Back

ⓘ Jumba la Sultani, Zanzibar. Jumba la Sultani ni jengo la kihistoria kwenye Mji Mkongwe wa Zanzibar. Linapatikana kando ya mtaa wa Mizingani likitizamana na baha ..
Jumba la Sultani, Zanzibar
                                     

ⓘ Jumba la Sultani, Zanzibar

Jumba la Sultani ni jengo la kihistoria kwenye Mji Mkongwe wa Zanzibar. Linapatikana kando ya mtaa wa Mizingani likitizamana na bahari, na Jumba la Maajabu lililoko jirani. Lilikuwa makazi ya Sultani wa Zanzibar kuanzia mwaka 1911 hadi mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964. Leo hii ni jumba la makumbusho.

                                     

1. Jumba la ukingoni

Jengo hili lilijengwa mahali pa jumba lililotangulia kuwa makazi ya masultani. Jumba hilo lilijulikana kwa jina la Kiarabu "Bait as-Sahel" Kiarabu: بيت الساحل bait as-sahel, au "Jumba la Ukingoni". Bait as Sahel ilijengwa kwenye miaka 1827-1834 kwa ajili ya Sultani Said. Mpelelezi Mwingereza Richard Burton aliiona mwaka 1872 akaandika lilikuwa jengo refu la ghorofa mbili, lenye kuta nyeupe na paa la vigae vya rangi ya kijani.

Burton aliandika kwamba mizinga 8 ilikaa mbele ya jumba kando ya bahari. Kuwepo kwa mizinga hiyo moja kwa moja mbele ya jengo kulisababisha pia kuharibika kwa jumba katika vita ya Uingereza dhidi Zanzibar mwaka 1896 ambako manowari za Waingereza walilenga kwanza kunyamazisha sehemu zote zenye mizinga na askari.

                                     

2. Jumba jipya baada ya 1896

Nyumba mpya ilijengwa mahali pa mtangulizi wake kwa kutumia ukuta uliokuwa umebaki. Jumba la Sultani ni jengo lenye ghorofa tatu na kuta nyeupe. Mwanzoni lilikaliwa na familia ya Sultani, na mnamo mwaka 1911sultani mpya Khalifa bin Harub aliingia hapa akikaa hadi kifo chake mwaka 1960. Mwanawe sultani Abdullah bin Khalifa aliishi pia hapa hadi mapinduzi ya mwaka 1964.

Baadaye jina likabadilishwa kuwa Jumba la Wananchi Peoples Palace nalo likatumiwa kama ofisi za serikali. Mwaka 1994 likabadilishwa kuwa jumba la makumbusho

                                     

3. Jumba la makumbusho

Ghorofa moja la jumba la makumbusho limewekwa wakfu kwa Sultani Khalifa bin Harub; nyingine kwa Sayyida Salme, anayejulikana kama Emily Ruete, aliyekuwa binti mmojawapo wa sultani aliyetoroka na mpenzi wake Mjerumani akawa mke wake na kuishi Ulaya. Maonyesho ni pamoja na vitabu na barua zake, nguo na vifaa vya maisha ya kila siku. Vitu kadhaa vya fenicha na mali nyingine kwa familia ya sultani ziko kwenye maonyesho ili kuwapa wageni picha ya maisha ya kifalme Zanzibar wakati wa karne ya 19.

                                     
  • ya mapinduzi ya Zanzibar na muungano na Tanganyika uliozaa Tanzania. Makala kuu: Said bin Sultani Usultani ulianzishwa wakati Sultani Sayyid Said alipoamua
  • iliporomoka. Jumba hilo lilijengwa mnamo mwaka 1883 kwa amri ya Barghash bin Said, Sultani wa pili wa Zanzibar Ilikusudiwa kuwa jumba la sherehe na ukumbi
  • ya Zanzibar zilizolengesha bunduki zake kwa jumba la sultani Saa 9.02 zilianza kulipiga jumba la sultani na kikosi cha wanajeshi kilishambulia jumba Saa
  • kikosi cha ulinzi wa jumba lake. Jeshi rasmi la Zanzibar lilikuwa chini ya Mwingereza Lloyd Mathews ambaye hakumtambua Khaled kama sultani akaweka kikosi chake
  • 1830 wakati Sultani Sayyid Said alipohamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja Unguja. Kati ya majengo maarufu ni Beit al Ajaib yaani Jumba la Maajabu lililobomoka
  • mama zao. Sultani wa pili wa Zanzibar yenyewe, Sayyid Bargash, alijitahidi kujenga uhusiano na nchi za nje. Alifunga soko la watumwa Zanzibar mjini kulingana
  • lililobomoka tarehe 24 Desemba 2020 Jumba la Sultani Ngome Kongwe, Kanisa Kuu la Anglikana lililojengwa mahali pa soko la watumwa na hasa nyumba nyingi za
  • Mkongwe wa Zanzibar Tanzania. Bustani ziko kando ya mtaa wa Mizingani unaopita ukingo wa bahari ya Mji Mkongwe, mbele tu ya majengo ya Jumba la Maajabu
  • karibu na jengo lingine la kihistoria la jiji, Jumba la Maajabu Ikulu ya zamani ya Sultani wa Zanzibar na inatazamana na Forodhani Gardens. Ilijengwa

Users also searched:

...
...
...