Back

ⓘ Jiografia ya Afrika inahusu bara hilo ambalo ni la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30.368.609 na vilevile kwa idadi ya wak ..
Jiografia ya Afrika
                                     

ⓘ Jiografia ya Afrika

Jiografia ya Afrika inahusu bara hilo ambalo ni la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30.368.609 na vilevile kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1.275.920.972. Asia ndiyo bara pekee la kushinda Afrika.

Kuna umbali wa kilomita 8.000 kutoka Ras ben Sakka nchini Tunisia 37°21 N, sehemu ya kaskazini kabisa hadi rasi ya Cape Agulhas nchini Afrika Kusini 34°5115" S, sehemu ya kusini kabisa.

Umbali ni km 7.400 kutoka upande wa magharibi rasi ya Cape Verde, 17°3322" W hadi mashariki Ras Hafun nchini Somalia, 51°2752" E.

Mlima mrefu zaidi barani unapatikana nchini Tanzania: ni volkeno Kilimanjaro mita 5.895 juu ya usawa wa bahari ambao ni pia mlima mrefu kuliko yote duniani usiojitokeza katika safu ya milima.

Mto mrefu zaidi barani na duniani ni Naili ukiwa na mwendo wa kilometa 6.758 kuanzia nchini Rwanda na Burundi, kupitia Tanzania, Uganda, Kenya, Sudan Kusini, Ethiopia, Sudan na hatimaye Misri.

Katika mwendo wake wa awali maji ya Naili yanakusanyika katika ziwa Nyanza/Viktoria ambalo ni pana kuliko yote barani na la pili duniani likiwa na kilometa mraba 59.947.

Afrika imezungukwa na bahari karibu pande zote. Kuna kiungo chembamba cha nchi kavu upande wa kaskazini mashariki na bara la Asia kwenye rasi ya Sinai.

Upande wa kaskazini iko Bahari ya Mediteranea, upande wa mashariki kuna Bahari Hindi pamoja na Bahari ya Shamu na upande wa magharibi iko Bahari Atlantiki.

Pwani yote ya Afrika ina urefu wa kilomita 26.000.

Kuna kisiwa kikubwa cha Madagaska na funguvisiwa mbalimbali.

                                     

1. Jiolojia

Kijiolojia Afrika iko kwenye bamba la Afrika. Lile bamba la gandunia la Afrika linaenea mbali zaidi kuliko maeneo tunayotazama kuwa Afrika kijiografia, ni pamoja na maeneo chini ya bahari linapopakana na mabamba ya Ulaya-Asia, Uarabuni, Uhindi na Australia, Antaktika, Amerika ya Kusini na Kaskazini. Upande wa mashariki wa bamba la Afrika kuna ufa unaozidi kupanuka ikielekea kujitenga kutoka Afrika kama bamba la Somalia.

                                     

2. Tabianchi

Tabianchi ya Afrika ni pana, kuanzia kanda za tropiki hadi kufikia maeneo ya nusu-aktiki baridi kwenye ncha za milima mirefu.

Nusu ya kaskazini ya bara ni jangwa au angalau yabisi. Sehemu za kati na za kusini zina maeneo ya savanna na kanda za msitu wa mvua.

Afrika ni bara lenye joto kuliko mabara yote na asilimia 60 za uso wake ni maeneo yabisi au jangwa.

                                     

3. Nchi za Afrika

Barani kuna nchi huru 54 zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa, maeneo 9 yenye hali ya pekee na madola mawili ambayo yanajitawala bila kutambuliwa kimataifa.

Nchi kubwa ya Afrika ni Algeria na nchi ndogo ni Shelisheli, funguvisiwa la Bahari Hindi. Nchi ndogo Afrika bara ni Gambia.

                                     

4. Wakazi

Wataalamu wengi wanakubaliana kutambua Afrika kama asili ya binadamu wote walioko duniani.

Mwaka 2010 idadi ya wakazi wa nchi zote za Afrika ilipita bilioni 1. Ni kwamba idadi yao imeongezeka sana katika miaka 40 iliyopita, ikipiku zile za Ulaya na Amerika.

Ilhali mwaka 1950 walikuwepo Waafrika milioni 229 pekee, idadi iliongezeka kuwa milioni 630 mwaka 1990 na milioni 1200 mnamo 2014.

Hivyo asilimia ya watoto na vijana ni kubwa. Kuna nchi kadhaa ambako zaidi ya nusu ya wananchi wako chini ya umri wa miaka 25. Wakazi wa Afrika ni vijana kuliko wale wa mabara mengine yote; mwaka 2012 umri wa wastani ulikuwa miaka 19.7, wakati kidunia ulikuwa 30.4.

Zaidi ya lugha elfu za Kiafrika zinazungumzwa barani leo, ingawa nyingi zinazidi kufifia.

Waafrika wana imani za dini nyingi tofauti, lakini takwimu zinazotolewa hazina hakika, pia kwa sababu suala hilo ni nyeti kisiasa kwa serikali zenye mchanganyiko mkubwa wa watu, kama vile Nigeria, Ethiopia na Tanzania.

Kadiri ya World Book Encyclopedia, Islam ndiyo inayoongoza, ikifuatwa na Ukristo. Kumbe kadiri ya Encyclopedia Britannica, 45% za wakazi ni Wakristo, 40% ni Waislamu na 10% wanafuata dini asilia za Kiafrika. Wachache tu ni Wahindu, Wabuddha, Wabahai au hawana dini yoyote.                                     

5. Tazama pia

 • Orodha ya milima ya Afrika
 • Historia ya Afrika
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
 • Mito mirefu ya Afrika
 • Maziwa ya Afrika
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
                                     

6. Viungo vya nje

 • Africa: The Human Footprint". Interactive map of human impact on Africa by National Geographic.
 • The Index on Africa from The Norwegian Council for Africa
 • Africa South of the Sahara from Stanford University
 • Wikimedia Atlas of Africa
 • Africa - Interactive Map with demographics and geopolitical information" from the United States Army Africa
 • Aluka Digital library of scholarly resources from and about Africa
 • Jiografia ya Afrika katika Open Directory Project
 • African & Middle Eastern Reading Room from the United States Library of Congress
                                     
 • na mlima Kenya, ulio wa pili kwa urefu barani Afrika Makala kuu: Jiografia ya Kenya Kenya ni nchi ya 47 kwa ukubwa duniani ikifuata mara Madagaska 580
 • mkuu wa milki ya Austria - Hungaria. Babake alifanya kazi ya benki. Oskar alipita shule za msingi na sekondari akaanza masomo ya jiografia kwenye Chuo Kikuu
 • magharibi ya kati na Kenya Ghuba ya Aden nayo iko mashariki. Mji mkuu na mji mkubwa zaidi ni Mogadishu wakazi 2, 120, 000 Makala kuu: Jiografia ya Somalia
 • upande wa kaskazini hadi kanda la Sahel upande wa kusini. Wataalamu wa jiografia husema Sahara haikuwa hivyo wakati wote. Kutokana na utafiti wa dalili
 • Ziwa Mobutu Sese Seko - ni moja ya maziwa makubwa ya Afrika Ni ziwa kubwa la saba katika Afrika likiwa na nafasi ya ishirini na saba kwa ukubwa katika
 • 1 Jiografia ya Mayotte Watu wa Mayotte Siasa ya Mayotte Uchumi wa Mayotte Mawasiliano ya Mayotte Maeneo ya ng ambo ya Ufaransa Wizara za serikali ya Ufaransa

Users also searched:

ramani ya afrika mashariki,

...
...
...