Back

ⓘ Johannes Gutenberg. Johannes Gensfleisch zur Laden zum Gutenberg, anayejulikana kifupi kama Johannes Gutenberg, alikuwa fundi dhahabu na mvumbuzi kutoka Ujeruma ..
Johannes Gutenberg
                                     

ⓘ Johannes Gutenberg

Johannes Gensfleisch zur Laden zum Gutenberg, anayejulikana kifupi kama Johannes Gutenberg, alikuwa fundi dhahabu na mvumbuzi kutoka Ujerumani anayekumbukwa hasa kama mbuni wa uchapaji vitabu kwa herufi za kusogezeka.

Alitengeneza mashine ya kwanza ya kuchapa vitabu, alibuni aloi ya kufaa kwa herufi alizotumia katika mashine hii pamoja na wino.

Alitengeneza pia kifaa kilichomwezesha kusubu herufi za metali haraka.

                                     

1. Vitabu kabla ya Gutenberg

Kabla ya Gutenberg vitabu vingi viliandikwa kwa mkono. Kunakili kitabu kimoja kama Biblia kwa mkono kulichukua angalau mwaka mmoja.

Teknolojia ya kuchapisha vitabu ilipatikana tayari lakini haikuridhisha. Kwa kawaida ukurasa wote ulichorwa halafu kukatwa katika ubao. Ubao ulipakwa wino na karatasi zilisukumwa kwenye ubao huu. Shida zilikuwa: kwanza kazi kubwa ya kutengeneza bao, halafu bao hizi hazikudumu sana.

                                     

2. Teknolojia mpya

Mbinu ya Gutenberg ilikuwa hasa kutumia herufi metalia za kusogezeka.

Metali inadumu kuliko ubao ikamwezesha Gutenberg kuandaa ukurasa na kuuchapisha mara maelfu. Aliweka maandishi kwa kuandaa herufi metalia nyingi alizounganisha kuwa maneno, mistari hadi ukurasa wote.

Ukurasa ulibanwa pamoja ukawa tayari kwa uchapishaji. Kama makosa yalionekana au mabadiliko yalihitajika aliweza kufungua ukurasa, kuongeza au kutoa herufi na kubana ukurasa upya.

Alitengeneza herufi kwa kumwaga aloi ya plumbi metali ya risasi, stani na antimoni katika kalibu ilipopoa. Kwa njia hii aliweza kusubu herufi nyingi zilizokuwa sawa kabisa, tofauti na herufi zilizokatwa kwa mkono katika ubao.

Baada ya kupanga herufi na kuzibana aliweza kuchapisha ukurasa mara nyingi jinsi ilivyohitajika. Aliweza pia kufungua mbano wa ukurasa na kutumia herufi kwa kazi nyingine au kutunza ukurasa kwa marudio yaliyotarajiwa.

Pamoja na hayo alibuni mgandamizo uliokuwa mashine bora ya kuchapa vitabu.

                                     

3. Matokeo ya kazi ya Gutenberg

Uvumbuzi huo wote ulianzisha mapinduzi ya teknolojia na utamaduni. Vitabu vilianza kupatikana haraka kuliko awali. Bei ya vitabu ilishuka. Baada ya kuongezeka kwa vitabu, watu wengi zaidi walianza kusoma. Shule zilienea kushinda zamani.

Teknolojia ya Gutenberg iliwezesha uenezi wa harakati ya matengenezo ya kiprotestanti iliyoanzishwa na Martin Luther mwaka 1517. Maandiko ya Luther yalisambaa haraka kote Ulaya. Maandiko ya wafuasi na wapinzani wake yalifuata. Watu wengi walishiriki na kufuatilia habari hizi.

Gutenberg amehesabiwa kati ya watu 100 wa historia ya dunia wenye athira kubwa. Gazeti la Newsweek alimteua kama "Mtu wa milenia 1000-2000".

                                     

4. Vyanzo

 • Duchesne, Ricardo 2006. "Asia First?". The Journal of the Historical Society 6 1: 69–91.
 • Childress, Diana 2008. Johannes Gutenberg and the Printing Press. Twenty-First Century Books. ISBN 978-0-7613-4024-9.
 • Wolf, Hans-Jürgen 1974. Geschichte der Druckpressen 1st ed. Frankfurt/Main: Interprint
 • Juchhoff, Rudolf 1950. "Was bleibt von den holländischen Ansprüchen auf die Erfindung der Typographie?". Gutenberg-Jahrbuch: 128−133
                                     

5. Marejeo

 • Man, John 2002. The Gutenberg Revolution: The Story of a Genius and an Invention that Changed the World. Headline Review. ISBN 978-0-7472-4504-9.
 • McLuhan, Marshall 1962. The Gutenberg Galaxy: The Making of Typographic Man, 1st, University of Toronto Press. ISBN 978-0-8020-6041-9.
 • 1997 The Coming of the Book: The Impact of Printing 1450-1800. Verso. ISBN 1-85984-108-2.
 • Blake Morrison, The Justification of Johann Gutenberg 2000
                                     

6. Viungo vya nje

 • The Digital Gutenberg Project: the Gutenberg Bible in 1.300 digital images, every page of the University of Texas at Austin copy.
 • English homepage of the Gutenberg-Museum Mainz, Germany.
 • Treasures in Full – Gutenberg Bible View the British Librarys Digital Versions Online
                                     
 • kutumia kalamu kwa sababu hii vilikuwa vichache na bei ilikuwa juu. Johannes Gutenberg alibuni mashine ya kuchapisha vitabu iliyofanikiwa na kurahisisha
 • kamusi elezo au ensaiklopedia zimekuwa na athari kubwa sana tangu Johannes Gutenberg na kupatikana kwa uchapaji wa vitabu ulioshusha kabisa bei ya vitabu
 • Mwanzilishi wa teknolojia hii mpya alikuwa fundi dhahabu na mfanyabiashara Johannes Gutenberg kutoka mji wa Mainz katika Ujerumani. Alibuni njia sawa jinsi walivyowahi
 • cha Ulaya kilianzishwa Fabriano Italia kabla ya mwaka 1264. Tangu Johannes Gutenberg abuni mashine ya kuchapa vitabu, mahitaji ya karatasi yaliongezeka
 • Ludwig van Beethoven Papa Benedikto XVI Johannes Brahms Johann Wolfgang von Goethe Günter Grass Johannes Gutenberg Georg Wilhelm Friedrich Hegel Henri II
 • tena aliamini jua ni kitovu chake na kwamba Nicolaus Copernicus pamoja na Johannes Kepler waliwahi kusema ukweli. Mwanzoni Papa Urban VIII aliyefuatilia

Users also searched:

...
...
...