoto wa misitu

Maeneo yenye misitu hupata mvua nyingi kwani mawingu huweza kufanyika kwa urahisi.Misitu hiyo pia huifadhi unyevu usipotee ardhini kwa urahisi kwa njia ya mvukizo.

                                     

10. Pepo

Pepo za msimu za Kaskazini-mashariki Huleta Mvua kidogo katika eneo kubwa la kenya na kaskazini mwa Tanzania. Pepo huvuma sambamba na pwani.Pepo hizi pia huvuma kutoka sehemu kubwa ya nchi kavu katika nchi ya Ethiopia na Sudani kabla ya kufika eneo la Afrika Mashariki.

                                     

11. Viungo vya Nje

 • A collection of spectacular images of the Sun from various institutions The Boston Globe
 • Satellite observations of solar luminosity
 • Astronomy Cast: The Sun
 • The Swedish 1-meter Solar Telescope, SST
 • Sun in Ultra High Definition NASA 11 January 2015
 • An animated explanation of the structure of the Sun Archived Agosti 10, 2011 at the Wayback Machine. University of Glamorgan
 • Album of images and videos by Seán Doran, based on SDO imagery
 • Solar Conveyor Belt Speeds Up – NASA – images, link to report on Science
 • NASA 5-year timelapse video of the Sun
 • Nasa SOHO Solar & Heliospheric Observatory satellite
 • Animation – The Future of the Sun
 • National Solar Observatory
 • Sun|Trek, an educational website about the Sun
                                     
 • Upepo wa jua kwa Kiingereza solar wind ni jina la mkondo mfululizo wa chembe za nyuklia unaotoka katika Jua Chembe za nyuklia ni vipande vidogo vinavyopatikana
 • Mfumo wa Jua en: solar system ni mpangilio wa Jua letu, sayari na sayari kibete zinazolizunguka pamoja na miezi yao, asteroidi, meteoridi, kometi na
 • Kalenda ya jua ni kalenda inayofuata mwendo wa jua jinsi inavyoonekana angani. Hali halisi tunaona matokeo ya mwendo wa dunia kuzunguka jua Katika kalenda
 • Masi ya Jua ing. Solar mass inataja masi ya Jua letu ambayo ni takriban kilogramu 1.99 1030 Hii inalingana na masi ya Dunia yetu mara 332, 946. Kiwango
 • Kupatwa kwa Jua kwa Kiingereza solar eclipse ni hali ya Jua kutoonekana au kuonekana kwa sehemu tu angani wakati wa mchana kwa muda fulani hata pasipo
 • Nusukipenyo cha Jua ing. solar radius ni nusu ya kipenyo cha Jua letu na hivyo sawa na umbali wa kilomita 696.342 au mara 109 nusukipenyo cha Dunia.
 • Madoa ya Jua ni sehemu kwenye uso wa Jua zinazoonekana nyeusi - nyeusi katika darubini ya mtazamaji. Madoa makubwa yanaweza kutazamiwa pia wakati wa machweo
 • Mng aro wa Jua kwa Kiingereza: luminosity of the Sun ni jumla ya mng aro au mnururisho wa sumakuumeme unaotoka kwenye Jua na kuelekea nje yake katika
 • Kalenda ya jua - mwezi kwa Kiingereza: lunisolar calendar ni kalenda inayotumia awamu za Mwezi pamoja na mwaka wa jua Kalenda ya Kiyahudi na ya Kichina

Users also searched:

...
...
...