Back

ⓘ Kale ya Washairi wa Pemba ni kitabu kilichokusanya mashairi ya kale ya Wazanzibari yaliyoandikwa na washairi wawili walioishi mwishoni mwa karne ya 18 na mwanzo ..
                                     

ⓘ Kale ya Washairi wa Pemba

Kale ya Washairi wa Pemba ni kitabu kilichokusanya mashairi ya kale ya Wazanzibari yaliyoandikwa na washairi wawili walioishi mwishoni mwa karne ya 18 na mwanzoni mwa karne ya 19. Washairi hao waNAjulikana kama Kamange na Sarahani na mashairi yao kukusanywa na Abdulrahman Saggaf Alawy na kuhaririwa na Abdilatif Abdalla mshairi wa mashairi ya Sauti ya dhiki na kisha kuchapishwa na Mkuki na Nyota mwaka 2011.

Kitabu hicho kimeelezea hali ya utawala ilikuwepo katika karne hizo mbili katika visiwa vya Pemba na Zanzibar; pamoja na kuelezea siasa kimeelezea pia namna washairi walivyoishi katika karne ya 19 na mwanzo wa karne ya 20.

Kitabu kimeelezea pia namna mashairi mengi yalivyopotea kwa kuchomwa moto wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar na kusababisha kumbukumbu nyingi za tungo hizo za kale kupotea.

Katika kuyaelezea maisha ya kiutunzi kwa washairi kitabu hiki kimeelezea namna washairi hao wawili walivyoweza kuishi kwa kuandikiana mashairi mara kwa mara hadi watu kuhisi kulikuwa na ugomvi baina ya Kamange na Sarahani. Pia kitabu kimeonyesha matumizi ya lugha na ufundi wa kutunga ambao kila mshairi anapaswa kuwa nao.

                                     
  • Novemba 1982 alikuwa mwanachuoni na mwanahistoria mkubwa wa Kiislamu na mmojawapo wa washairi wakubwa kutoka Zanzibar lakini baadaye alihamia Mombasa

Users also searched:

...
...
...