Back

ⓘ Karen Blixen. Karen Christence Blixen-Finecke alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Alitumia pia majina ya Tania Blixen, kwenye nchi zinazozungumza Kijeruma ..
Karen Blixen
                                     

ⓘ Karen Blixen

Karen Christence Blixen-Finecke alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Alitumia pia majina ya Tania Blixen, kwenye nchi zinazozungumza Kijerumani, Osceola na Pierre Andrézel.

Aliishi Kenya -wakati ule: Afrika ya Mashariki ya Kiingereza- kati ya 1913 hadi 1931 akiongoza shamba la kahawa karibu na mji wa Nairobi. Eneo la shamba lake la zamani hadi leo laitwa "Karen" ni kitongoji cha Nairobi.

Aliandika kumbukumbu ya maisha yake Kenya na kitabu hiki kikawa msingi wa filamu "Out of Africa". Huko Denmark alijulikana sana kwa kazi yake iitwayo Seven Gothic Tales.

Karen Dinesen alizaliwa Rungstedlund, kaskazini mwa Copenhagen. Baba yake, Wilhelm Dinesen 1845–1895, alikuwa ni mwandishi na ofisa wa kijeshi toka familia ya wamiliki wa mashamba ya Jutland yenye uhusiano wa karibu na ufalme, kanisa na siasa za mrengo wa kulia. Mama yake, Ingeborg Westenholz 1856–1939, alitoka kwenye familia tajiri inayofanya biashara. Karen Dinesen alikuwa ni mtoto wa pili kati ya watoto watatu wa kike na wawili wa kiume. Mdodo wake wa kiume, Thomas Dinesen, alipata tuzo ya Victoria Cross wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Dinesen was known to her friends as "Tanne".

                                     

1. Vitabu

 • Shadows on the Grass 1960 Uingereza na Denmark, 1961 Marekani
 • Sandhedens hævn – En marionetkomedie, Mei 1926, akitumia jina la Karen Blixen-Finecke
 • Winters Tales 1942
 • Ehrengard baada ya kufa 1963, Marekani
 • Last Tales 1957
 • Plojeren The Ploughman, Oktoba 1907, kwa jina la Gads danske Magasin,akitumia jina la Osceola
 • Anecdotes of Destiny 1958 pamoja na Babettes Feast
 • Out of Africa 1937 Denmark na Uingereza, 1938 nchini Marekani
 • The Angelic Avengers 1946
 • Letters from Africa, 1914–1931 baada ya kufa 1981, Marekani
 • Eneboerne The Hermits, Agosti 1907, kilichapishwa kwa jina la Tilskueren kwa jina lake la uandishi Osceola
 • Carnival: Entertainments and Posthumous Tales baada ya kufa 1977, Marekani
 • On Modern Marriage and Other Observations baada ya kufa 1986, Marekani
 • Seven Gothic Tales 1934 nchini Marekani, 1935 nchini Denmark
 • Familien de Cats The de Cats Family, Januari 1909, kwa jina la Tilskueren akitumia jina la Osceola
 • Karen Blixen in Danmark: Breve 1931–1962 baada ya kufa1996, Denmark
 • Karen Blixen i Afrika. En brevsamling, 1914–31 i IV bind baada ya kufa 2013, Denmark
 • Daguerreotypes and Other Essays baada ya kufa 1979, Marekani
                                     

2. Viungo vya nje

 • Jumba la Makumbusho la Karen Blixen Archived Desemba 24, 2007 at the Wayback Machine., Kenya
 • Tovuti ya Karen Blixen – Isak Dinesen
 • Wasifu mfupi wa Isak Dinesen/Karen Blixen Archived Oktoba 30, 2007 at the Wayback Machine.
 • Jumba la Makumbusho la Karen Blixen Archived Machi 14, 2006 at the Wayback Machine., Denmark
 • Karen Blixens Kenya Archived Agosti 13, 2007 at the Wayback Machine.
                                     
 • Gummer, Miranda Otto, Sonja Richter, Jo Harvey Allen, Hailee Steinfeld, and Karen Jones. Shared with Carey Mulligan, Helena Bonham Carter, Anne - Marie Duff

Users also searched:

...
...
...