Back

ⓘ Mtakatifu Ireneo alikuwa askofu wa mji wa Lyon nchini Ufaransa. Ametambuliwa tangu kale kuwa mtakatifu kama mfiadini. Sikukuu yake ni tarehe 28 Juni. ..
Mtakatifu Ireneo
                                     

ⓘ Mtakatifu Ireneo

Mtakatifu Ireneo alikuwa askofu wa mji wa Lyon nchini Ufaransa.

Ametambuliwa tangu kale kuwa mtakatifu kama mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Juni.

                                     

1. Maisha

Ireneo alizaliwa yapata mwaka 130.

Alilelewa katika mji wa Smirna leo Izmir nchini Uturuki, akiwa ni mwanafunzi wa Mt. Polikarpo aliyekuwa askofu wa mji huo baada ya kuwa mfuasi wa Mtume Yohane.

Mwaka 177, baada ya kuhamia Ufaransa, Ireneo alipata upadrisho huko Lyons, na baada ya kutumwa kidogo Roma kama mjiumbe kwa Papa, akinusurika hivyo kuuawa katika dhuluma dhidi ya Wafiadini wa Lyon, aliteuliwa kuwa askofu wa hapo.

Ni muhimu kwa juhudi zake za kupigania umoja wa Kanisa dhidi ya uzushi, akisisitiza umuhimu wa mlolongo wa kitume wa maaskofu, akitoa kama mfano orodha ya wale wa Kanisa la Roma baada ya Mtume Petro. Alidai makanisa yalingane na imani ya Kanisa hilo.

Katika maandishi yake alijitahidi sana kutetea imani ya Kanisa Katoliki inayotegemea mapokeo ya Mitume wa Yesu dhidi ya mafundisho ya Wagnosi yaliyotegemea ujuzi ambao yeyote alidai kuwa nao akianzisha kikundi chake.

Ni wa kwanza pia kushuhudia Injili nne kuwa Neno la Mungu.

Kwa mujibu wa mapokeo, aliifia dini yake mnamo mwaka 200.

                                     

2. Marejeo

 • Minns, Denis 1994. Irenaeus. Washington, D.C.: Georgetown University Press. ISBN 0878405534.
 • Eusebius 1932. The Ecclesiastical History, Kirsopp Lake and John E.L. Oulton, trans, New York: Putnam.
 • 1885 The Ante-Nicene Fathers. Buffalo, NY: The Christian Literature Company.
 • Wolfson, Henry Austryn 1970. The Philosophy of the Church Fathers: Faith, Trinity, Incarnation. Cambridge, MA: Harvard University Press.
 • Schaff, Philip 1980. History of the Christian Church: Ante-Nicene Christianity, A.D. 100-325. Grand Rapids, Mich: Eerdmans. ISBN 0802880479.
 • Payton Jr., James R. Irenaeus on the Christian Faith: A Condensation of Against Heresies.
 • Hägglund, Bengt 1968. History of Theology, Gene J.Lund, trans, St. Louis: Concordia Publishing.
 • Tyson, Joseph B. 1973. A Study of Early Christianity. New York: Macmillan.
 • Quasten, J. 1960. Patrology: The Beginnings of Patristic Literature. Westminster, MD: Newman Press.
                                     

3. Viungo vya nje

 • Book II, ch. 22, where Irenaeus argues his unconventional views about the age of Jesus and the length of his ministry.
 • A nineteenth-century translation of Irenaeus work
 • Fragments from his lost works
 • Demonstration of the Apostolic Preaching
 • Early Christian Writings Irenaeus
 • EarlyChurch.org.uk Extensive bibliography.
 • "St. Irenæus, Bishop of Lyons, Martyr", Butlers Lives of the Saints
 • Opera Omnia by Migne Patrologia Graeca with analytical indexes
 • Gregory S. Neal: "The Nature of Evil and the Irenaean Theodicy" Grace Incarnate 1988 Archived Februari 7, 2010 at the Wayback Machine.
 • Critique of Irenaeus, Elaine H. Pagels
 • Critique of Pagels article by Father Paul Mankowski
                                     
 • 204 Makala hii inahusu mwaka 200 BK Baada ya Kristo bila tarehe Mtakatifu Ireneo Askofu wa Lyons Wikimedia Commons ina media kuhusu: 200
 • 134 Makala hii inahusu mwaka 130 BK Baada ya Kristo bila tarehe Mtakatifu Ireneo Askofu wa Lyons Wikimedia Commons ina media kuhusu: 130

Users also searched:

...
...
...